Msitiri anahitajika (MUME)

Msitiri anahitajika (MUME)

Aamin. Nakushukuru tena na tena. Hekima yako ni kubwa mno. Mola akujaalie pale linapokupungukia!
Allahuma Amin...
Sintotulia hadi nimsikie shemeji akinisalimia kwa Uwezo wa Allah-aRahimu !! kwani amethibitsha hili kwa kusema "Niombeni niwaitikie"
*{ ad3uni astajib~Lakum}*
 
Nimekuelewa bwana Kikoozi, ila mbona umri wako ni mdogo sana. Tafadhali usinielewe vibaya ila hiyo tofauti ni kubwa. Nakuombea upate ambae utakuwa umemzidi kidogo jamani, sisi wanawake tunachoka haraka sana na hivyo ni muhim kuoa ambae ni mdogo kwako ili mzeeke wote mkiwa na nguvu.

Nashukuru kwa kuonyesha nia KIkoozi na Mungu akujalie upate mwenza mwema wa nje na ndani ya roho!

Aaaah, miaka 30 kwa 33 sio mingi sana GCM_RCM mpe nafas mdau huyo,bi Aisha aliolewa na Mtume,walitofautiana ki umri,,,,,
 
Last edited by a moderator:
Aaaah, miaka 30 kwa 33 sio mingi sana GCM_RCM mpe nafas mdau huyo,bi Aisha aliolewa na Mtume,walitofautiana ki umri,,,,,

Mkoroshokigolihunitakii mema jamani, nduguze watasema namuonea ndugu yao. Hivi unajua ndugu wanavyokuaga wakorofi hasa kwenye mambo ya umri, yani bora ingekuwa tunalingana, lakini hii ni tofauti ya kuonekana. Kumbuka wanaume hamchoki haraka. halafu jamani unafananisha na Bi Aisha, wale walijaaliwa imani ya hali ya juu ambay sisi hatuna. Nielewe tu hii ni kwa nia njema na si vinginevyo!
 
Tunashukuru kwa kutukumbusha (Bi.Khadijah !!!, radhi ya Allahu kwake)
BarakaAllahu~fikum (God blesses) FYI, bi Khadijah alikuwa ana biashara zake na alikuwa na mtaji wa kutosha... hivyo nawe wa wezaiga na kufuata khatuwa hizo kwani Moula hupenda Wanaume wenye kuoa binti yatima (kuna fadhila maalum) na hupenda Mwanamke atakae mnyanyuwa mwenza kimaendeleo !! (fursa hiyo uwe miongoni mwa changamoto za kidunia) na huko L akhera uwe minna L faizina !! AMIN
 
Hongera GCM_RCM ubarikiwe kwa kuliweka wazi hili jangaa lilozidi miaka hii ya karibuni ( idadi ya wanawake ni kubwa ) kwa kuhakiki tumeshuhudia matangazo mengi humu....!!

Nakunyanyulia mikono juu kwa kukuombea muradi wako "Allah SubaHana wajaala akujaalie mume mwema na kizazi muruwa"
Allahuma Ameen.

Aaaaaamin aaamin Allah amjaalie dada yetu apate aliye na kheri na yeye
 
Last edited by a moderator:
Aaaaaamin aaamin Allah amjaalie dada yetu apate aliye na kheri na yeye
In-Shaa-Allah hata akitaka mume Mwaarabu ntamtafutia ilimradi atimize ndoto na pendo la uhai wake, Japo kaibaguwa rangi.....
Lakini atapata hivi karibuni, kuna dozi nimempa (Qiyamu LyL
GCM_RCM ukifikia uamuzi usisite kunishauri..
 
