Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,752
- 7,876
&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];...Hebu leo tujadiliane Usongo wa Mawazo katika MMU. Tangu zamani pamekuwepo na matukio ya Mauaji ya kimapenzi, ama kusikia Mwanaume au Mwanamke amejiua kutokana na "wivu" wa kimapenzi.
Watu hawa ni sawa na mimi na wewe katika maisha ya kila siku, mpaka linapotokea tukio ndipo unapopatwa na akili "dahhh;.!" kumbe jamaa hakuwa wa kawaida!
Hebu jiangalie unajielewa vipi kukabiliana Usongo wa mawazo kukuepusha na madhara makubwa kwako, kwa mwenza wako na jamii inayokuzunguka.
Kama ushawahi jiambia, "sioni faida ya maisha!" "sina thamani tenasitapata mwingine tena Nishaonekana sina maana somo hili linakuhusu sana.
Chukulia umegombana na Mpenzi wako, au hata mzazi wako, au ndugu yako kipenzi,Unakabiliana vipi na maumivu hayo?
Je, hujifungia chumbani peke yako na kutafakari?
Je, hujiamulia kutoka nje kufunga upepo peke yako?
Je, huwatafuta Marafiki mwende nao sehemu ukajiliwaze?
Je, Kuna mtu (mpango wa pembeni) ambaye humtumia kujiliwaza nae?
Au, wewe ni katika wale wanaochukulia hizi ni changamoto za kawaida&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];.litapita tu?
Kumbuka!
Pombe, sigara, ngono, etc&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];. kwa wengi ni "short term solutions" kwa matatizo yanayosababisha Usongo wa Mawazo.
Karibuni tujadiliane
Cc; Eiyer Dark City BAK King'asti MwanajamiiOne Rock City Mentor, Nyamayao The Boss sakapal TIMING AshaDii Tuko EMT Fixed Point afrodenzi BelindaJacob, na wengineo wote mnaohusika katika "mada nzito"