Msiwashangae wanawake wanapokuwa na vurugu kichwani….!

Msiwashangae wanawake wanapokuwa na vurugu kichwani….!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,443
Reduce-belly-fat.jpg


Kwa mujibu wa takwimu zisizo rasmi zinaonyesha kwamba idadi ya wanawake wasiyoikubali miili yao hapa nchini ni kati ya 25 hadi 35, kwa maana kwamba ni wanawake 25 hadi 35 katika kila wanawake 100 wasiyokubali miili yao. Ndiyo maana siku hizi tunashuhudia baadhi ya wanawake hapa nchini wanaohangaikam kutafuta dawa za kukuza makalio yao na kubadili rangi ya ngozi zao.

Lakini pia wanawake watatu hadi watano kati ya wale ambao hawakubaliani na jinsi wanavyoonekana kisura, kiafya na hata kuvutia kimapenzi, huwa pia na wanakabiliwa na matatizo ya kisaikolojia, kama vile sononi, upweke, na kujihisi kuwa hawana thamani kama watu wengine. Matatizo mengine kama yale ya kukosa hamu ya tendo la ndoa yanatokana na wanawake hao kutojikubali kimwili.

Kwa nini nimeamua kuzungumzia jambo hili leo?

Ni kwa sababu nimebaini kwamba, kuna idadi kubwa na hasa ya vijana wa kike hapa nchini ambao wanateswa sana na hali ya kujikataa, kukataa miili yao, sura zao na namna walivyo kwa ujumla. Kwa hiyo, wengi wanajitahidi kwa shida kubwa kujibadili ili waonekane kama ambavyo wanaamini ndiyo miili na sura nzuri zilivyo. Na zaidi ni sura za Wamarekani ndizo zilizo nzuri.

Hali halisi kwangu ni kwamba, kama mtu hapendi kitu au jambo fulani, analibadili au analikubali. Sijawahi kuona njia nyingine au mbadala. Kuna mambo ambayo, yanaweza kubadilishwa, ambayo, ni kama vile wembamba, unene, nywele na vingine. Mtu anavibadilisha kwa sababu gani na kwa namna gani, hilo ni jambo linalomhusu mhusika mwenyewe.

Kuna yale ambayo mtu hawezi kuyabadili, kama vile sura, makalio, kimo na maumbile ya sehemu za siri. Hata hivyo baadhi yake, huwa yanabadilishwa kwa kufanyiwa upasuaji na matumizi ya dawa au kemikali fulani. Lakini siku zote mabadiliko hayo yemekuwa ni maumivu makubwa kwa wanaoyafanya, lakini pia ni gharama.

Kumbuka wale ambao wamebadili matiti yao kuwa makubwa au madogo wamejikuta wakilipia gharama kubwa ya maumivu ya kihisia, kwa matiti hayo kuwa kama mawe tu kwa kukosa msisimko yanapoguswa.

Na pia, kila mtoto hufundishwa kama ajikubali au ajikatae wakati anapokua. Mtoto anapooneshwa kwamba, ana mwili mzuri au anapooneshwa kwamba, ana sura nzuri na ana uwezo mkubwa kiakili, hukua akimini hivyo. Anapooneshwa kinyume chake, huamini hivyo pia.

Lakini kuna haja ya kukumbuka kwamba, siku hizi kuna walezi au wazazi wengi. Kuna televisheni, inteneti, vijarida na redio ambavyo vyote kwa pamoja humfundisha mtoto kuwa yeye ni nani. Kwa mtoto wa kike kama atawatazama akina Agnes Gerald maarufu kwa jina la Masogange au Rose Donatus Ndauka waigizaji wa filamu hapa nchini anaweza kuamini kwamba, mwanamke mrembo anayekubalika kwa viwango vya urembo ni yule mweupe mwenye umbo namba nane na mwenye makalio makubwa yaliyobinuka kama hao wasanii niliowataja hapo juu.

Kwa hiyo mtoto wa kike ataanza kuchanganyikiwa akishagundua kwamba muonekano wake haufanani na hao wasanii niliowataja, hata kama nyumbani alifundishwa kwamba mwili ni mwili na ule mtu alio nao ndiyo wake. Lakini, kama hakupata bahati hiyo, hali ndiyo itakuwa mbaya zaidi. Kwa hiyo bado kama wazazi inabidi tufanye kazi ya ziada kuwaambia mabinti zetu kwamba, wana miili mizuri na wenyewe ni wa zuri bila kujali wana muonekano wa namna gani.
 
Haya kakaa nikipata mwana wa kike ntaanza kukaambia kakiwa kadogo kwamba kako vizuri.
 
^^
Yaani hata ingewezekana kubadili kabila, wengine wangebadili
^^
 
siku zote unaboronga kwa thread zako ila leo umetoa kitu mwake baba Ngina

na ungekuwa na kashomori nahisi ungekuwa wa kwanza kukaambia maneno haya

barikiwa mkuu
 
Last edited by a moderator:
eh... bora kaka mkubwa Mtambuzi umewambia maana wengine wanakwambia oh sababu sie wanaume ndio tunataka sijui weupe, oh vyembamba, oh makalio makubwa....
issue ya msingi ni kujitambua na kujikubali...
 
Last edited by a moderator:
siku zote unaboronga kwa thread zako ila leo umetoa kitu mwake baba Ngina

na ungekuwa na kashomori nahisi ungekuwa wa kwanza kukaambia maneno haya

barikiwa mkuu

..huyu mh. anaborongaga kweli?? Sredi zake zilivyonyooka, lol. Au umetania tu?
 
Last edited by a moderator:
Teh teh teh...!!!
Be unbiased, big dark bu.tts are just more than awesome...
 
Hapo ndio kosa lilipo. Katika maisha hatupaswi kuwajadili watu kwa muonekano wa mwili kama nywele, weupe, miguu ama makalio. Tinapaswa kuwaongelea watu kwa utu wa ndani. Na hao mabinti watakua wakijali utu wao wa ndani, kwa sababu wataamini utu wa ndani una thamani zaidi. Mwisho wa siku watajiamini bila kulinganisha makalio yao na ya wengine, ama miguu yao na ya wenzao.

cc OLESAIDIMU
[/QUOTE=Munkari;9865410]Haya kakaa nikipata mwana wa kike ntaanza kukaambia kakiwa kadogo kwamba kako vizuri.[/QUOTE]
 
Last edited by a moderator:
kope bandia
kucha bandia
nywele bandia
rangi bandia
lips bandia
nyusi bandia (zipo za tattoo siku hiz)
titiz bandia
papuchi ladha bandia
takoz bandia
vyote hivi vipo tena kwa bei chee kabisa!
mwe si tunakuwa midoli sasa?
 
Back
Top Bottom