Msimamo wa Jeshi la Polisi kufuatia mauaji ya Raia Arusha

Chonde chonde wana chadema. someni alama za nyakati. Kama nilivyowahi kusema huko nyuma chadema wametengeneza uadui na mamlaka inayotawala kwa hiyo wasitarajie mteremko katika mambo yao. Inapofikia unasusa hata sherehe za UHURU wa nchi yetu basi jua matokeo ya baadaye na ujiandae vilivyo.

Msitarajie kuwa watakaokufa na kuumia kwa sababu ya propaganda za kuingia IKULU kwa nguvu na umwagaji damu ni raia wasio na hatia pekee bali hata viongozi , watoto ,wake na au mahawara wao pia yatawapata madhara. Kuweni waangalifu sana na mtii amri/ushauri wa mamlaka inayotawala. Kama kuna mambo hayaendi sawa basi tumieni njia za kistaarabu pamoja na kwenda mahakamani kudai haki. Nabii SULEIMAN alisifika kwa HEKIMA na sio VISASI NA KUSUSA kike kike.

Chonde chonde, japo tunajua wazi kuwa KANISA lipo nyuma yenu lakini watanzania wapenda AMANI hatuko tayari kuona kikundi kidogo kikiharibu usalama na amani yetu.
Siku ikifika hayo mahekalu na madhabahu wanayojifichia yatageuka kuwa ndiyo makaburi yenu na yao pia. Rwanda sio mbali na 1994 sio mbali pia. Mtakumbuka kuwa maiti nyingi zilikutwa Makanisani. Tugeuke nyuma na tuangalie wapi tumejikwaa. Akili za kuambiwa changanya na zako!

Naandika haya nikichelea kuwa pasije kusemwa: "HAPAKUWEPO WENYE HEKIMA NDIO MAANA TUMEANGAMIA".

KAGUMYAMHETO umetumwa! kutoa ujumbe wa mauaji kwa viongozi wa vyama vya siasa! wambie waliokutuma kwamba mahakama ya kimataifa inawaita, wasidhani watamwaga damu tu na wao wawe salama wakila kuku na kusherekea 'birthday' na familia zao salama daima dumu!
 
Chonde chonde wana chadema. someni alama za nyakati. Kama nilivyowahi kusema huko nyuma chadema wametengeneza uadui na mamlaka inayotawala kwa hiyo wasitarajie mteremko katika mambo yao. Inapofikia unasusa hata sherehe za UHURU wa nchi yetu basi jua matokeo ya baadaye na ujiandae vilivyo.

Msitarajie kuwa watakaokufa na kuumia kwa sababu ya propaganda za kuingia IKULU kwa nguvu na umwagaji damu ni raia wasio na hatia pekee bali hata viongozi , watoto ,wake na au mahawara wao pia yatawapata madhara. Kuweni waangalifu sana na mtii amri/ushauri wa mamlaka inayotawala. Kama kuna mambo hayaendi sawa basi tumieni njia za kistaarabu pamoja na kwenda mahakamani kudai haki. Nabii SULEIMAN alisifika kwa HEKIMA na sio VISASI NA KUSUSA kike kike.

Chonde chonde, japo tunajua wazi kuwa KANISA lipo nyuma yenu lakini watanzania wapenda AMANI hatuko tayari kuona kikundi kidogo kikiharibu usalama na amani yetu.
Siku ikifika hayo mahekalu na madhabahu wanayojifichia yatageuka kuwa ndiyo makaburi yenu na yao pia. Rwanda sio mbali na 1994 sio mbali pia. Mtakumbuka kuwa maiti nyingi zilikutwa Makanisani. Tugeuke nyuma na tuangalie wapi tumejikwaa. Akili za kuambiwa changanya na zako!

Naandika haya nikichelea kuwa pasije kusemwa: "HAPAKUWEPO WENYE HEKIMA NDIO MAANA TUMEANGAMIA".

Huna hekima hata chembe!! Nahisi wakati unazaliwa ulipitia kwenye tigo au mdomoni!! kinyesi au matapishi tu.
 
Jeshi la polisi la makaburu lilikuwa na nguvu sana, lilikuwa katiri kuliko jeshi lenu, liliua raia wengi wasiokuwa na hatia lakini bado lilisalimu amri na kushindwa katika mapambano na nguvu ya umma!!! Ni nawaahidi kuwa polisi na vikaragosi vyao wote watashindwa na Wananchi wa Tanzania watashinda na kuwaondoa madarakani mafisadi wote na wafuasi wao.
 
JESHI la Polisi nchini limesema lililazimika kutumia risasi za moto dhidi ya waandamanaji wa Chadema, ili kujihami na kuhami kituo chake kilichokuwa kinakaribia kuvamiwa.

“Polisi ililazimika kutumia mbinu za kujihami na kukihami kituo ili kunusuru utekaji wa kituo hicho ambacho kilikuwa na silaha nyingi nzito, katika mazingira hayo risasi za moto ililazimika
kutumika, matokeo yake vikatokea vifo na majeruhi,” hiyo ni kauli ya Mkurugenzi wa Operesheni wa Polisi, Kamishna Paul Chagonja.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Chagonja alisema matatizo yaliyojitokeza Januari 5 mwaka huu Arusha na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine 14 kujeruhiwa, yalitokana na uhamasishaji na uchochezi wa viongozi wa kitaifa wa Chadema katika mkutano wa hadhara.

Alisema maandamano ya chama hicho yalizuiwa baada ya taarifa za kiintelijensia kuonesha kwamba kuna tishio kubwa la kiusalama lililolenga kuharibu sura ya Jiji la Arusha kwenye uso wa dunia, ikizingatiwa kwamba ni Jiji la kitalii.

Aliongeza kwamba haki ya maandamano na mikutano ya hadhara ni ya msingi na Polisi inatakiwa kuhakikisha yanafika kwa usalama na njia zinazopitwa ni salama pia, lakini baada ya maandamano hayo kuzuiwa, na Chadema kukataa kutumia njia mbili zilizopendekezwa na Jeshi hilo, isivyo halali wapenzi na wanachama walifanya maandamano ambayo yalisitishwa na Polisi.

Njia ya kwanza ilikuwa ya kuanzia Philips, Sanawari Mataa na kushika na barabara ya AICC kupitia Goliondi, Sokoine, Friends Corner na kuingia uwanbja wa NMC.

Njia ya pili ilipendekezwa ya kuanzia Philips, Sanawari Mataa, Mianzini Mataa, Florida Annex, kituo cha mabasi, benki ya CRDB kupitia Friends Corner hadi uwanja wa NMC.

Kwa mujibu wa Kamishna Chagonja, Polisi iliwapa uhuru huo kwa kuwa siku hiyo ilikuwa ya kazi na wananchi wengine walitakiwa kuwa na uhuru wa kuendelea na shughuli zao bila kuathiriwa.

Alisema chama hicho kilitakiwa kutoa taarifa mapema kuhusu njia waliyochagua, ili Polisi ijipange lakini Januari 3 mwaka huu, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha Mjini, alipokea barua ya chama hicho, ikimjulisha kuwa maandamano yataanzia Philips na msafara wa Dk. Slaa ungeanzia uwanja mdogo wa ndege Kisongo.

Maandamano hayo kwa mujibu wa barua hiyo iliyosainiwa na Magoma Derick, Mwenyekiti wa Chadema wilaya, yalipangwa na chama hicho kukutana Annex Hotel na kuelekea katika uwanja wa mkutano.

Kamishna Chagonja alisema, barua hiyo ilionesha kuwa chama hicho kimekiuka utaratibu wa kutakiwa kuchagua njia moja, na badala yake wakaongeza njia ya pili ya maandamano ya Dk. Willibrod Slaa kinyume na maelekezo ya Polisi.

Alisema wakati wanafanya mawasiliano na chama hicho kuwekana sawa, ndipo taarifa za kiintelijensia zilipoonesha kuwepo kwa tishio hilo la kiusalama na Polisi ikalazimika kuzuia na kukubali kutoa ulinzi katika mkutano.

“Kitendo cha kusitisha maandamano hakikusababisha matatizo makubwa, isipokuwa uchochezi wa maneno ya wazungumzaji kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya NMC na kusababisha mihemko na jazba za wafuasi na wapenzi wa Chadema na kuzua ghasia na kutaka kuvamia kituo kikuu cha Polisi,” alisema.

Alisema kabla ya hapo, saa 5 asubuhi siku hiyo, wapenzi na wanachama wa chama hicho isivyo halali waliandamana zaidi ya kilometa moja wakitokea hoteli ya Mount Meru kwenda viwanja vya NMC kwenye mkutano huo.

Chagonja alisema Polisi iliwaamuru waandamanaji kusitisha maandamano hayo mara moja, baada ya kuona yataleta uvunjifu wa amani kutokana na jazba ya waandamanaji hao.

