Kwanza nikupongeze kwa kuona umuhimu wa mume.....
Baada ya hayo naona matatizo kadhaa kwenye bango lako ambayo ni matatizo ambayo hutokea kwenye mabango mengi hasa ya wadada..
Tatizo la kwanza ni elimu,umesema elimu yoyote lakini umesema A level ndio afadhali,huwa najiuliza sana ni kitu gani huwa kinawafanya mnahusisha elimu na ndoa,najua unahitaji ndoa a amani na furaha huku ikiwa na ridhiko la ndani,sasa elimu inahusikaje hapo? Elimu haijawahi kuboresha ndoa kabisa na shuleni hatufundishwi namna ya kubiresha ndoa isopokuwa tunafundishwa mafomula na mambo mengine ya kufanana na hayo lakini sio ndoa
Umbo,umetoa na sharti la umbo liwe na aina fulani,dada nilikuwa nadhani kwa umri wako utakuwa unajua muonekano wa nje hauna impact yoyote kwenye kuifanya ndoa kuwa ya furaha na yenye amani,sidhani kama wewe unahitaji ndoa yenye mavurugu,kipi bora,kupata mwanaume mnene au mwembamba lakini mlevi,mgomvi,asiekusikiliza na kukuheshimu au mwanaume mwenye sifa hizo bila kujali ana umbo gani?
Dini,hili nalo ni tatizo lingine,anaweza kupatikana mtu safi kabisa anaeweza kuwa mumeo lakini akawa dini tofauti au akawa hana dini,je itakuaaje hiyo?
Kwa kukushari tu ni kwamba sisemi kuwa haya hayawezekani isipokwa uwezekano wa kutokea nimdogo sana ukizingatia huo umri wa mume unaemtafuta,nasema hivyo kwasababu wengi wanakuwa tayari wako kwenye ndoa na zaidi sana Waislam mara nyingi ni wachache sana ambao wanaweza kifikia huko na akawa hajaoa kitokana na utamaduni wa dini yenyewe
Nakushauri upeleke tangazo hili na kwenye msikiti unaoswali ili uongeze uwezekano wa kimpata umtakae...
Huu ni ushauri tu usijali unaweza kuupuuza pia...
Nakutakia kila la kheri bibie.....