Mtaa wa Mwalimu Kihere Tanga

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,918
30,260
MTAA WA MWALIMU KIHERE TANGA

Mwenye historia ya Mwalimu Kihere atuwekee hapa.

''Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika haikuwa na jingine isipokuwa kumuomba Idd Faiz Mafungo asafiri kwenda Tanga na kupata fedha zaidi kutoka huko.

Mwalimu Kihere alikuwa tayari amekusanya fedha hizo na alikuwa anasubiri tu zije zichukuliwe na kupelekwa makao makuu kutunisha mfuko wa safari ya Nyerere UNO.

TANU ilipata habari kwamba yeyote ambaye angeenda Tanga kuchukua fedha hizo kwa ajili ya safari ya Nyerere angekamatwa.

Kabla ya kuondoka, Oscar Kambona, Katibu Mkuu wa TANU, na John Rupia, Makamo wa Rais wa TANU, walikwenda kuonana na Idd Faiz nyumbani kwake Ilala kumuaga, kumtakia safari njema na kumpa maelezo kwa ufupi.

Safari ya kwenda Tanga haikuwa na tatizo lolote, lakini katika wakati wa kurudi basi ambalo Idd Faiz alikuwamo lilisimamishwa njiani Turiani na makachero.

Idd Faiz alikamatwa, akavuliwa nguo na kupekuliwa, lakini hakukutwa na fedha.

Hili lilimshangaza na kumchanganya yule afisa aliyemkamata kwa sababu walikuwa na taarifa kwamba Idd Faiz alikuwa amechukua fedha kutoka kwa Mwalimu Kihere kule Tanga.

Idd Faiz aliwekwa chini ya ulinzi na kupelekwa Dar es Salaam kwa usaili zaidi wakati wote akiwa analindwa na askari wenye silaha.

Baadaye Idd Faiz aliachiliwa huru. Zile fedha za TANU zilifika makao makuu ya TANU Dar es Salaam, salama salimini. Zilizokuwa zimepewa kubeba msichana mdogo aliyekuwa abiria ndani ya basi lile alimokuwa Idd Faiz.''

(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes)

Ikiwa mnataka historia zaidi ya Mwalimu Kihere In Shaa Allah nifahamisheni.

Picha: Mwalimu Kihere.

1700935165210.png

1700935215271.png

Mwalimu KIhere

 
Back
Top Bottom