Hata hivyo, alisema amri hiyo ilipuuzwa na maandamano kuendelea, matokeo yake viongozi saba na wafuasi kadhaa walikamatwa na kufikishwa kituo kikuu cha Polisi kwa hatua zaidi na maandamano hayo kuzimwa, na hali ya utulivu ikarejea na mkutano ukafanyika.

“Katika mkutano huo maneno ya uchochezi na uhamasishaji yalitolewa ili watu wafanye vurugu na waende kituo cha Polisi kuvamia na kuwatoa kwa nguvu watuhumiwa waliokamatwa … ulifanywa na Dk. Willibrod Slaa Katibu Mkuu, Philemon Ndesamburo, Mbunge wa Moshi Mjini na Mwenyekiti wa Mkoa, Samson Mwigamba,” alisema.

Alisema kwa hamasa hiyo wafuasi wa Chadema wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 3,000 waliitikia mwito wa viongozi wao na kuelekea kituo hicho kuwatoa kwa nguvu watuhumiwa waliokuwa mahabusu.

Wakiwa njiani kuelekea kituo hicho, walichoma moto duka na kuharibu vibanda vya biashara, walivamia kituo kidogo cha Polisi cha Unga Limited na kufanya uharibifu mkubwa wa mali, miundombinu ya shule ya msingi Kaloleni, ofisi ya CCM ya mkoa, magari ya Polisi na raia na kuvamia vituo vya Polisi vya Maraa na Kaloleni kwa nia ya kuvichoma moto.

“Walipokaribia kituo kikuu cha Polisi umbali wa meta 50 huku wakirusha mawe, chupa, fimbo, nondo, mapanga na visu, amri halali na hadhari za msingi zilizotolewa kuwataka watawanyike mara moja, lakini walikaidi amri na kuzidi kukaribia kituo kwa lengo la kutimiza azma yao ya kukivamia,” alisema.

Alisema baada ya maonyo hayo kupuuzwa, yalipigwa mabomu ya kutoa machozi, lakini bado walikaidi na kusonga mbele, zilitumika risasi baridi na mabomu ya vishindo wakakaidi na kuzidi kukaribia kituo cha Polisi, na hatimaye kupigwa risasi juu za onyo lakini wakaendelea kusonga mbele.

“Kilichofuatia ni mapambano ya ana kwa ana kati ya askari na waandamanaji waliokuwa wakisonga mbele kuvamia kituo ambapo polisi walilazimika kutumia mbinu za kujihami na kukihami kituo … katika mazingira hayo risasi za moto ililazimika kutumika,” alisema.

Alisema walilazimika kufanya hivyo kutokana na historia kuonesha kwamba mwaka jana vituo vingi vya Polisi vilivamiwa na kuchomwa moto na polisi kuuawa, hivyo waliona yangetokea maafa makubwa kama maandamano hayo yasingezuiwa Hata hivyo alisema operesheni ya

kurejesha amani na utulivu imekamilika na sasa Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, kwa kushirikiana na timu ya wadau wengine wa usalama, wanaendelea na uchunguzi ili kuona matukio yoyote ya makosa ya kiutendaji na mengine ya
kijinai yaliyotendwa kwa upande wa Chadema na viongozi wao.

Katika hatua nyingine, alisema ni lazima mamlaka zilizopo, sheria na Katiba zifuatwe na viongozi waliopo madarakani wasidhalilishwe wala kukebehiwa na kuwataka wenye tatizo wafikishe ujumbe kwa njia sahihi badala ya kumgeuza kiongozi kama tambara la deki.

Alisema kuwa anashangazwa kuona viongozi wa Chadema wakiwa na simanzi wakati kazi hiyo wameifanya wenyewe na kusababisha vifo hivyo kwa sababu Polisi isingewafuata wananchi nyumbani mwao na kuwapiga risasi kama wasingeandamana.
 
Nimependa tamko la polisi! Wameeleweka vizuri sana! Chadema aibu yao!

Vp kuhusu wafanyabiashara wa Mahenge na dereva taxi, Mtui na mwenzake waliopigwa risasi Kijenge Arusha ....Arusha hivi majuzi tu.

watakuwa wanaku-dosana ndio maana unaona ni sawa tu.
 
