Msambichaka Mkinga
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 1,646
- 2,911
Wewe ni big O, unasoma lakini huelewi unachosoma. Marekebisho ya katiba ya Zanzibar yamejenga takwa la kikatiba kuwa kwaajili ya utengamano wa watu wa Zanzibar, chama chochote kinachoshinda kitaunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.Huyu mwanasheria anayedai matokeo hayajakidhi matakwa ya kikatiba hivyo unapaswa kurejewa ni jipu lililooza inabidi atumbuliwe mapema! Ni aibu kwa mwanasheria kudai hivyo!
Ukweli ni kwamba matokeo hayajakidhi kuundwa kwa serikali ya UMOJA wa kitaifa! Kwa hiyo itaundwa serikali ya chama kimoja!
Mantiki ya serikali ya UMOJA wa kitaifa ni matokeo ya uchaguzi kutokutofautiana kwa kiasi kikubwa. Lakini kwa matokeo ambayo mgombea mmoja amezoa zaidi ya asilimia 90 katiba iliona hakuna mantiki ya kuunda serikali ya UMOJA wa kitaifa! Ndiyo maana katiba haisemi katika mazingira hayo serikali ya UMOJA wa kitaifa itaundwaje, maana haipaswi kuundwa katika mazingira hayo!
Ndiyo maana Hamad Rashid ameangukia pua!
Kama Shein akichagua Makamu wa kwanza wa rais katika mazingira haya, atakuwa amevunja katiba na baraza la wawakilishi wanaweza kumwajibisha!
Napiga chai hapa na Magimbi huku nikitembea na huu uzi. Nafurahi kwamba tumetoka vizuri na kwa pamoja tukiwa na two third kwenye BLW kwenda kwa wananchi kupata ridhaa kupitia sanduku la kura za maoni. Nasema mazingira hayahaya yaliyompatia shen ushindi mnono kwa amani na utulivu ndiyo hayohayo yatakayotumika kupata two third kutoka kwa wananchi wa Zenji. Chukua tu picha ya hizo kura za prezident na gawanya kwa waliojiandikisha huko visiwani. Ukiwa na swali uliza tena.Samahani Kada mwenzangu..mtoa mada amezungumzia two third kama itapitishwa na baraza la wawakilishi ili ipigwe kura ya maoni kubadili katiba kuondoa SUK..kama itafanyika hivyo basi wananchi wa Zanzibar two third haitafika hata kama tufanye hujuma. Lakini two third kwa Baraza mbona ipo tayari shekhe..mtiti ni kwa wananchi wenyewe wa Zanzibar..CUF watakataa na sisi tutakubali lakini hatuzidi NUSU ya Wazanzibar wote.
Wewe ndiyo zero kabisa! Haujiulizi kwa nini katiba haikuweka provision ya namna ya kuunda serikali ya UMOJA wa kitaifa kuaccommodate mazingira ambapo mgombea mmoja amepata zaidi ya aslimia 90 ya kura zote halali!Wewe ni big O, unasoma lakini huelewi unachosoma. Marekebisho ya katiba ya Zanzibar yamejenga takwa la kikatiba kuwa kwaajili ya utengamano wa watu wa Zanzibar, chama chochote kinachoshinda kitaunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Kisha katiba hiyo ikatengeneza scenario ya uundwaji wa serikali hiyo. Moja ni pale kuna mgombea wa Urais zaidi ya mmoja, na ya pili ni pale ambapo kuna mgombea mmoja tu.
Takwa hili la kikatiba ndiyo lililoilazimisha CCM kutokukubali kuwaondoa wagombea wote ambao walisema wamejitoa. Na pia wakaweka tahadhari nyingine ambayo ilikuwa ni kuwabembeleza wanasiasa tumbo kutangaza kuwa wao watashiriki.
Vyovyote watakavyofanya, CCM imeitia aibu kubwa Tanzania, Zanzibar na watu wote wa Taifa hili. Dr. Shein mtu aliyeonekana muungwana ameingia kwenye rekodi mbaya ya tamaa ya madaraka. To hell CCM.
Huwezi kupatiwa jibu kwa sababu roho zao km za pakaAsilimia kubwa ya wanasiasa wetu ni wachumia tumbo,muangalie huyo Hamad Rashid kwa alichokifanya,
Pili kama Jecha alijua fika kuwa serikali ya umoja wa kitaifa inatambulika kikatiba na ili kumpata makamu wa Rais unahitaji angalau 10% ya kura zote basi wangechakachua kwa kumpa Hamad Rashid hiyo 10% ili awe makamu wa kwanza wa Rais,kama hawakuliona hilo na katiba ndivyo inavyotamka,je watampata wapi makamu wa Rais ilhali hakuna ailefikia hicho kiwango?watupe jibu.
Binam mambo yako?sio kweli..
alafu hata kama ni kweli CCM wanashindwaje kufanya ubabe katika hili?
Mimi difikirii kama wamekosea hesabu, matokeo haya yamepangwa yawe hivyo kwa malengo maalum ili kuacha nafasi ya majadiliano kwa Mara nyingine tens kati ya CUF na CCM.
Kura za ADC na CUF hazitofautiani sana, sasa kati ya Maalim na Hamad nani ni mtaji kwa CCM kusaidia utulivu wa Zanzibar? Hamad angepata kura zaidi ya 10% inamaana angekua makamu wa kwanza moja kwa moja, lakini Je, hali ingekua shwari Zanzibar? Unafikiri kweli wameshindwa kupika matokeo ya kumpa Hamad ushindi?
am good binamuuu..wwBinam mambo yako?
hapa kuna weza kuwa na harufu ya ukweli flani.Ni kweli unavyosema, lakini kubadilisha katiba ni lazima ipigwe kura ya maoni Zanzibar, na kwa maana hiyo, uchaguzi mwengine ni lazima, kubadilisha katiba ama kuendelea na katiba! Venginevyo, CCCM wanakula kiti moto mwezi wa Ramadhani mchana na hio wameona haitoshi, wameagiza kreti za bia. Haramu juu ya haramu
porojo gani hizi........cuf sasa wajifunze kwamba sera za kususia na ubinafsi hazina tija. oneni sasa wapemba watawakilishwa na wabunge wasiokua na ridhaa yao kwa ubinafsi wa seif. kama yeye hawezi kushinda basi wote wakose.
Zanzibar Post
BAADA YA CCM KUKOSEA KUKOKOTA TARAKIMU NA KUTOA TAARIFA RASMI YA MATOKEO YA UCHAGUZI WA MAJEREO MATOKEO RASMI HAYAKIDHI MATAKWA YA KATIBA YA ZANZIBAR YA SASA NA HIVYO UNAPASWA KUFANYIKA UPYA SIO MAREJEO TENA. - SHENI NI MKOSI !
Kufuatia matokeo rasmi yaliotangazwa na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Jecha Salim Jecha kutokidhi matakwa ya kikatiba uchaguzi wa Zanzibar unapaswa kuitishwa upya na sio marejeo tena.
CCM wanapenda namba lakini hawajui kukukota, walipaswa kujua athari za matokeo rasmi waliyotangaza, inashangaza Tume ya Uchaguzi Zanzibar mkurugenzi wake ni mtu wa mahesabu na makamishna wawili ni watu wa mahesabu lakini bado wamefanya makosa yatakayoligharimu taifa fedha nyingi.
Kwa kukidhi matakwa ya katika ya sasa uchaguzi unapaswa huitishwa upya, yaani uandikishaji wapiga kura upya, uteuzi wa wagombea upya, kampeni nyengine na upigaji kura upya (fresh election).
Na hii inatokana na CCM kuwa "rigid" kupanga matokeo ya wao kusomba viti vyote, kwa mujibu wa masharti ya katiba raisi mteule baada ya kuapishwa atatakiwa kuteuwa makamu wawili wa raisi ndani ya siku saba, na mmoja katika makamu wa raisi ni makamu wa kwanza wa raisi ambaye atatokana na na chama kilichopata nafasi ya pili katika idadi ya kura kwa angalau 10% na hakuna chama kilichoshiriki uchaguzi wa marejeo kilichofika 10%.
Na kama hakuna chama kilichofika 10% katiba inataka nafasi hiyo kupewa chama kilichopata wingi wa viti katika baraza la wawakilishi endapo ingekuwa mgombea wa CCM hakuwa na mpinzani, lakini katika uchaguzi wa marejeo CCM ilikuwa na wapinzani 12 katika nafasi ya uraisi.
Ili kukidhi matakwa ya katiba inabidi aidha katiba kubadilishwa na hilo lina ghamara kubwa kwa sababu kubadilisha kifungu chochote cha katiba ni lazima marekebisho hayo yapelekwe katika baraza la wawakilishi na hoja kupita kwa theluthi mbili na kisha yapigiwe kura ya maoni na wanzanzibari wote kwa wingi wa theluthi mbili kuondoa vifungu vya katiba vinavyoweka masharti hayo ya kikatiba.
Vinginevyo uchaguzi unapaswa kuitishwa upya (fresh election) kuanzia uandikishaji, uteuzi wa wagombea, kampeni na upigaji kura ili kukidhi matakwa ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 toleo la 2010.
Vinginevyo Zanzibar itaingia katika mgogoro mkubwa wa kikatiba tangu katiba ya Zanzibar ilipoasisiwa mwaka 1984.
Chanzo : Mwandishi Wetu Zanzibar Post
Mnaita watu wasaliti baadae wenyeviti wenu wanaandaa press kuwasafisha, hata Zitto mlimwita msaliti lakini mmemkubali na mwenye kiti wenu kamtaka radhi. Kiongozi mkuu wa ukawa baada ya kuwanunua mmetumia muda mwingi kumsafisha hata kwa kuita watu wasaliti.
Aiseeee namshukuru Mungu, sijakutia machoniam good binamuuu..ww
Soma katiba ya Zanzibar, usipaparike. Kwa mazingira ya Zanzibar, wakati wanaandika katiba haikufikiriwa kuwa kuna siku itatokea chama kimoja kinaweza kupata kura zaidi ya 90%.Wewe ndiyo zero kabisa! Haujiulizi kwa nini katiba haikuweka provision ya namna ya kuunda serikali ya UMOJA wa kitaifa kuaccommodate mazingira ambapo mgombea mmoja amepata zaidi ya aslimia 90 ya kura zote halali!
Hicho kichwa siyo cha kubeba nywele tu! Fikiri!
mkuu hii sentensi ya mwisho ni lugha gani? kijaluo au lugha ya wakikuyu?sentensi yenyewe ndio hii (huo ugunyu sasa bhanaa)Wazanzibar mnatuzingua bhanaa imekuwa kila siku uchaguzi tu hamna shughuli zingine za maendeleo mkazifanya ???? Huo ugunyu sasa bhanaa
ndio nani?Ya ngoso