Mtaa wa Nyerere kutinga Palestina

Mtaa wa Nyerere kutinga Palestina

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803

HABARI
[h=1][/h]

Na Zacharia Osanga (
email the author)

Posted Jumatatu,Januari21 2013 saa 22:29 PM

KWA UFUPI

“Sababu kubwa za kuipa barabara hii jina hili ni kuwa Rais Arafat alizuru mara kadhaa hapa Tanzania akialikwa na Mwasisi wa Taifa lenu Mwalimu Nyerere. Uhusiano huu uliendelea baada ya Rais Ali Hassan Mwinyi kuchukua madaraka na baadaye Rais Mkapa” alisema Balozi Abujaish.

JINA la Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ni miongoni mwa majina yatakayotumika kuitambulisha mitaa ya Makao Makuu ya Mamlaka ya Palestina, Ramallah.

Hayo yalithibitishwa na Balozi wa Palestina hapa nchini, Nasri Abujaish wakati wa hafla ya kuzindua jina la Barabara ya Yasser Arafat, iliyopo Oysterbay jijini Dar es Salaam jana.

Abujaish alisema Mwalimu alikuwa na uhusiano mzuri na kiongozi huyo wa zamani wa Mamlaka ya Palestina ambaye pia alikuwa Rais wa kwanza wa Chama cha Ukombozi wa Palestina (PLO).

“Sababu kubwa za kuipa barabara hii jina hili ni kuwa Rais Arafat alizuru mara kadhaa hapa Tanzania akialikwa na Mwasisi wa Taifa lenu Mwalimu Nyerere. Uhusiano huu uliendelea baada ya Rais Ali Hassan Mwinyi kuchukua madaraka na baadaye Rais Mkapa” alisema Balozi Abujaish.

Balozi wa Taifa hilo linalopigana vita visivyoisha kati yake na Israel aliwaambia waandishi wa habari waliohudhuria hafla hiyo kuwa, Arafat ndiye aliyeanzisha upinzani dhidi ya Taifa hilo dogo la Mashariki ya Kati kudai ardhi yao wanayoikalia kimabavu kwa zaidi ya miongo mitano sasa.

“Ni matumaini yangu kuwa kwa kufanya hivi tutaweka kumbukumbu zetu na vizazi vijavyo kuwa hai kwa waasisi wa mataifa yetu”

Abujaish aliongeza kuwa kiongozi huyo aliyefariki Novemba 2004 wakati akitibiwa katika hospitali moja ya kijeshi nchini Ufaransa, ndiye chimbuko la maono ya kutaka Palestina itambuliwe kama Taifa huru.

Alisema kuwa ingawa Arafat hayupo, lakini msingi aliouweka umezaa matunda kwa Palestina kutambuliwa kama Taifa ingawa siyo mwanachama wa Umoja wa Mataifa (UN), lakini mapambano yataendelea hadi ardhi yao ipatikane na Palestina kuwa mwanachama kamili wa UN.

Balozi huyo alisema uhusiano wa Tanznaia kwa Palestina upo kwa jinsi wanavyoshikamana na kuwaunga mkono katika mapambano yao dhidi wakoloni wa ardhi yao kama ambavyo walifanya wakati wa ubaguzi wa rangi huko Afrika Kusini.

Katika hafla hiyo Diwani wa Kata ya Kigogo, Richard Chengula aliyemwakilisha Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda, alisema kuwa wananchi wa Oysterbay ndiyo waliamua barabara hiyo iliyokuwa ikiitwa Hill Road kupewa jina hilo kutokana na kuwa karibu na makazi ya Balozi wa Palestina.

Yeah GOOD... Alikuwa anatetea sana FREEDOM FIGHTERS...
 
nngu007 mbona kichwa cha habari na na habari yenyewe haviendani.

Au mie ndio sijaelewa!
 
Last edited by a moderator:
Akili za kitumwatumwa hizi sijui zitaishaga lini vichwani mwetu. "Yasser Arafat" road? huyuhuyu Arab terrorist naye anaenziwa hapa Tanzania hadi anapewa barabara? Hivi tumekosa kuwatambua watanzania wenzetu wapigania uhuru wa taifa letu, wenzetu waliojitolea maisha yao kulinda mipaka ya nchi yetu, watu waliojitolea nguvu zao, akili zao na uzalendo wao katika kulitumikia taifa letu hadi anatafutwa mtu tu wa pembezoni mashariki ya kati ambaye ukichunguza tu legacy yake duniani ni fujo za kisiasa na kidini dhidi ya jirani zake? I hate this.
 
Lakini tunaambiwa Nyerere alikuwa dhidi ya Waislamu na Uislamu... hawakumuuliza hilo huyo Balozi au kina Mohammed Said hawajasoma hii habari?
Hapana Mzee Mwanakijiji, Wapalestine sio Waislam SWAFI, Bali Waislam swafi ni hawa Wapemba na Wamanyema kina Faiza na ShePonda.
 
Last edited by a moderator:
Hahaha, Hill Road inakuwa "Yasser Arafat Road"?

Might as well, the place is hardly recognizable any more, what with the boxy monstrosities rising up like mushrooms everywhere.

Wakazi waliulizwa lakini? Au ndo undakindaki tu?
 
