Msimamo wangu

Msimamo wangu

kwenu usikute hamna ata baiskel maisha ya mboga moja alaf unataka kutajirikia kwa mwanaume.
nyie ndo wale mnaua wanaume mnak na mali.
watu wenye pes wanaoa wanawake wenye futute kiongeza power.
huna pesa utapata wa hadhi yako

Duuuuh!! Akili zingine bwana!!! Sasa baiskeli ya kwetu inahusiana nn na misimamo yangu na mume wangu?? Hiyo ilikuwa kwetu hapa ni kwangu, napajenga kwa misingi yangu na kwa nguvu zangu.
 
Wanaume wanaujitambua, wanaume wapambanaji, wanaume halisi... wale wanaume WANAUME wanapenda mwanamke wa kumpa changamoto.
Humu wapo wanaume wachache.
 
Wanaume wanaujitambua, wanaume wapambanaji, wanaume halisi... wale wanaume WANAUME wanapenda mwanamke wa kumpa changamoto.
Humu wapo wanaume wachache.

Sanaaaaaa!!! Changamoto kidogo tu anatokwa na jasho hadi la meno, kwanza "MWANAUME" anapata wapi muda wa kucoment uozo au matusi, akitoa anatoa moja tu tena linakuwa bonge la fact, humu wapo wachache sn.
 
MSIMAMO WANGU

1. Changu ni changu, cha mume/mpenzi wangu tunashea.

2. Mwanaume bahili akae mbali na mimi.

3. Sina huruma na pesa ya mwanaume, labda atakaekuwa mume wangu wa ndoa.

4. Ntafanya majukumu yote kama mpenzi/mke wake, lakini when it comes to my money asahau, imeandikwa "mwanamke atazaa kwa uchungu na mwanaume atakula kwa jasho" so let him provide.

5. Ni marufuku mambo ya joints a/c eti mmoja wetu anaweza kutoa pesa pasipo saini ya mwingine sitaki.

6. Pesa zangu ni zangu ata password cmpi, bora nimpe Mama angu ata nikifa ajifutie nazo machozi.

7. Hata kama nina pesa kuliko yeye, mwanaume ni lazima awajibike, sio pesa ake awanufaishe wengine, maana kuna wanaume ndani wabahili ila nje wanahonga balaa.

8. Nyumba tutasaidiana kujenga, na itakuwa na jina langu na lake, au kama tutakuwa na watoto nao tutawaweka humo.

9. Ni marufuku ndugu wa mume kujihusisha na mali zetu, narudia tena ni marufuku ndugu wa mume kujisogeza karibu na mali zangu mm na mume wangu! Hizi haziwahusu kabisa tena mkae mbali.

NIMEMALIZA

Umri unakutia jeuri, Labda na kipato chako cha sasa, If you will not be careful utaishia kutumiwa na wenye Hela. Na ukaishia kuwa single mother.

Halafu, haya maneno tuu. Hutofanya any of these.

Bora ungekaa kimya.
 
Weee eli wewe! Endeleeni kubahatisha, maana nshapachikwa makibila hapa ya kila aina, kila mtu kwa mtazamo wake, mie ni mtanzania.
Kila mtz ana mahali pa asili ujuwe. Hatusemi hili ili ku promote ukabila bali ku promote utani baina ya makabila. Haya sema nijuwe kama wewe mtani wangu ama vipi!!!
 
Wanaume wanaujitambua, wanaume wapambanaji, wanaume halisi... wale wanaume WANAUME wanapenda mwanamke wa kumpa changamoto.
Humu wapo wanaume wachache.
We Da Pretty unajuwaje kama humu kuna wanaume wachache? au......................teh!
 
Last edited by a moderator:
Hata kama, huo ndio msimamo, fullstop. Kisichokufaa wewe kinamfaa mwenzio.

Ni kweli coz kama we ndo utakua umependa pengine hata hayo masharti hautayaconsider, utaishia kuyasemea humu JF na kwa wanaume wanaokupenda tu
 
We Da Pretty unajuwaje kama humu kuna wanaume wachache? au......................teh!
Wanatetea hoja kwa hisia. Ipo hivi...
Kwenye mdahalo huwa tunakubaliana kutokubaliana, sasa ukiona mtu badala ya hoja anatumia makusudi maneno mabaya unajua tu huyu kaguswa yeye kabisa.
Kuna watu humu wanajibu tu hoja haijalishi inawahusu au haiwahusu.
Ila kuna watu wanajibu kwa hisia unaona kabisa tungekua tunaonana wangepigana.
Umenielewa eeh..?
 
Last edited by a moderator:
Sanaaaaaa!!! Changamoto kidogo tu anatokwa na jasho hadi la meno, kwanza "MWANAUME" anapata wapi muda wa kucoment uozo au matusi, akitoa anatoa moja tu tena linakuwa bonge la fact, humu wapo wachache sn.

Na ningeiona mapema mbona ningepata kesi mbaya...! ningewavuruga wangekunywa sumu kwa hasira.
 
Umri unakutia jeuri, Labda na kipato chako cha sasa, If you will not be careful utaishia kutumiwa na wenye Hela. Na ukaishia kuwa single mother.

Halafu, haya maneno tuu. Hutofanya any of these.

Bora ungekaa kimya.

Eti eeeh!! Endelea kuota
 
Kuna yule mwanaume mzinzi kule anaenyatia mahausgeli na wageni wa mkewe...
ANANICHEFUA JAMANI.
Hivi yupo timamu yule?
 
Kila mtz ana mahali pa asili ujuwe. Hatusemi hili ili ku promote ukabila bali ku promote utani baina ya makabila. Haya sema nijuwe kama wewe mtani wangu ama vipi!!!

Mie mtani wako wa tanzania na asili yangu ni tanzania
 
Ni kweli coz kama we ndo utakua umependa pengine hata hayo masharti hautayaconsider, utaishia kuyasemea humu JF na kwa wanaume wanaokupenda tu

Nimependa yaani ileile na misimamo ipo palepale, and he knows it.
 
Back
Top Bottom