Msokotano mpya wazuka Zanzibar

Hivi bado kuna watu wanaendelea kuwaza uchaguzi wa Zanzibar?

Uchaguzi umeshakwisha na Rais ameshapatikana yaliobaki ni mayowe yasiyokuwa na msaada wowote zaidi ya kutuumiza masikio
 
Mbona nyinyi hamtaki kuelewa? CCM imeshinda kwa kishindo katika nafasi mbalimbali za Uongozi mara baada ya uchaguzi wa marejeo. Ina wawakilishi wengi hadi huko Barazani ambako ndiko wataamua kuendelea na SUK au kuitupilia mbali. Hiyo two third sio issue kabisa. CUF wajiandae kuisoma namba tu.
 
UPDP imepata kiti kimoja

Zanzibar njiapanda
 
Hii Nchi inavilaza sana! Hawakuwaza hayo yote? Mistake zingine Ni za kizembe sana! Wanaume Kabisa mmekaaa Miezi yote hiyo mkiandaa haya mambo, hamkufikiria Hivi vitu? Yaani hata ushindi wa 60% ulikua unatosha Kabisa! Mungu kawaumbua peupeeeee!

Wenyewe wanasema;

"Ukiwa muongo uwe Na kumbukumbu"
 
Hivi hao watoto wamepiga kura kweli au utani? Kama ni kweli walio bariki ujinga huo walikuwa wanafikiria nini, au ndio kulewa madaraka kwenyewe!!!

Wamepiga kweli.CCM kila kitu cha wezekana
 
Jambo dogo sana hili, kubwa lilikuwa lile la kupora ushindi wa mtu mchana kweupeeee. Kama kufuta matokeo ilikiukwa katiba waziwazi tena bila haya, itashindikanaje hapa??!!!
 

Mnaita watu wasaliti baadae wenyeviti wenu wanaandaa press kuwasafisha, hata Zitto mlimwita msaliti lakini mmemkubali na mwenye kiti wenu kamtaka radhi. Kiongozi mkuu wa ukawa baada ya kuwanunua mmetumia muda mwingi kumsafisha hata kwa kuita watu wasaliti.
 
Samahani Kada mwenzangu..mtoa mada amezungumzia two third kama itapitishwa na baraza la wawakilishi ili ipigwe kura ya maoni kubadili katiba kuondoa SUK..kama itafanyika hivyo basi wananchi wa Zanzibar two third haitafika hata kama tufanye hujuma. Lakini two third kwa Baraza mbona ipo tayari shekhe..mtiti ni kwa wananchi wenyewe wa Zanzibar..CUF watakataa na sisi tutakubali lakini hatuzidi NUSU ya Wazanzibar wote.
 
Wamefanikiwa kuvunja Muungano ndio washindwe kubadilisha hicho kifungu? Subiri watakuja wanasheria wao sasa hivi na watasema hakuna Katiba iliyovunjwa. Subirini muone
 
Naomba wachambuzi mahiri mtusaidie sisi mbumbumbu. Hivi hali y kisiasa ya Zanzibar inatofautiana kiasi gani na hali aliyojenga Nkurunziza nchini Burundi?
 
Kama wamelazimisha uchaguzi kurudiwa, watashindwaje kulazimisha jambo lolote kuhusu uundaji wa serikali mpya? Ukishaharibu, dawa ni kuendelea kuharibu zaidi. Hongera CCM ZNZ, endeleeni kuharibu mpaka kieleweke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…