Msipotoshe, CCM haijatawala Miaka 50

Msipotoshe, CCM haijatawala Miaka 50

kwahiyo hatujawahi kutawaliwa na mkoloni kwa vile tunaitwa Tanzania sasa?????kwa minajili hiyo ccm sio chama cha ukombozi kilichoitoa nchi yetu mikononi mwa mkoloni mzungu????

Binti Magufuli analeta hoja duni mno kiasi kwamba huenda akasababisha ama thread yake itupiwe kapuni kwa sababu ya milipuko ya wachangiaji au watu wapigwe ban humu ndani.

Vv
 
Ni uongo mkubwa kusema CCM imetawala Tanzania kwa miaka 50

taratibu naona mmeanza kukataa chimbuko na uhalisia wenu mnajidai kuwa ni chama kipya kumbe genge la wahuni na mafisadi. Hakuna namna watanzania wameshasema ccm kwaheri karibu ukawa.
 
Watetezi wengi wa Lowassa ni watoto wa 1990- na ukijumlisha na uvivu wao wa kusoma basi unapata jibu la wanayoyasema haraka tu, ukiwaona wote much know, yaani kila mtu anajua, ila ndo unawaona katika productions zao maeneno tofauti, wanalipua, wanatoa vitu ambavyo ni cheap mno, vichwani weupe zaidi ya sembe ..yaani ni hasara kwa Taifa kama kunakuwepo watu wenye soft minds kiasi hiki
 
Mbona Lodi Lofa alisema pale Jangwani kuwa CCM ilitukomboa toka kwa wakoloni?
lodilofa1.jpg
 
CCM ipo katika hatua za mwisho za urushaji mateke ya kukata roho,dalili ni nyingi,Push ups katika mikutano ya Siasa,Tafiti tata za Twawezwa na REJECT,Maandalizi kabambe ya Goli la Mkono,iga iga ya kauli mbiu,ahadi danganya toto zisizohesabika wala kutekelezeka,Kuandaa matamasha badala ya mikutano,nunua nunua ya Viongozi wasaliti na Wasanii mizigo wakati wana Mabadiliko ni Wananchi ambao hawanunuliki,sombasomba ya wanachama na wasio wanachama kwa malori na mabasi,honga honga ya fedha,kanga,vitenge,Tshirts na Kofia,kejeli na matusi kwenye majukwaa ya Siasa,kusambaratika kwa timu ya watu 32 ya Kampeni ya CCM,n.k!Wana UKAWA tunasema ‪#‎HapaZikaTu‬!..Lowassa TOSHA KABISA!!..Mwenyezi MUNGU atawaumbua kwa kila Ovu walipangalo!!!
1) 2015-1977=50.....(M4C) Mabadiliko kwa kweli!
2) 2015-1977=38.....(CCM & true History)
3) Dr.Slaa alipojitokeza kuueleza umma wa Tanzania kilichotokea majibu yalikua KANUNULIWA.
4) Dr.slaa alipoamua kutaja hadharani mafisadi...ALIUNGWA MKONO.
Sasa huu ukinyonga utatupeleka wapi??
Kwa utangulizi hapo juu hata midahalo inakimbiwa kwa kutoa sababu dhaifu.
 
Nimekupenda binti magufuli unaongea kipooooole kwa utaratibu kama mgonjwa aliyepewa mpako wa mwisho!
 
Ok Binti Magufuli, tuchukulie ni miaka 19. Hii inatutia hamasa zaidi kuiondoa CCM kwa vile kama kwa miaka kumi na tisa imebomoa na kuharibu maendeleo yote yaliyofanywa na TANU, kuna sababu gani ya kuendelea kuwaacha madarakani!
 
