Msitiri anahitajika (MUME)

Msitiri anahitajika (MUME)

GCM_RCM

Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
26
Reaction score
27
Eeeh Mungu! wenye nia njema na wanione ili wanistiri na mimi!!!!

Napenda kwanza kutoa salaam kwenu nyote.

Jamani nimekuja hapa mbele yenu kwa lengo la kutafuta mwenza ili tustiriane. Najua huwa ni ya kushangaza kwa wengi pale mwanamke anapojitokeza na kuamua kutafuta mume maana haiendani na tamaduni zetu, naomba mtambue kwamba yamenifika shingoni na naona naumia moyoni kwa kusubiri hilo litokee, kwani muda unaenda na natamani hasa kuwa na mwenzangu katika dunia ya mahusiano. Naamini Mungu atanisaidia katika hili. Basi naomba kwa atakae kuwa na nia njema ajitokeze ili nami niweze kufarijika. Sifa zangu ni kama zifuatavyo;

Jinsia: KIKE
Umri:33
Elim: Degree
Kipato: Muajiriwa
Rangi:Mng'avu ila sio mweupe
Umbo: Mwembamba
Kimo: ~160cm
Dini: Islam

Sifa za mwenza
Umri:35-45
Elim: Yeyote tu ila angalau form six
Kipato: Sio lazima muajiriwa ila ni uhakika tu wa kusaidiana kutunza familia
Rangi:yeyote
Umbo: Awe wa kawaida ile sio mnene sana
Kimo: chochote tu
Dini: Islam

Kwa mawasiliano tafadhali naomba tutumie Private message (PM) au email: gcmrcm2011@gmail.com.
Natanguliza shukran zangu za dhati na nipo tayari kwa maswali yenu.
Karibuni waungwana.
 
Wa umri huo tushaoa kitambo karibia tunajukuu!,labda uwe 'chungu' cha pili!
Ila umeandika vizuri,kila la kheri!
 
Kwanza nikupongeze kwa kuona umuhimu wa mume.....

Baada ya hayo naona matatizo kadhaa kwenye bango lako ambayo ni matatizo ambayo hutokea kwenye mabango mengi hasa ya wadada..

Tatizo la kwanza ni elimu,umesema elimu yoyote lakini umesema A level ndio afadhali,huwa najiuliza sana ni kitu gani huwa kinawafanya mnahusisha elimu na ndoa,najua unahitaji ndoa a amani na furaha huku ikiwa na ridhiko la ndani,sasa elimu inahusikaje hapo? Elimu haijawahi kuboresha ndoa kabisa na shuleni hatufundishwi namna ya kubiresha ndoa isopokuwa tunafundishwa mafomula na mambo mengine ya kufanana na hayo lakini sio ndoa

Umbo,umetoa na sharti la umbo liwe na aina fulani,dada nilikuwa nadhani kwa umri wako utakuwa unajua muonekano wa nje hauna impact yoyote kwenye kuifanya ndoa kuwa ya furaha na yenye amani,sidhani kama wewe unahitaji ndoa yenye mavurugu,kipi bora,kupata mwanaume mnene au mwembamba lakini mlevi,mgomvi,asiekusikiliza na kukuheshimu au mwanaume mwenye sifa hizo bila kujali ana umbo gani?

Dini,hili nalo ni tatizo lingine,anaweza kupatikana mtu safi kabisa anaeweza kuwa mumeo lakini akawa dini tofauti au akawa hana dini,je itakuaaje hiyo?

Kwa kukushari tu ni kwamba sisemi kuwa haya hayawezekani isipokwa uwezekano wa kutokea nimdogo sana ukizingatia huo umri wa mume unaemtafuta,nasema hivyo kwasababu wengi wanakuwa tayari wako kwenye ndoa na zaidi sana Waislam mara nyingi ni wachache sana ambao wanaweza kifikia huko na akawa hajaoa kitokana na utamaduni wa dini yenyewe

Nakushauri upeleke tangazo hili na kwenye msikiti unaoswali ili uongeze uwezekano wa kimpata umtakae...

Huu ni ushauri tu usijali unaweza kuupuuza pia...

Nakutakia kila la kheri bibie.....
 
kigezo cha umri kwa muislamu kukuta hajajistiri ni ngumu...
 
Hongera GCM_RCM ubarikiwe kwa kuliweka wazi hili jangaa lilozidi miaka hii ya karibuni ( idadi ya wanawake ni kubwa ) kwa kuhakiki tumeshuhudia matangazo mengi humu....!!

Nakunyanyulia mikono juu kwa kukuombea muradi wako "Allah SubaHana wajaala akujaalie mume mwema na kizazi muruwa"
Allahuma Ameen.
 
Last edited by a moderator:

Eiyer; nimependa ushauri wako sana, nahakikisha nitaufanyia kazi bila mapungufu. Mungu akubariki sana.
 
Nadhani amekuelewa umezungumza kiume, japo hata yeye amesema maji yamemfika shingoni kila lenye heri dada legeza kidogo shart la dini na shule.

LWITIKO LWITIKO ndugu yangu, hapo kwenye shule hapana shida naweza kuwa hata na wa kidato cha nne. Ila sas hapo kwenye dini, yani hapo ni pagumu sana kwangu. Kwa upande wangu dini ni kitu muhim sana maan kitatuunganisha kiroho na kimwili pia. Hata malezi kwa watoto huwa ni rahisi sana maana hawasumbuki kuamua wapi waende hasa katik umri wao mdogo. Ukweli hili la dini kwangu linakipaumbele sana na namuomba sana Mungu anisimamie kwa hili!
Ubarikiwe sana kwa mchango wako LWITIKO LWITIKO
 
Kuwa na subra utapata tu!, km ulivyokuwa ukitafuta kazi hatimae ukapata sasa imani ile ielekezee kule ili upewe mume sahihi. Kila raheli madame! am still young tungesaidiana lakin gap ni kubwa sana. Pata kazi pata mume
 
Hongera GCM_RCM ubarikiwe kwa kuliweka wazi hili jangaa lilozidi miaka hii ya karibuni ( idadi ya wanawake ni kubwa ) kwa kuhakiki tumeshuhudia matangazo mengi humu....!!

Nakunyanyulia mikono juu kwa kukuombea muradi wako "Allah SubaHana wajaala akujaalie mume mwema na kizazi muruwa"
Allahuma Ameen.

Ameen. Shukran sana kwa dua iliyonjema!
 
Mkifikaa miaka33 mnatafutaa,elimu yoyote tu mkiwa 20 mnataka mtu mwenye masters :'(

Hapo sasa ndio ujuwe huyo kakomaa, anajua maisha sio shule tu. Tafadhali lichukulie hili positive! Maisha yanafundisha mambo mengi, ndio maana tukaambia kuwa uyaone, sasa tunayaona hayo yote.Niirahisi kujifunza kwa vitendo kuliko kwa kusikia tu, nimejifunza, nimeona na nimekiri haya yote. Ila unachosema ni kweli 90%, hasa kwa wale walio masomoni!
 
mpendwa kwenye hizo sifa zako hujataja milage ya k ikoje, kama iko chini ya 10000km nitafute, na ingine isiwe imetiwa mikono na mafundi!

Kweli hapa sijui nisemeje, hili sijui tunalipimaje jamani. Nashukuru lakini kwa ujumbe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom