Msimamo wa Zitto Kabwe kuhusu Katiba mpya

Msimamo wa Zitto Kabwe kuhusu Katiba mpya

Kwenye ile orodha yako haikustahili kuweka habari za msiba, kwa maana siamini kwa hali ya kawaida msiba hauwezi kumpoteza MTU na umfanye achanganyiwe, tena mtu mwenyewe Hugo unayemdhania
Sawa! Zito yupo katika wakati mgumu.
 
Angalia kiwango cha uzalendo kati ya watanzania na wakenya ndipo utakapo gundua kuwa UKAWA hawana nia yoyote njema kwa watanzania zaidi ya kujinufaisha wao binafsi kupata madaraka kwa kutumia "divide and rule method" na hiyo ndo siri hasa ya kutaka serikali tatu hivyo usilinganishe kilicho tokea kenya na kinacho endelea tanzania , tume wagundua ukawa na hawapati kitu hapa (team ukawa a.k.a team wasaka tonge)
 
Ndio maana tunamsikitikia sana kwa kutusaliti.
chuki binafsi, ndio maana hamkwenda kwenye msiba wa mama yake,halafu mnamnanga eti ana matatizo,mnajitahidi kumtegenga hadi mnatumia msiba wa mama yake kumfrastrute!
Wabaya nyie, yaani mmejianika Sana na tunawafahamu kwa range zenu zote.
 
chuki binafsi, ndio maana hamkwenda kwenye msiba wa mama yake,halafu mnamnanga eti ana matatizo,mnajitahidi kumtegenga hadi mnatumia msiba wa mama yake kumfrastrute!
Wabaya nyie, yaani mmejianika Sana na tunawafahamu kwa range zenu zote.

Basi sawa mkuu! Wasalimie huko
 
samilakadunda unaongea kama mm vile ni mwana CCM?Hapana unakosea dada mm ni independent sina chama!

Nikiwa independents sitakiwi kutoa msimamo wangu dada Samila?
pole sana kwa kukuatack mkuu, ila swala katiba lina kera sana jamani lakini naamini mwafaka upo, sio mda mrefu. ila mimi sio DADA mkuu, ni mwanaume kamili.
 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh Zitto Kabwe amesema kamwe hatajiunga Muungano wa Umoja wa Katiba (UKAWA) kwa kuwa baadhi yao nia yao nikuvunja Muungano na Wamejificha kwenye kivuli cha Serikali tatu.

CHANZO:MWANANCHI
 
Last edited by a moderator:
Hivi huyu mfesenge anatafuta kick kwa staili gani?kuna mtu aliwahi kumuomba aingie ukawa?aache kujipendekeza mambo ya ukawa atuachie ukawa wenyewe.Na asipoangalia atajikuta anajifanya chizi kwenye kundi la wapumbavu(ccm)
 
Hivi huyu mfesenge anatafuta kick kwa staili gani?kuna mtu aliwahi kumuomba aingie ukawa?aache kujipendekeza mambo ya ukawa atuachie ukawa wenyewe.Na asipoangalia atajikuta anajifanya chizi kwenye kundi la wapumbavu(ccm)

yaani huyo mrundi mxenge sijapata ona. kazi wafanye wengine, sifa ajipatie yeye manina namdharau kama ma^i anakera sana.
 
Dar es Salaam. Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amesema hawezi kujiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa sababu baadhi ya wajumbe wa umoja huo hawautaki Muungano na wamejificha nyuma ya pazia la kutaka muundo wa serikali tatu.

Amesema si kila mtu anayetaka serikali tatu anaupenda Muungano na kusisitiza kuwa ni aibu kuwa na marais watatu ndani ya nchi moja.

“Msimamo wangu wa serikali tatu si msimamo wa marais watatu kwa sababu najua msimamo wa marais watatu utavunja nchi. Msimamo wangu ni rais mmoja wa Jamhuri ya Muungano, Mkuu wa Serikali Zanzibar na Mkuu wa Serikali Bara,” alisema.

Zitto ambaye alivuliwa nyadhifa zake zote ndani ya Chadema, moja ya vyama vinavyounda Ukawa, alitoa ufafanuzi huo wiki iliyopita katika mahojiano maalumu na gazeti hili nyumbani kwake Masaki, Dar es Salaam.

Pamoja na Chadema, Ukawa inaundwa na vyama vya CUF na NCCR-Mageuzi pamoja na wajumbe wachache wa Kundi la 201 ambao walisusia vikao vya Bunge Maalumu la Katiba tangu Aprili 16, mwaka huu, wakitaka ijadiliwe Rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Marekebisho ya Katiba yenye kupendekeza muungano wa serikali tatu badala ya mbili zinazopendekezwa na CCM.

Akieleza sababu za kutoungana na Ukawa, Zitto alisema baadhi ya wajumbe wake wanasema njia nyepesi ya kubakia na Zanzibar ni serikali tatu, wengine wanasema njia nyepesi ya kubakia na Tanganyika ni serikali tatu, “Binafsi ni muumini wa Muungano na dola duniani kote hazivunjwi, bali zinaimarishwa.”

Kuhusu muungano anaoupendekeza alisema: “Chama chenye wawakilishi wengi kwenye Baraza la Wawakilishi Zanzibar kitatoa Mkuu wa Serikali Zanzibar na chama chenye wabunge wengi Baraza la Wawakilishi Tanganyika kitatoa Mkuu wa Serikali Tanganyika na Bunge liwe moja.”

Alisema anachofikiria ni namna ya kuzifanya nchi za Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya zinakuwa pamoja na Tanzania na si kujadili namna ya kuzitenganisha na Tanzania.

“Tumeona Ethiopia na Eritrea zilivyotengana. Nini kimetokea pale Wasudani walipoamua kujitenga wenyewe kwa wenyewe. Tujifunze kwa mifano hii, hatuwezi kuwa na wakuu wa nchi watatu ndani ya nchi moja, tutachekwa na dunia. “Lakini kwa sababu wenye sauti za kuukataa muungano ni wengi zaidi katika Ukawa lakini hawawezi kujionyesha, mimi siwezi kuwa nao na nipo wazi kabisa.”

Alisema Ukawa walimwalika katika vikao Dodoma wakati Bunge la Katiba linaanza lakini aliwakatalia na kuwaeleza kuwa miongoni mwao wapo wanaotaka muungano uvunjike.

Kuhusu kuingia bungeni alisema: “Siendi katika vikao vya Bunge la Katiba kwa sababu ni kupoteza muda tu. Huwezi kutengeneza Katiba ya nchi bila maridhiano. Lazima mridhiane ndipo mkae mtengeneze. Katiba haina mshindi.”

Alisema kitendo cha baadhi ya wajumbe kususia vikao na wengine kuendelea si jambo la kufurahia kwa kuwa Katiba inaweza kupata uhalali wa kisheria lakini ikakosa uhalali wa kisiasa.


Chanzo: Mwananchi


 
Hoja ya zitto ina mashiko kwa kiasi flani.. kuna wakati ni bora ukabaki neutral
 
tatizo sio kuwa neutral ni hoja ya msingi. Je hapo kuna hoja? Kama kuna hoja ya msingi tuijadili.
 
Back
Top Bottom