Last edited by a moderator:
Kubadili nembo,jina na rangi ya Kampuni au Chama hakubadili misingi,katiba,sera,utendaji wa viongozi au namuna ya uendeshaji wa kampuni au hama. Mfano kubadili jina la TANU+ASP kuwa CCM hakukubadili namuna ya kutawala siasa za Tanzania. Hivyo unaweza kusema kimsingi CCM ambayo ni mwendelezo wa TANU na ASP kimetawala kwa miaka zaidi ya 50. Maana tangu uhuru misingi ya chama kinachotawala dola ni ilele
 
All in All mabadiliko kwa kuweka (screpa) chama kikongwe hayakwepeki. Hamna namna nyingine sasa. Jaman tushirikiane kuitokomeza!!
 
Je mwaka 1961 kulikuwa na Chama cha CCM?
Ni kama vile Useme ukawa ilikuwepo tokea 2010 kwa kuwa tu vyama vya umoja huo vilikuwepo miaka hiyo.

Jiongezee

Hivi kwani mtu ukibadili jina lako na umri wako nao unabadilika?

Ama kweli ndo maana huwa nasema huwezi ukawa na akili timamu halafu bado ukawa unaiunga mkono CCM.
Binti Magufuli hebu soma haya majibu musharabu toka kwa Nyani Ngabu na kama wewe unayo akili kidogo tuu unaweza kuelewa anamaanisha nini.
 
Last edited by a moderator:
Nilifikiri kuwa kipindupindu kiko Kinondoni tu kumbe hadi Jamiiforums! Garbage
 
Utotoni mwaka 1961 mimi niliitwa Maganga lakini baadaye mwaka 1977 nikabatizwa na kuitwa Moisemusajiografii.Binti Magufuli,kwa hiyo mimi ni "watu" wawili tofauti?
 
Hivi kwani mtu ukibadili jina lako na umri wako nao unabadilika?

Ama kweli ndo maana huwa nasema huwezi ukawa na akili timamu halafu bado ukawa unaiunga mkono CCM.

Hapa umemaliza kazi ..
 
Mwendelezo ;
Umesahau na ndani ya miaka hiyo 19,
10) Sumaye amekuwa waziri mkuu kwa miaka 10, na 11)Lowasa kwa miaka karibu 3. Wakiwa kama wasimamizi wakuu wa shughuli zote za serikali.
12) ndani ya kipindi cha Sumaye, yeye ndiye aliidhinisha uuzwaji wa nyumba za serikali.
13) Richmond dili ilisimamiwa na Lowasa akiwa waziri mkuu
Naomba wengine waendeleze
Safi kabisa, naendelea
katika muda huo mfupi wa ccm magufuli ndiye aliyekuwa waziri aliyeuza nyumba za serikali na kumpa mdogo wake nyumba mbili ubungo
ni katika kipindi hicho cha utawala w ccm twiga wamepanda ndege na kuibiwa bila kujulikana na vyombo vya usalama
tembo wameuliwa sna na meli ya kinana ndio iliyokuwa inabeba pembe hizo za ndovu
madawa ya kulevya yanauzwa sana hadi na familia za vigogo hakuna hatua inayochukuliwa
epa watu wameiba fedha mabilioni mwenyekiti wa ccm akasema warudishe watasamehewa.
Escrow mabilioni yanatolewa benki cash vyombo vya uchunguzi vinakosa ushirikiano wa benki kupata majina ya waliochukua mabilioni
meremeta, gesi, mauaji ulimboka, mwangosi hakuna aliyefikishwa mahakamani
mwingine aendelee
 
Huu ndiyo ukweli na ni lazima tuuelezenchama cha mapinduzi hatujaongoza nchi kwa miaka 50 Iko hivi...

...1977 ndipo tuliunganisha vyama vya TANU na ASP na kuzaliwa CCM hivyo ccm iliiongoza tanzania toka 1977 hadi 1995
Je huo mwaka 1977, CCM ilipata wapi idhini ya kuongoza Tanzania? Je tulifanya uchaguzi? Bila shaka kwa haya maswali mawili utauona ujinga wako uliouleta JF Binti Magufuli. Kila siku mnazidi tu kulidhalilisha jamvi letu...kweli kuishabikia CCM lazima kwanza akili zishupae.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom