msishangae matokeo ya uchaguzi kupinduliwa

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Kuanzia sasa msishangae matokeo ya uchaguzi kupinduliwa.
Kwanza, Chama chenyewe ni cha MAPINDUZI, kwa hiyo kupindua matokeo
si jambo la ajabu.
Pili, Viongozi wake wote wa juu ni Wanajeshi kitaaluma
Mwenyekiti: Luteni Kanali Jakaya Kikwete
Katibu Mkuu: Luteni Yusuf Makamba
Naibu Katibu Mkuu: Kapteni George Mkuchika
Katibu wa Itikadi/Uenezi: Kapteni john Chiligati
Meneja Kampeni: Kanali Abdulrahaman Kinana
Tatu, Gazeti la Serikali, Daily News ambalo editor in Chief ni
Rais, limeshasema: Dk. Slaa hatakuwa rais wa tano wa Tanzania
Nne: Tamko la Luteni Jenerali Shimbo linajieleza: "Wagombea
wakubali matokeo, la sivyo..."
Tano: Katiba ya nchi/ sheria ya uchaguzi iko wazi: Matokeo ya
urais yakishatangazwa, hakuna chombo chochote kinachoweza kuyapinga.
Sasa mnashangaa nini eti mnajidanganya bila kujua kuwa nchi hii ni
ya utawala wa kijeshi.
Haya muwe mnaenda kupiga kura kutimiza haki yenu ya kikatiba,
narudia tena kutimiza haki yenu ya kikatiba.
Nawasilisha;
Mkurugenzi wa Tume,
Rajab Kiravu.
Nakala: Msajili wa Vyama vya Siasa - John Tendwa,
Dk Slaa

ni Utani tu
 
Back
Top Bottom