Last edited by a moderator:
naomba msaada kutuma pm unafanyaje ili niwasiliane na huyu mhitaji?
 
mh! haya ndugu nimekuelewa. Nashukuru kwa muda na ushauri wako.

usikosee kunielewa.
kawaida ya uafrika (angalau kwa siku hizi) mtu mume hutafuta mtu mke na kumshawishi ili amuoe. wakikubaliana ndipo michakato ya ndoa huanza.

kwa umri ulionao kama umetuambia sahihi ilipaswa uwe umekutana na mitongozo mingi sana, katika hili misimamo na mivigezo hutibua mambo sana kwa wadada.
unasubiri au kumkubali mtu anayekupotezea muda wa ku experience maisha ya mapenzi unakuja kushtuka umechelewa sana, kila atakayekutokea anakutana na mpenzi mzigo, anaamua kula kona na kukuachia maumivu ya moyo.

ujeuri umebebwa na kiburi kinachosababisha dharau (mi nna bachelor huyu nae na mitumba yake!!!) unaishia kuwanyali wanaume ukija kushtuka unaifukuza 40.

ukitaka kugongwa na treni kalale relini, ukiisubiria treni kwenye barabara ya lami utazeekea hapo.

nina maana walipo wanaume nawe uwepo ni lazima utamvutia mmojawapo au hata wanaweza kukupigania. Haya yote unayaweza ukijitenga na dharau.

ukifika 40 choice zinapungua, binti yangu akifika umri huo nikawa sijaletewa posa ni lazima nikubaliane na matokeo, (Namuomba YEHOVA hilo lisitokee kwa binti yangu)

usifikiri nimekudharau au sijawa na huruma juu ya tatizo lako, Bali ukisoma kwa uangalifu katikati ya maneno yangu kuna hekima kubwa ya ndoa.

Nasubiri kadi ya mchango wa sendoff.
 
Eeeh Mungu! wenye nia njema na wanione ili wanistiri na mimi!!!!

Napenda kwanza kutoa salaam kwenu nyote.

Jamani nimekuja hapa mbele yenu kwa lengo la kutafuta mwenza ili tustiriane. Najua huwa ni ya kushangaza kwa wengi pale mwanamke anapojitokeza na kuamua kutafuta mume maana haiendani na tamaduni zetu, naomba mtambue kwamba yamenifika shingoni na naona naumia moyoni kwa kusubiri hilo litokee, kwani muda unaenda na natamani hasa kuwa na mwenzangu katika dunia ya mahusiano. Naamini Mungu atanisaidia katika hili. Basi naomba kwa atakae kuwa na nia njema ajitokeze ili nami niweze kufarijika. Sifa zangu ni kama zifuatavyo;

Jinsia: KIKE
Umri:33
Elim: Degree
Kipato: Muajiriwa
Rangi:Mng'avu ila sio mweupe
Umbo: Mwembamba
Kimo: ~160cm
Dini: Islam

Sifa za mwenza
Umri:35-45
Elim: Yeyote tu ila angalau form six
Kipato: Sio lazima muajiriwa ila ni uhakika tu wa kusaidiana kutunza familia
Rangi:yeyote
Umbo: Awe wa kawaida ile sio mnene sana
Kimo: chochote tu
Dini: Islam

Kwa mawasiliano tafadhali naomba tutumie Private message (PM) au email: gcmrcm2011@gmail.com.
Natanguliza shukran zangu za dhati na nipo tayari kwa maswali yenu.
Karibuni waungwana.
kama kweli uko serious njoo inbox tukubaliane na kufahamiana zaidi...inshaallah
 
Eiyer; nimependa ushauri wako sana, nahakikisha nitaufanyia kazi bila mapungufu. Mungu akubariki sana.
Tubarikwe sote bibie kwani lengo ni kuyafanya maisha yawe mepesi....

Ukilegeza masharti unakuwa umejiweka kwenye mazingira makubwa zaidi ya kupata,lakini kuwa makini sana na wanaoku PM....

Nakutakia mafanikio sana
 
LWITIKO LWITIKO ndugu yangu, hapo kwenye shule hapana shida naweza kuwa hata na wa kidato cha nne. Ila sas hapo kwenye dini, yani hapo ni pagumu sana kwangu. Kwa upande wangu dini ni kitu muhim sana maan kitatuunganisha kiroho na kimwili pia. Hata malezi kwa watoto huwa ni rahisi sana maana hawasumbuki kuamua wapi waende hasa katik umri wao mdogo. Ukweli hili la dini kwangu linakipaumbele sana na namuomba sana Mungu anisimamie kwa hili!
Ubarikiwe sana kwa mchango wako LWITIKO LWITIKO

Hupati mume. Machinoo sana, na halafu used sana yaani old mamalia. Labda small house.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom