Msimamo wa Jeshi la Polisi kufuatia mauaji ya Raia Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msimamo wa Jeshi la Polisi kufuatia mauaji ya Raia Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MsandoAlberto, Jan 10, 2011.

 1. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  IGP Mwema amepotoka (amepotoshwa) na kukosea kwenye mambo mawili;

  1. Mamlaka ya kusitisha maandamano au mkusanyiko wa watu yapo kwa OCD na sio IGP. Hoja ni kwamba ameingilia mamlaka ya OCD.

  2. Taarifa za kipolisi kama zitatolewa kwa vyombo vya habari lazima ziandikwe (typed or written) na kama ni verbal (za mdomo) ni lazima ziandikwe mara baada ya kutolewa. Hoja ni kwamba IGP ametoa taarifa bila kufuata utaratibu hivyo maandamano ya CDM yalikuwa halali hayakufutwa kisheria.

  Ushahidi wa hayo ni kama ifuatavyo (nukuu kutoka kwenye Police General Order as revised in 2006);

  A) Taarifa kupitia vyombo vya habari:

  Police General Order No. 294

  1. The following officers ONLY are authorized to release information on police matters to the Press:-

  a) The Inspector General - on all matters affecting Force policy and security.

  b) Director of Criminal Investigation - Crime reports, wanted person notices and appeals to the public in connection with crime, accidents etc

  c) Chief of Public relations Police Headquarters - Routine Press notices affecting the whole Force.

  d) Regional Commanders - Routine Press Notices affecting particular Region.

  2. All Press and radio releases shall normally be typed or written. Verbal releases are only permissible in emergency and shall always be confirmed, in writing, at the earliest opportunity.

  B) Maandamano na Mikusanyiko

  Police General Order No. 403

  1. (a) Any person who is desirous of convening, collecting, forming or organising any assembly or procession in any public place shall, not less than forty eight hours before the time when the assembly or procession is scheduled to take place submit a written notification of his impending assembly or procession to the police officer in charge of the area.....

  b) where a person submits a notification in accordance with the preceding paragraph, he may proceed to convene, collect, form, or organise the assembly or procession in question as scheduled unless and until he receives an order from the Police Officer in charge of the area directing that the assembly or procession shall not be held as notified.

  c) A Police Officer to whom notification has been submitted pursuant to paragraph 1)(a) shall not give a stop order in relation to the notification unless he is satisfied that the assembly or procession is likely to cause breach of peace or to prejudice the public safety or maintenance of public order or to be for any unlawful purpose

  IGP Mwema, amekosea na amekosea sana kwa sababu ni kutokana na makosa yake maisha ya watu watatu wasio na hatia yamekatishwa. Makosa yake yamesabisha majeraha makubwa kwa raia na pia yameumiza mioyo ya watanzania wote wanaoipenda nchi yao!! Ni lazima ajaiuzulu kama kweli ni kiongozi mwenye busara na hekima!

  Atueleze Policer Officer incharge wa Arusha alimpa nani 'stop order'? yeye anatoa wapi mamlaka ya kutoa 'stop order' kupitia tv na radio ambayo haijaandikwa??

  Ni kwa nini Police walitembea na wananchi kutokea Philips mpaka tank la maji (zaidi ya kilometre 3) ndipo police wakaanza kuwapiga mabomu? Au walitaka wapite maeneo ambayo kuna wazungu (Mt. Meru Hotel na AICC) na kuanza kupiga raia maeneo ya Kaloleni wanapoishi walalahoi??

  Kwa nini Police hawakutangazia wananchi pale Mt. Meru Hotel kwamba wasambae mkusanyiko na maandamano yamezuiwa? Je ilitolewa 'dispersal order' yoyote kuwatahadharisha wananchi lakini wakakaidi? Hakuna hata gari moja la police lilitotangaza kwa vipaza sauti wananchi watawanyike badala yake waliwasindikiza wananchi mpaka tank la maji na kuwa sambaza kwa risasi na mabomu!!

  Ni kwa nini pikipiki na magari ya polisi yalikuwa yanawakimbiza wananchi na kuendelea kupiga mabomu uwanjani ambapo mkutano ulikuwa umeruhusiwa? Uwanjani yalipigwa mabomu katikati zaidi ya 30 kabla ya mkutano kuanza na gari la maji ya kuwasha lilipita likimwaga maji. Je hiyo ndiyo dispersal order kwa mujibu wa taratibu za jeshi la polisi??

  Kutokana na vitendo vya kinyama vilivyofanyika ni lazima wahusika wachukuliwe hatua!! Ndugu mwana JF piga kura yako ya kumtaka IGP na Maofisa wake wajiuzulu na sheria ichukue mkondo wake!!!

  Ni vyema tukasaini petition ya kumtaka ajiuzulu kwa lazima kama busara yake itamtuma vinginevyo!!
   
 2. msafiri.razaro

  msafiri.razaro JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 616
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Tunasaini wapi mkuu?
   
 3. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kutokana na mapendekezo ya wana-JF utaratibu wa kusaini utaandaliwa na petition itazungushwa kila mwenye moyo asaini. Petition itakuwa kukusanya saini zaidi la elfu kumi!!!! Ila ni vyema tukapata mawazo ya wengine kiongozi!
   
 4. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #4
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  hata suala la pingu za Jerry Muro aliomba akapekue...na hakujibu kamwe!
   
 5. K

  Kisaa kyafo Member

  #5
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama una evidence na unasema toka hadharani utoe hoja zako,na nadhani pia unaweza pata wenzako wa kukuunga mkono,sio unajificha ndo unasema,nafkiri umenipata.
   
 6. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #6
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Kama huyu IGP anasoma humu AMA Kama kuna wapambe wake wanaomsomea na kumtafsiria yanayiandikwa humu age bass na akanushe hivo vipengere ulivunukuu labda waseme kwamba Neno at earierist ni ambiguous ingawaje kazi ya kutafsiri si Yao ni ya akina pilato! Wahusika wote waliohusika ktk jambi hili la Arusha wajipime jama mwenzao Lowasa ba lowasa atajiwekea mazingira mazuri kisiasa Kama atatamka hadharani kuwataka wahusika wajipime Kama alivyojipima! Come lowasa say something!!!
   
 7. msafiri.razaro

  msafiri.razaro JF-Expert Member

  #7
  Jan 10, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 616
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Ninaingoja Kwa hamu, huyi IGP hafai kabisa. Ajiuzulu.
   
 8. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #8
  Jan 10, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 326
  Trophy Points: 180
  Jambo la kushangaza kabisa stop order ilyotolewa aliyoisema IGP alipoongea na wanahabari ilisainiwa mwaka jana januari 4 2010 yenye kumb. No. ARR/B.5/I/VOL.VIII/24. Kunahaja ya kulifungulia jeshi la polisi mashitaka ya uaji wa kukusudia kwani wao ndo walivunja sheria
   
 9. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #9
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mhe Kikwete, Mizengo Pinda, George Mkuchika, Shamsi Vuai Nahodha, Said Mwema, Adengenya wajiuzulu kushindwa kwao kuzuia mauaji ya kikatili Arusha wakati walikua wa uwezo wa kufanya hivyo kama ambavyo sheria zetu zinavyoelekeza.
   
 10. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #10
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni umbumbumbu wa Saidi Mwema kama IGP umesababisha vifo Arusha. Ajiuzulu. Kama haoni kwamba amesababisha hivi vifo, basi Rais atengue uteuzi wake, yaani amfukuze.
   
 11. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #11
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Ajiuzulu sasa no time to waste
   
 12. Masaningala

  Masaningala JF-Expert Member

  #12
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 539
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Ajiuzulu mara moja.
   
 13. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #13
  Jan 10, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Peleka mahakamani vielelzo ili ahukumiwe! JF haina meno, imeshindwa hata kumuondowa JK madarakani kwa kura!
   
 14. Ngoreme

  Ngoreme Senior Member

  #14
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  “Jeshi la Polisi linatakiwa kufanya kazi kwa mipaka ili kuhakikisha kuwa linadumisha amani nchini,” alisema Membe akielezea kuwa ni maoni yake binafsi kuhusiana na tukio hilo linaloelekea kuliwekea doa Tanzania ambayo inajulikana kuwa ni kisiwa cha amani.

  BINAFSI IGP ACHUKULIWE HATUA ZA KINIDHAMU KAMA KILA MTU AMEONA HIVYO MSEMAJI WA TAIFA NJE YA MIPAKA KASEMA NA NDIVYO ILIVYO

   
 15. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #15
  Jan 13, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wasema hawakukosea, Chadema ndo walikaidi amri halali ya serikali iliyoko madarakani

  source BBC jioni hii
   
 16. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #16
  Jan 13, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Source?
   
 17. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #17
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  wanaumwa bado. kwani Andenfenya ndio serikali? Ngoja tuone matokeo. Membe kashaawambia ukweli wao
   
 18. czar

  czar JF-Expert Member

  #18
  Jan 13, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 340
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo Mh Membe alikosea kwenye maoni yake sio? Mbona siku ya maziko hakukuwa na fujo? Polisi kimavi chenu hiko, Igp na Rpc wa Atown wajibikeni.
   
 19. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #19
  Jan 13, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Me mwenyewe nimemsikia Chagonja akiropoka.....amekataa kuulizwa maswali na waandishi wa habari,alipomaliza kuongea akakimbia nje ya ukumbi. Alijua waandishi wangepiga za uso.....Waandishi wa habari wa Tanzania mnahitaji pongezi (baadhi yenu). Mmefanya kazi nzuri kwenye uchaguzi na sasa bado mnaendelea kuwakilisha.
   
 20. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #20
  Jan 13, 2011
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Pia huyo msemaji polisi, anasema Hawatovumilia endapo , raisi wa nchi atadhalilishwa, na kutukanwa
  souce BBC swahili
   
Loading...