Msinipigie simu, na hizo hela msinipe

Msinipigie simu, na hizo hela msinipe

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
457
Reaction score
773
Achana na hustles za mtaani ndugu zangu, Jamaa yangu alihudhuria mafunzo ya ujasiriamali SIDO ili aweze kupata hela za mkopo ambazo kwa kipindi kile zilikuwa nafuu sana. Basi jamaa alitoa hela ya mafunzo akitegemea hela nyingi sana.

Mafunzo yalikwenda kwa miezi miwili walipomaliza akaambiwa asubiri, aisee alisubiri sana, alisubiri hadi akasahau kuwa kuna sehemu aliweka mchongo wa hela.

Walimpigia simu miezi 9 baadae na kumwambia hela yake ipo tayari akachukue, kipindi hiko hata wazo la biashara alililokuwa nalo awali ashalisahau alikuwa anapiga mishe nyingine. Na kimsingi alisahau kama aliomba hela ilibidi jamaa wajitambulishe.

Aliwajibu tu kwa upole msinipigie simu, namba zangu zifuteni, nisije nikala hela zenu halafu mkanifunga bure. Baadae jamaa aliishi kama wamemuharibia siku hivi.

Kwa ndugu zangu kwenye hustles za kujiajiri mshawahi kutana na kisanga kama hiki?
 
Jamaa yuko sahihi. Kama alisha elekeza nguvu zake somewhere else then aachane nao tu...mtaan only the "Daring & fearless people" survives...
 
Huwa sina tabia ya kuacha hela ambazo niliziweka kwenye target halafu nikamiss target lakin badae zikaja ku tick lazima ntazitafuna tu.
 
Kwani huyo jamaa ni mgeni na hela za Serikali? Afadhali hizo ni mikopo but unaweza kuta unadai kabisa Serikali weather ulikuwa supplier au Ulitoa huduma lakini hela kuipata unaweza chukua miaka 1 hadi zaidi.

Serikalini kuna milolongo lukuki hadi hela kutoka.

Waliofanikiwa kukopeshwa hela za Halmashauri waje watoe shuhuda zao
 
Hela za watu hizo.. Jamaa kaona badae isije kuwa noma.
 
Kama alishamove on na plans zingine, basi yuko sahihi kuzikataa. Kwanini ujiongezee madeni kizembe?
 
Jamaa kakosea, hata mabilionea huwa wanakopa. Yeye kama asliishapata plan nyingine sidhani kama amefikia level ambayo hahitaji kupanua zaidi biashara yake. Hii ilikuwa fursa muhimu sana kwake kuongeza mtaji. Sidhani kama level yake anamzidi mohamed enterprises au azam.

Ana fikra za kimasikini sana
 
Angezichukua halafu akasepa nazo huko kijijini Nyakanazi Tanzania kubwa hii hawawezi mshika
 
Back
Top Bottom