Msomi UDSM atabiri kifo cha CUF 2020

Ado Shaibu

Verified Member
Jul 3, 2010
99
225
MSOMI WA UDSM ATABIRI KIFO CHA CUF 2020

Mwanazuoni kutoka Idara ya Fine and Performing Arts ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dk. Charles Kayoka amesema Chama cha CUF kitadhoofika ifikapo mwaka 2020 kutokana na kupukutikiwa na viongozi na wanachama wake waliojiunga ACT Wazalendo kumfuata Maalim Seif.

Dk. Kayoka amesema hali aliyojionea Zanzibar ambako alitembelea hivi karibuni CUF imeshafutika. Kayoka alitoa mfano wa Stone Town kulikoshamiri bendera za CUF lakini hivi sasa hazizidi mbili.

Kwa upande wa Zanzibar, amesema hakuna Mbunge wala Mwakilishi ambaye anaweza kushinda ubunge kwa CUF kwa sababu "ACT Wazalendo hivi sasa ndio habari ya mjini".

Amesema baada ya uchaguzi mkuu wa 2020 CUF kitapoteza ruzuku na kushindwa kujiendesha.

Kayoka amesema ACT Wazalendo kina uwezekano mkubwa wa kukua na kupata wabunge wengi Zanzibar na kwenye baadhi ya maeneo ya bara.

Sikiliza mahojiano yote aliyoyafanya na Icon TV

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
2,452
2,000
Zitto ni bonge la kulenga
1.Unakumbuka mke wake na ndoa kafunga wapi.hapo ujue shabaa yake hana taka kuweka wapi miaka ya mbele.
2.Dini nayo ni kitu kikubwa ambacho watu wakigoma wanakubalika sana ukanda wa pwani kwa msimamo wa kidini.
3.Hakuna chama pinzani upande wa visiwani kutoka bara kikampokea maalim sefu.
....nipo natafakari baa
 
samesame

Senior Member
Jul 21, 2019
115
250
Hata hii inahitaji utabiri ! Tuache masihara hata asiye kwenda shule anakukwambia nini kifuatacho
 
Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,004
2,000
Ado huu sio utabiri
Huu ni ukweli na kila mtz anajua
CUF mwisho wake ni November,2020
 
Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,361
2,000
Hivi hata hili nalo linahitaji Msomi wa Degree ya kwanza ya Political Science kulifahamu ama kulitabili achilia mbali huyo Msomi wa Performing Arts!! CUF inapumulia masikio
 
Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,361
2,000
Hata hii inahitaji utabiri ! Tuache masihara hata asiye kwenda shule anakukwambia nini kifuatacho
Neno utabiri limekosa maana kabisa kama kufa kwa CUF nako kunatabiriwa sasa! Unatabiri kitu ambacho tayari kimetokea? Huenda huyo msomi anaigiza!
 
carter

JF-Expert Member
Jan 23, 2009
3,088
2,000
Natabiri kesho asubuhi jua litaanza kuchomoza upande wa mashariki. Kesho muwe makini sana kuangalia hilo.
 
BUBERWA D.

JF-Expert Member
Apr 22, 2011
2,166
2,000
KAYOKA (Kanyoka) + Zitto + Shaibu +Kigoma= ACT. Huu ujumbe ni mwiba kwa chama kingine wala si CUF. ACT 2020-2025; chama kikuu cha upinzani. Go ACT!
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
24,951
2,000
Sio rahisi CUF kufa huyu msomi kachemka .CUF haijui kabisa .CUF iliyokuwepo wakati Maalim Seif Yupo CUF ilikuwa Ni ya Makundi mawili ya Wapemba na waafrika ngozi nyeusi wa Zanzibar na bara kiongozi wao ndani alikuwa Profesa Lipumba.

Vita ndani ya CUF ilikuwa Kati ya Watoto wa sultani akina Maalim Seif na Wapemba wenzie na waafrika watoto wa Mzee karume wakiongozwa na mtoto wa Mzee Karume Ibrahim Lipumba.Kama Mzee Karume alivyomvurumisha Sultani ndivyo Lipumba alivyomvurumisha Maalimu Seif.

Mapinduzi ya 1964 yalijirudia.Sasa hivi CUF Ina waafrika weusi wa bara na Zanzibar.Haifi ng'ooo.Huyu msomi namshangaa Sana ana uelewa finyu Tena mdogo mno hiyo PhD yake alipataje?

Hivi hajui kabisa kuwa Stone town Ni eneo wanaishi Wapemba? Ameshindwa kulijua hata Jambo dogo Kama hilo
 
Michibo

JF-Expert Member
Feb 16, 2015
1,551
2,000
Mamlaka zinatumia simu ya Ado Shaibu kupotosha, tunajua zimeshikiliwa kwa uchunguzi.... itakuwa alijisahau ku-log out.
 
Abul Aaliyah

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
3,531
2,000
Et co rahc tawi Lenu ndo lishakatika tena
Sio rahisi CUF kufa huyu msomi kachemka .CUF haijui kabisa .CUF iliyokuwepo wakati Maalim Seif Yupo CUF ilikuwa Ni ya Makundi mawili ya Wapemba na waafrika ngozi nyeusi wa Zanzibar na bara kiongozi wao ndani alikuwa Profesa Lipumba.

Vita ndani ya CUF ilikuwa Kati ya Watoto wa sultani akina Maalim Seif na Wapemba wenzie na waafrika watoto wa Mzee karume wakiongozwa na mtoto wa Mzee Karume Ibrahim Lipumba.Kama Mzee Karume alivyomvurumisha Sultani ndivyo Lipumba alivyomvurumisha Maalimu Seif.

Mapinduzi ya 1964 yalijirudia.Sasa hivi CUF Ina waafrika weusi wa bara na Zanzibar.Haifi ng'ooo.Huyu msomi namshangaa Sana ana uelewa finyu Tena mdogo mno hiyo PhD yake alipataje?

Hivi hajui kabisa kuwa Stone town Ni eneo wanaishi Wapemba? Ameshindwa kulijua hata Jambo dogo Kama hilo
 
Gullam

JF-Expert Member
Dec 1, 2013
5,249
2,000
Yaaani kwa usaliti alioufanya Madgarena Sakaya na kundi lake lazime kife tu.
 
ndammu

JF-Expert Member
Apr 21, 2017
1,857
2,000
Sio rahisi CUF kufa huyu msomi kachemka .CUF haijui kabisa .CUF iliyokuwepo wakati Maalim Seif Yupo CUF ilikuwa Ni ya Makundi mawili ya Wapemba na waafrika ngozi nyeusi wa Zanzibar na bara kiongozi wao ndani alikuwa Profesa Lipumba.

Vita ndani ya CUF ilikuwa Kati ya Watoto wa sultani akina Maalim Seif na Wapemba wenzie na waafrika watoto wa Mzee karume wakiongozwa na mtoto wa Mzee Karume Ibrahim Lipumba.Kama Mzee Karume alivyomvurumisha Sultani ndivyo Lipumba alivyomvurumisha Maalimu Seif.

Mapinduzi ya 1964 yalijirudia.Sasa hivi CUF Ina waafrika weusi wa bara na Zanzibar.Haifi ng'ooo.Huyu msomi namshangaa Sana ana uelewa finyu Tena mdogo mno hiyo PhD yake alipataje?

Hivi hajui kabisa kuwa Stone town Ni eneo wanaishi Wapemba? Ameshindwa kulijua hata Jambo dogo Kama hilo
Japo kwamba ukweli huutaki lakini bakia tu kuubali.

Cuf kutoka Zanzibar ndio kwishinei kabisa.

Hiyo ccm yako unayoiyona inajipamba kwa kila hatua Zanzibar kwamba inakubalika basi ujue nikinyume chake.

Unajua kwamba ccm akifanya mikutano Zanzibar hasa Pemba inabeba mamluki ya watu kutoka Tanganyika na Unguja ili kuziba mapengo?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom