Msimamo wa wahisani juu ya Zanzibar leo

Msimamo wa wahisani juu ya Zanzibar leo

Mbona marekani sisi hatuendi kuwa watazamaji wa uchaguzi wao? Mbona hata aibu hawaoni!? Nini lakini ,sisi mbona hatujasema chochote kuhusu wanavyomlushia mabango mgombea wao wa urais Donald Trump kiboko yao. Go Zanzibar Go shein Go Magufuli Go beloved Tanzania
 
21 Machi 2016 Tamko La Pamoja Kuhusu Uchaguzi Wa Marudio Visiwani Zanzibar Mabalozi na wawakilishi wa nchi za Ubelgiji, Canada, Denmark, Umoja wa Ulaya, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Ireland, Italia, Uholanzi, Norway, Hispania, Sweden, Switzerland, Uingereza na Marekani hivi leo wametoa tamko kuhusu uchaguzi wa marudio uliofanyika Zanzibar tarehe 20 Machi 2016: “Tumesikitishwa na uamuzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) wa kuendesha marudio ya uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba 2015, bila kuwepo makubaliano ya pamoja baina ya pande kinzani na ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa visiwani humo uliotokana na majadilino baina ya pande husika. “Ili uwe wa kuaminika na kukubalika ni lazima mchakato wa uchaguzi uwe jumuishi na unaowakilisha kwa dhati matakwa ya watu. “Tunarejea wito wetu kwa Serikali ya Tanzania kuonyesha na kuchukua uongozi katika suala la Zanzibar na kujielekeza katika kupatikana kwa ufumbuzi wa mgogoro huu kwa kupitia mazungumzo baina ya pande husika kwa lengo la kudumisha amani na umoja katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. “Kwa mara nyingine tunawapongeza wananchi wa Zanzibar kwa utulivu na ustahimilivu waliouonyesha katika kipindi chote cha mchakato huu na kuvitaka vyama vyote na wafuasi wao kuanzisha tena mchakato wa maridhiano ya kitaifa ili kupata ufumbuzi jumuishi, endelevu na wa amani.”



March 21, 2016 JOINT STATEMENT ON ELECTION RE-RUN IN ZANZIBAR The High Commissioners and Ambassadors to Tanzania of Belgium, Canada, Denmark, the European Union, Finland, France, Germany, Ireland, Italy, the Netherlands, Norway, Spain, Sweden, Switzerland, the United Kingdom and the United States, today issued the following statement regarding the election re-run which took place in Zanzibar on March 20th, 2016: “We regret the Zanzibar Electoral Commission’s decision to hold a re-run of the 25 October 2015 election, without a mutually acceptable and negotiated solution to the current political impasse. “In order to be credible, electoral processes must be inclusive and truly representative of the will of the people. “We reiterate our call on the Government of Tanzania to exercise leadership in Zanzibar, and to pursue a negotiated solution between parties, with a view to maintaining peace and unity in the United Republic of Tanzania. “We commend once again the population of Zanzibar for having exercised calm and restraint throughout this process, and call on all parties and their supporters to re-start the national reconciliation process to find an inclusive, sustainable and peaceful resolution.
Hakuna haja kuendeleza majadiliako kwa watu waliosusa majadiliano kwani pesa zitaendelea kutumika tu,uchaguzi umeisha la msingi tupige hatua mbele za kimaendeleo. Matamko ya kichochezi kila siku tumeyachoka wakayatoe kwa Trump
 
Kwa kumbukumbu zangu zisizo rasmi siku 25 kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana utawala wa kikwete ulipatiwa mamilioni ya dola kwa ajili ya umeme vijijini lakini mara tu utawala huu mpya kuingia madarakani haukukaa hata mwezi mmoja watoa msaada wakauzuia msaada huo kwa maelezo ya kutoridhika na uchaguzi wa zanzibar na sasa kwa tamko hili tukae mkao wa kukaza mikanda huenda vikwazo zaidi vya kiuchumi vikatuhusu

na hivi mvua zilivyogoma kuivisha mazao mashambani mwaka mbona utakuwa mgumu kwa sisi walalahoi mungu tuokoe na balaa hili
 
Mbona marekani sisi hatuendi kuwa watazamaji wa uchaguzi wao? Mbona hata aibu hawaoni!? Nini lakini ,sisi mbona hatujasema chochote kuhusu wanavyomlushia mabango mgombea wao wa urais Donald Trump kiboko yao. Go Zanzibar Go shein Go Magufuli Go beloved Tanzania
Huwezi kusimamia uchaguzi wa watu walokuzidi ubavu. Sisi tunaenda kusimamia chaguzi za S. Sudan, Burundi and alike! Ni sawa na mwalimu mwenye diploma hawezi kusimamia mitihani ya Master degree, kitu hicho hakiwezekani! Au mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kusimamia uchaguzi mkuu wa Raisi wa ST
 
Katiba ya Tanzania inawalinda sana Wazanzibari.

Mwaka 1995 na 2000 tuliona kilichofanyika Zanzibar ndicho kinachofanyika kwa sasa.

Zanzibar ni nchi ndani ya nchi!

Utamlaumu tu Rais wa Tanzania kama kuna overwhelming lack of peace and security in Zanzibar.

Hata Waingereza wanafahamu, sio yote yanayoendelea ndani ya Scotland unaweza kumlaumu Waziri Mkuu wa Uingereza kwa sababu Scotland ndani ya UK kwa kiwango kikubwa ni sawa na Zanzibar ndani ya Tanzania.
 
Huwezi kusimamia uchaguzi wa watu walokuzidi ubavu. Sisi tunaenda kusimamia chaguzi za S. Sudan, Burundi and alike! Ni sawa na mwalimu mwenye diploma hawezi kusimamia mitihani ya Master degree, kitu hicho hakiwezekani! Au mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kusimamia uchaguzi wa Raisi mkuu wa ST
maoni yako nini kuna chuo kifunza wapi mataifa kusimamia uchaguzi?
 
Mimi hata mambo ya Zanzibar sasa hivi sihangaiki nayo ,watu wamepewa ushauri wameona kurudia uchaguzi ndio suluhisho la matatizo ya Wanzanzibar,
Waliorudia uchaguzi pengine wana njia nyingine ngoja tuone vinginevyo tunampigia tu mbuzi gitaa
 
Katiba ya Tanzania inawalinda sana Wazanzibari.

Mwaka 1995 na 2000 tuliona kilichofanyika Zanzibar ndicho kinachofanyika kwa sasa.

Zanzibar ni nchi ndani ya nchi!

Utamlaumu tu Rais wa Tanzania kama kuna overwhelming lack of peace and security in Zanzibar.

Hata Waingereza wanafahamu, sio yote yanayoendelea ndani ya Scotland unaweza kumlaumu Waziri Mkuu wa Uingereza kwa sababu Scotland ndani ya UK kwa kiwango kikubwa ni sawa na Zanzibar ndani ya Tanzania.

Kama hao Waingereza wanapata wapi ujasiri wa kupiga domo wakati wana majibu ya muda mrefu kama Gibraltar, the Foklands?
 
Hakuna lolote hapo, hao wazungu wanatazama maslahi yao tu. Watasahau yote haya baada ya mwezi mmoja tu. Raia wao watakuja na kupewa maene wajenge hotel, serikali itatoa order ya vifaa vya kivita kutoka kwenye hizo nchi na hapo ndio kazi itakua imekwisha.
 
Back
Top Bottom