Msuva aing'arisha Wydad Casablanca CAF Champions league, yafuzu makundi

tyc

JF-Expert Member
Feb 25, 2014
1,179
2,955
Wydad (Morocco) 3-0 Stade Malien (Mali)
( aggr 3-1)

Mtanzania Simon Msuva jana alicheza kwa dakika 86 kabla ya kufanyiwa Sub, ambapo kwa muda huo mnamo dakika ya 46 kipindi cha pili alipiga krosi mujarrabu iliyomfikia Ellafi na kuweka mpira kimiani ikiwa ni goli la pili kwa Wydad Casablanca.

Hvyo mpaka mpira unaisha, Wydad wamefuzu kuingia hatua ya makundi.

Hii ni mechi ya pili ya CAF Champions league kwa Simon Msuva ndani ya uzi wa timu yake mpya ya Wydad.

Kongole Msuva kwa kuweza kuaminia na Kocha na kupewa nafasi ya kucheza na kufanya vyema.
 
Hahahaa! Wasikuelewe vibaya
Kabisa mkuu. Kupiga cross ni wajibu wa mchezaji ambaye amepangwa kwenye nafasi husika na kuzaa goli ni suala lingine ambalo hutegemea ushapu wa mfungaji mwenye njaa ya goli!
 
Kwa hiyo hiyo cross moja ndio kaifanya timu yake ifuzu? Na ing'are?
..
Hebu ongeza kidogo mchango wa mtanzania mwenzetu katika hilo!
..
NB: Sina tatizo na Msuva
ulitaka uambiwa kapiga kona ikatoka au? umeambiwa tu kwa ufupi moja ya tukio lake kwa dk 86
 
Kwa hiyo hiyo cross moja ndio kaifanya timu yake ifuzu? Na ing'are?
..
Hebu ongeza kidogo mchango wa mtanzania mwenzetu katika hilo!
..
NB: Sina tatizo na Msuva

Jamaa amenogesha tu.. waydad kabla hata ya msuva huwa inafika hatua ya makundi kila msimu na huwa haitolewi hatua ya makundi.. wydad nusu fainali ni stage anayofika kila msimu
 
Back
Top Bottom