Lakini tunaambiwa Nyerere alikuwa dhidi ya Waislamu na Uislamu... hawakumuuliza hilo huyo Balozi au kina Mohammed Said hawajasoma hii habari?

Labda atumiwe kitabu cha SIVALON na kile cha MUSLIM AND THE STATE ndio atajua

lakini pia usisahau kuwa si kila Mpalestina ni musilam au kila mwarabu ni musilam

afterall mafundisho ya uuislam ni kuwa ISLAM comes first before nationality.

ohhh btw

Nyerere ndio chanzo cha Mfumo Kristo Tanzania
 
Akili za kitumwatumwa hizi sijui zitaishaga lini vichwani mwetu. "Yasser Arafat" road? huyuhuyu Arab terrorist naye anaenziwa hapa Tanzania hadi anapewa barabara? Hivi tumekosa kuwatambua watanzania wenzetu wapigania uhuru wa taifa letu, wenzetu waliojitolea maisha yao kulinda mipaka ya nchi yetu, watu waliojitolea nguvu zao, akili zao na uzalendo wao katika kulitumikia taifa letu hadi anatafutwa mtu tu wa pembezoni mashariki ya kati ambaye ukichunguza tu legacy yake duniani ni fujo za kisiasa na kidini dhidi ya jirani zake? I hate this.
Terrorist?????????? Remember Mandela was still in the list of ‘terrorists’ of the CIA even after he became president of the RSA, so it doesn’t appeal to me to call Arafat an Arab terrorist. It sounds racist, Islamophobic and Arab-phobia. I’m neither an Arab nor a Muslim but I hate it when people are labelled as terrorists for their skin colours or their religious beliefs.
 
Labda atumiwe kitabu cha SIVALON na kile cha MUSLIM AND THE STATE ndio atajua

lakini pia usisahau kuwa si kila Mpalestina ni musilam au kila mwarabu ni musilam

afterall mafundisho ya uuislam ni kuwa ISLAM comes first before nationality.

ohhh btw

Nyerere ndio chanzo cha Mfumo Kristo Tanzania

Hoja gani hizi!? Au zinatoka kwenye kichwa cha Cocos nucifera?
 
Lakini tunaambiwa Nyerere alikuwa dhidi ya Waislamu na Uislamu... hawakumuuliza hilo huyo Balozi au kina Mohammed Said hawajasoma hii habari?
Mzee mwanakijiji samahani muungwana mwenzangu hivi hujawahi kuona chuki za baba yako nyerere dhidi ya waislamu unamacho lakini huoni unamaskio lakini huskii unamoyo lakini huna hisia kweli st nyerere ni nouma
 
Hoja gani hizi!? Au zinatoka kwenye kichwa cha Cocos nucifera?

121Cocos-nucifera-whole-nuc.jpg
 
Akili za kitumwatumwa hizi sijui zitaishaga lini vichwani mwetu. "Yasser Arafat" road? huyuhuyu Arab terrorist naye anaenziwa hapa Tanzania hadi anapewa barabara? Hivi tumekosa kuwatambua watanzania wenzetu wapigania uhuru wa taifa letu, wenzetu waliojitolea maisha yao kulinda mipaka ya nchi yetu, watu waliojitolea nguvu zao, akili zao na uzalendo wao katika kulitumikia taifa letu hadi anatafutwa mtu tu wa pembezoni mashariki ya kati ambaye ukichunguza tu legacy yake duniani ni fujo za kisiasa na kidini dhidi ya jirani zake? I hate this.
kwa vile tafsiri yako terrorist ni mwislam basi utapata shida sana. hivi wewe bwe.ge ni yupi terrorist halisi kati ya mpalestina aliyenyang'anywa ardhi yake na jiyahudi lililonyang'anya. you should see psychiatric otherwise mirembe panakufaa sana.
 
Lakini tunaambiwa Nyerere alikuwa dhidi ya Waislamu na Uislamu... hawakumuuliza hilo huyo Balozi au kina Mohammed Said hawajasoma hii habari?
umepewa macho lakini huoni kwayo, umepewa masikio lakini husikii kwayo, umepewa akili lakini hufaidiki nazo, wewe mwanakijiji unaishi dunia ipi? nenda maeneo ya waislam then utajua nyerere alichokifanya. hata pale palipokuwa panapumua aliua. binafsi wala huwa sitakagi hata kulisikia hili jina. huwa najisikia kuchefuchefu.
muda si mrefu atakuwa mwenyeheri, hiki ni cheo cha kidini na kwa mtu mwenye mchango kwenye hiyo dini, nyerere alikuwa kiongozi wakisiasa. anaingiaje huko? wake up mwanakijiji and see
 
Dini ni nini katika dunia hii na mbele ya hukumu ya GOD. It's absolutely nowt.

Masikini na fukara wa hekima na busara tu ndiye anayepiga kelele kwa jina la dini katika dunia hii wakati binadamu wanadunda kwa matendo yao.

Hata GOD huwa anawasikitikia kama siyo kuwacheka wanaopatwa na jaziba za dini wakati kipimo cha hukumu ni matendo yao.

Keep on yelling and screaming kwa jina la dini.
 
Back
Top Bottom