Msukule ni nini?

Inasemekana hukatwa ulimi,hili lina ukweli wowote?
Wapo wanaokatwa ulimi na hii ndio hatua ya mwisho ya kukamilisha usukule wao...hapo hata ikitokea akarudi katika hali ya uzima wa kawaida hataweza kuongea lolote
Katika maisha yangu niliwahi kumuona msukule wa kweli (sio hawa wa kina mitume na manabii)mwaka 1984 kipindi kile cha uhujumu uchumi na ni baada ya mmiliki wake kufa, kwa mdomo wake alisema kamhifadhi fulani kwenye shamba lake kubwa la migomba
 
Nashukuru sana Dr. MziziMkavu kwa maelezo mazuri sana. Pamoja na majibu na maelezo hayo bado nina mambo yenye kuhitaji ufafanuzi.
Baada ya kufanywa msukule wanakula nini ?
Je akishakuwa msukule atakaa na hiyo hali kwa muda gani na mwisho wake ni nini? Je anakufa tena au anafanyaje au hatakuwa na mwisho?
Wakiwa katika hali hiyo wanaweza kufanya kazi gani ?
Asante.
 
Shukrani kwa elimu adimu mkubwa.
 
Zipo aina nyingi za kuchukua watu misukule, aina iliyozoeleka sana ni mtu kufa kisha mwili wake ukazikwa, aina ya pili ni wachawi kuondoa nafsi ya mtu akiwa hai na kuingiziwa pepo na akaendelea kuishi, aina ya tatu ni wachawi kuchukua nyota ya mtu na kuuziwa mtu mwingine.
 
Baada ya kwisha kuwa wewe Msukule wanakutumia kwa kazi zao mpaka hapo utakapo kufa kifo cha kawaida wanakuzika au kukutupa porini unaliwa na wanyama fisi,simba ndio mchezo umemalizika.

 
Wapo watu huwa wanatafuta watu wa kumfanyia kazi zake bila ya malipo, watu kama hao huwaendea wachawi na kumwomba amtafutie vijana wenye nguvu kwa ajili ya kazi za shamba au kwa kazi ya kushusha nyavu za uvuvi wa samaki chini ya maji, au kwa kazi ya kwenda kuiba, au kwa kazi za kwenye viwanda n.k

Mchawi akimwona kijana mwenye sifa hizo huandaa uchawi na kuita jini kwa ajili ya kumzibiti, kwa sababu kifo chochote ni lazima kuwepo na sababu, njia wanazotumia sana ni kutumiwa jini na kijana anaumwa sana kichwa mbele ya paji la uso na baada ya muda kijana anafariki, kabila ya kifo chake wanachukuwa kipande cha mgomba, yule jini aliyetumwa anaingia ndani ya ule mgomba na kuvaa sura ya marehemu kabisa wanafana kwa kila kitu. Mchawi aliyepewa kazi ya kutafuta wafanyakazi humshika yule kijana na kumpaka madawa ya kumpumbaza na kumfanya asionekane kwa macho ya kawaida, hubaki naye ndani ya nyumba.

Ndugu mnachukua mgomba wenu na kuanza maandalizi ya mazishi, kwa kawaida vifo vya aina hii huwa vina vituko vingi sana, ndugu kutokuelewana, jambo dogo unazuka ubishi hadi watu wanapigana.

Jambo muhimu sana kwa wachawi hawa kukamilisha shughuli ni kuwafanya ndugu wakubali kuwa ndugu yao amekufa, na mbinu kubwa wanayotumia na kuhakikisha ndugu wanalia sana. Wakiona hakuna mtu anayelia, atatokea mtu hasa mwanamke atakuja analia sana na kujitupa chini kwenye vumbi, ajabu iliyoje ni kuwa huyo mwanamke atakua hajulikani kabisa kwenye hiyo familia.

Ndugu wanapoanza nao kumlilia ndugu yao, basi mjue kilio chenu ndiyo rukhusa ya wachawi kuondoka na ndugu yenu, kama ndugu wakitulia kabisa, ukweli ni kuwa hawa wachawi hawataweza kamwe kumwondoa ndugu yenu ndani ya nyumba yake.

Kama wamefanikiwa kuondoka nae, zipo dawa za kumsafisha asionekane na dawa zingine ananyweshwa ulimi unarudi ndani ya tumbo na hataweza kuongea. Misukule huwa wanalishwa sana pumba za nafaka, damu za watu na nyama za watu waliokufa.
 
Lipo pia hili la watoto wadogo/wachanga wanafariki na kusemekana nao wamefanywa msukule angali hawana nguvu za kufanya kazi au hili nalo lipoje hili..na je hizo dawa source yake ni nini?
 
Mkuu MziziMkavu nahitaji kuwa mchawi ili na mimi niweze kuwa na misukule yangu, maana kuna mdada humu ndani atongozeki, so ni bora nimtoe awe Msukule wangu ili tufanye yetu!!!
 
Duh asante sana kwa elimu hiyo. Mpaka nimeogopa sana. Kwanini ni mgomba mara nyingi. Je ni upatikanaji wake au kuna siri gani kwenye mgomba na sio mti au kitu kingine?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…