Msishangae ndugu Watanzania kuona taarifa za kejeli kama hii,mimi binafsi kama mtu niliyezoea kuendeshwa kwa mazoea na serikali hii dhalimu naona kawaida na nlitegemea pia kitu kama hicho.Sina mengi sana ila maswali machache kwa huyo kamanda wa operesheni arusha.
1.Kibali cha maandamano kilieleza zitumike njia zipi na kwanini mwanzoni jeshi lako liliwalinda kuanzia tengeru na mkawafanyia uharamia tank la maji?
2.Katika taarifa hiyo ya kejeli kwanini hakuna lile zoezi la polisi aliyemnyang'anya simu mfukoni Luccy Owenya na kupasua vioo vya gari lake?
3.Kwanini mliwafukuza waandishi wa habari,mkawalazimisha kufuta picha walizokuwa wamepiga na kuwakamata na kuwatesa?
4.Kulikuwa na njama gani za kudanganya jina la marehemu Paul Njuguma ambaye ni Mkenya kwa kudanganya anaitwa Mwita Waitara wa Mara?
5.Je wale wasafiri waliopigwa pale stand akiwemo Njuguna aliyeuwawa nao waliandamana?
6.Siku hizi ruhusa ya maandamano hutolewa kwa maandishi na kukanushwa kwa mdomo?
7.Polisi siku hizi imekuwa taasisi ndani ya chama kama UVCCM?
8.Kwanini polisi imetoa taarifa na kukimbia ukumbini bila ufafanuzi na kujibu maswali?
9.Kama mawaziri wote isipokuwa Makamba<mpigaramli>wamekiri kuwa mlikosea na nyinyi mmetoa taarifa ya kibabe,mnafanyia kazi jamhuri ya Ivory coast au Tanzania?na rais wenu na amiri jeshi mkuu ni nani?
10.wale ambao moja ya magazeti hapa nchini yaliandika mmewazika kama mbwa,mnadhani kwamba Mungu hufichwa?kama ndio mbona mliumbuka kule Mbeya mlikokua mkichukua rushwa hadharani?
Mimi kama walivyo watanzania wengine tukipata majibu ya angalau hayo maswali 10 tutaanza angalau kuisoma hiyo taarifa yenu japo inanuka na itachafua hata mikono yetu.
 
choosew.jpg
 
Nyie pongo risasi zetu zimeua tena ndg na walipa kodi jifunzeni toka kwenye Biblia "Heri kuwa na maarifa kuliko kuwa na nguvu ..." Oooh tunataarifa za kiintelejinsia, maran oooh tulifanya kazi yetu.Leo kwenye press conf mmeogopa maswali. Mnanuka aibu aibu aibu
 
JESHI la Polisi nchini limesema lililazimika kutumia risasi za moto dhidi ya waandamanaji wa Chadema, ili kujihami na kuhami kituo chake kilichokuwa kinakaribia kuvamiwa.

“Polisi ililazimika kutumia mbinu za kujihami na kukihami kituo ili kunusuru utekaji wa kituo hicho ambacho kilikuwa na silaha nyingi nzito, katika mazingira hayo risasi za moto ililazimika
kutumika, matokeo yake vikatokea vifo na majeruhi,” hiyo ni kauli ya Mkurugenzi wa Operesheni wa Polisi, Kamishna Paul Chagonja.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Chagonja alisema matatizo yaliyojitokeza Januari 5 mwaka huu Arusha na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine 14 kujeruhiwa, yalitokana na uhamasishaji na uchochezi wa viongozi wa kitaifa wa Chadema katika mkutano wa hadhara.

Alisema maandamano ya chama hicho yalizuiwa baada ya taarifa za kiintelijensia kuonesha kwamba kuna tishio kubwa la kiusalama lililolenga kuharibu sura ya Jiji la Arusha kwenye uso wa dunia, ikizingatiwa kwamba ni Jiji la kitalii.

Aliongeza kwamba haki ya maandamano na mikutano ya hadhara ni ya msingi na Polisi inatakiwa kuhakikisha yanafika kwa usalama na njia zinazopitwa ni salama pia, lakini baada ya maandamano hayo kuzuiwa, na Chadema kukataa kutumia njia mbili zilizopendekezwa na Jeshi hilo, isivyo halali wapenzi na wanachama walifanya maandamano ambayo yalisitishwa na Polisi.

Njia ya kwanza ilikuwa ya kuanzia Philips, Sanawari Mataa na kushika na barabara ya AICC kupitia Goliondi, Sokoine, Friends Corner na kuingia uwanbja wa NMC.

Njia ya pili ilipendekezwa ya kuanzia Philips, Sanawari Mataa, Mianzini Mataa, Florida Annex, kituo cha mabasi, benki ya CRDB kupitia Friends Corner hadi uwanja wa NMC.

Kwa mujibu wa Kamishna Chagonja, Polisi iliwapa uhuru huo kwa kuwa siku hiyo ilikuwa ya kazi na wananchi wengine walitakiwa kuwa na uhuru wa kuendelea na shughuli zao bila kuathiriwa.

Alisema chama hicho kilitakiwa kutoa taarifa mapema kuhusu njia waliyochagua, ili Polisi ijipange lakini Januari 3 mwaka huu, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha Mjini, alipokea barua ya chama hicho, ikimjulisha kuwa maandamano yataanzia Philips na msafara wa Dk. Slaa ungeanzia uwanja mdogo wa ndege Kisongo.

Maandamano hayo kwa mujibu wa barua hiyo iliyosainiwa na Magoma Derick, Mwenyekiti wa Chadema wilaya, yalipangwa na chama hicho kukutana Annex Hotel na kuelekea katika uwanja wa mkutano.

Kamishna Chagonja alisema, barua hiyo ilionesha kuwa chama hicho kimekiuka utaratibu wa kutakiwa kuchagua njia moja, na badala yake wakaongeza njia ya pili ya maandamano ya Dk. Willibrod Slaa kinyume na maelekezo ya Polisi.

Alisema wakati wanafanya mawasiliano na chama hicho kuwekana sawa, ndipo taarifa za kiintelijensia zilipoonesha kuwepo kwa tishio hilo la kiusalama na Polisi ikalazimika kuzuia na kukubali kutoa ulinzi katika mkutano.

“Kitendo cha kusitisha maandamano hakikusababisha matatizo makubwa, isipokuwa uchochezi wa maneno ya wazungumzaji kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya NMC na kusababisha mihemko na jazba za wafuasi na wapenzi wa Chadema na kuzua ghasia na kutaka kuvamia kituo kikuu cha Polisi,” alisema.

Alisema kabla ya hapo, saa 5 asubuhi siku hiyo, wapenzi na wanachama wa chama hicho isivyo halali waliandamana zaidi ya kilometa moja wakitokea hoteli ya Mount Meru kwenda viwanja vya NMC kwenye mkutano huo.

Chagonja alisema Polisi iliwaamuru waandamanaji kusitisha maandamano hayo mara moja, baada ya kuona yataleta uvunjifu wa amani kutokana na jazba ya waandamanaji hao.

Hata hivyo, alisema amri hiyo ilipuuzwa na maandamano kuendelea, matokeo yake viongozi saba na wafuasi kadhaa walikamatwa na kufikishwa kituo kikuu cha Polisi kwa hatua zaidi na maandamano hayo kuzimwa, na hali ya utulivu ikarejea na mkutano ukafanyika.

“Katika mkutano huo maneno ya uchochezi na uhamasishaji yalitolewa ili watu wafanye vurugu na waende kituo cha Polisi kuvamia na kuwatoa kwa nguvu watuhumiwa waliokamatwa … ulifanywa na Dk. Willibrod Slaa Katibu Mkuu, Philemon Ndesamburo, Mbunge wa Moshi Mjini na Mwenyekiti wa Mkoa, Samson Mwigamba,” alisema.

Alisema kwa hamasa hiyo wafuasi wa Chadema wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 3,000 waliitikia mwito wa viongozi wao na kuelekea kituo hicho kuwatoa kwa nguvu watuhumiwa waliokuwa mahabusu.

Wakiwa njiani kuelekea kituo hicho, walichoma moto duka na kuharibu vibanda vya biashara, walivamia kituo kidogo cha Polisi cha Unga Limited na kufanya uharibifu mkubwa wa mali, miundombinu ya shule ya msingi Kaloleni, ofisi ya CCM ya mkoa, magari ya Polisi na raia na kuvamia vituo vya Polisi vya Maraa na Kaloleni kwa nia ya kuvichoma moto.

“Walipokaribia kituo kikuu cha Polisi umbali wa meta 50 huku wakirusha mawe, chupa, fimbo, nondo, mapanga na visu, amri halali na hadhari za msingi zilizotolewa kuwataka watawanyike mara moja, lakini walikaidi amri na kuzidi kukaribia kituo kwa lengo la kutimiza azma yao ya kukivamia,” alisema.

Alisema baada ya maonyo hayo kupuuzwa, yalipigwa mabomu ya kutoa machozi, lakini bado walikaidi na kusonga mbele, zilitumika risasi baridi na mabomu ya vishindo wakakaidi na kuzidi kukaribia kituo cha Polisi, na hatimaye kupigwa risasi juu za onyo lakini wakaendelea kusonga mbele.

“Kilichofuatia ni mapambano ya ana kwa ana kati ya askari na waandamanaji waliokuwa wakisonga mbele kuvamia kituo ambapo polisi walilazimika kutumia mbinu za kujihami na kukihami kituo … katika mazingira hayo risasi za moto ililazimika kutumika,” alisema.

Alisema walilazimika kufanya hivyo kutokana na historia kuonesha kwamba mwaka jana vituo vingi vya Polisi vilivamiwa na kuchomwa moto na polisi kuuawa, hivyo waliona yangetokea maafa makubwa kama maandamano hayo yasingezuiwa Hata hivyo alisema operesheni ya

kurejesha amani na utulivu imekamilika na sasa Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, kwa kushirikiana na timu ya wadau wengine wa usalama, wanaendelea na uchunguzi ili kuona matukio yoyote ya makosa ya kiutendaji na mengine ya
kijinai yaliyotendwa kwa upande wa Chadema na viongozi wao.

Katika hatua nyingine, alisema ni lazima mamlaka zilizopo, sheria na Katiba zifuatwe na viongozi waliopo madarakani wasidhalilishwe wala kukebehiwa na kuwataka wenye tatizo wafikishe ujumbe kwa njia sahihi badala ya kumgeuza kiongozi kama tambara la deki.

Alisema kuwa anashangazwa kuona viongozi wa Chadema wakiwa na simanzi wakati kazi hiyo wameifanya wenyewe na kusababisha vifo hivyo kwa sababu Polisi isingewafuata wananchi nyumbani mwao na kuwapiga risasi kama wasingeandamana.
 
This is the Best Defense Statement Ever. Mbona Risasi Hazifyatuki Kwenye Sherehe za Muungano na Uhuru Viwanjani? Mbona JK na Mafisadi Wakilindwa Mabarabarani Mbona Sija Wahi Kusikia Risasi Zikifyatuka kwa Bahati Mbaya? Kama ni Kweli "Polisi Wamesema Haya" ni Kumkamata Huyo Aliesema na Apigwe Mawe Hadharani. "Demokrasia ya Chooni Hii"
 
Bado inaonekana hawajapata stori nzuri ya kutokea. Ningependa kujua mauaji yalifanyika wapi in relation to the Police station. Maana tunaweza kuuziwa mbuzi kwenye gunia hivi.
 
Pelekeni upuuzi wenu huko, kumbukeni damu zisizo na hatia mnazomwaga ni laana kwa kizazi chenu chote,,Jitahidini kujisafisha ilihali mnajua yote mliyotenda mlielekezwa na wanasiasa, na siku mtakapokufa mkifika huko hao mliowauwa ndo mtawakuta mlangoni wanaandikisha majina ya wanaoingia sijui mtawaambiaje
 
Hawa jamaa wameishiwa, Kwa wale wenye kumbukumbu nzuri watakubaliana nami kuwa utetezi huu wa kuvamia vituo ni copy and paste ya utetezi wa mauaji ya 2001 Unguja na Pemba. Walikuja na utetezi kama huu na wakapata public sympathy. This time wamekosea hesabu kikombe hiki hakiwezi kuwaepuka wauaji hawa na wakiendelea kutoa utetezi wa uongo wanazidi kuwaweka wenzao front liners ambao wanaishi nyumba za kupanga mitaani kwenye hatari kubwa kwani Public anger inazidi kupanda badala ya kushuka
 
Me mwenyewe nimemsikia Chagonja akiropoka.....amekataa kuulizwa maswali na waandishi wa habari,alipomaliza kuongea akakimbia nje ya ukumbi. Alijua waandishi wangepiga za uso.....Waandishi wa habari wa Tanzania mnahitaji pongezi (baadhi yenu). Mmefanya kazi nzuri kwenye uchaguzi na sasa bado mnaendelea kuwakilisha.

In rules of natural justice, no one can be a judge on his own cause (nemo iudex in causa sua).

Hawa polisi hawajui sheria. Katika shauri la Arusha wao ni watuhumiwa iweje wao wawe wasemaje? Wasubiri Judicial Commission of Inquiry.
 
Back
Top Bottom