mtotowamjini
JF-Expert Member
- Apr 23, 2012
- 4,526
- 1,169
maskini NAPE.... atakua anatoa statement kila mwezi between now na 2015 maana CDM watakua wanawalalamikia CCM kila siku
[h=3]MSIMAMO WA CCM KUHUSU TUHUMA ZA KUHUSIKA NA MAUAJI YA WANACHADEMA[/h]
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Hivi karibuni chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kilielezea kile ilichoeleza kuwa ni kutishwa na wimbi la mauaji yanayotishia amani ya nchi kikidai kuwa jumla ya wanachama wake 15 wameuawa katika wilaya ya Igunga peke yake.
Madai hayo ya CHADEMA, pamoja na wanachama wengine na mashabiki wao, yalitolewa na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, ambaye alidai kuwa mauaji hayo yana mkono wa serikali ya CCM, ambayo kwa madai yao imeona wazi kuwa upepo wa kisiasa umekiendea vibaya na sasa kinataka kujiimarisha katika utawala kwa kuua watu wanaoipinga.
Akifungua kikao cha Baraza Kuu la chama hicho jijini Dar es Salaam Aprili 29 mwaku huu mwenyekiti huyo alifafanua kuwa mbali na kuuawa kwa watu wanne kwa pamoja na juzi kifo cha mwenyekiti wao wa tawi huko Arumeru mkoani Arusha, jumla ya wanachama wake 15 wameuawa katika wilaya ya Igunga peke yake tangu kumalizika kwa uchaguzi mdogo wa jimbo hilo mwaka jana.
Mbowe katika maelezo yake alijaribu katika maeneo kadhaa kuihusisha CCM na au serikali yake katika matukio kadhaa yaliyowakabili baadhi ya wanachama na viongozi wa Chadema katika maeneo mbalimbali nchini likiwemo lile la Mbunge Highness Kiwia ambaye Suala lake bado Lipo mikononi mwa vyombo Vya dola likishughulikiwa.
Katika sehemu kubwa ya maelezo ya Ndg. Mbowe amejitahidi kuonesha kuwa mauaji yote yaliyoikabili na yatakayokuwa yakiikabili Chadema kupitia wafuasi wake yanafanyika kisiasa, Jambo ambalo ni la uzushi, kwani Halina ushahidi wa kisheria hata kimazingira, wa Moja kwa Moja unaoondosha ujinai au makosa hayo, na kuwa ni makosa yanayolenga muktadha wa kisiasa.
Huku akitaka kuuaminisha umma kuwa huo ndio ukweli, Ndg. Mbowe amesisitiza kuwa hilo lime kuwa likitekelezwa na CCM kwa lengo la kuwatisha wananchi kujiunga na chama hicho hoja ambayo haina msingi wowote wa kiutafiti.
Hivyo CCM kwa kutambua kuwa Suala la mauaji linabeba Kosa la jinai, na kwa kuwa Ndg. Mbowe ameshutumu Moja kwa Moja CCM na serikali yake kuihusisha na mauaji hayo, ni vema sasa nasi tukatoa msimamo wetu dhidi ya tuhuma, hiyo.
Kwanza, si busara hata kidogo kuihusisha CCM katika matukio hayo, kwani uchunguzi unaofanywa na vyombo vya dola umeshindwa mpaka sasa kuhusisha matukio hayo na siasa, badala ya kuyahusisha na makosa ya jinai ambayo hufanywa na watu kwa malengo tofauti na yale ambayo Ndg. Mbowe anataka kuwaaminisha watu.
Pili, CCM haijawai, haiwezi, na haitakuja fanya jambo lolote lenye lengo la kuvuruga Amani na Usalama wenye utulivu ndani ya taifa letu, hivyo uzushi na usingiziaji uliofanywa na Mtu Kama Ndg. Mbowe, si vema kuuacha kimya, badala yake nimetumia wasaa Huu muhimu Kujibu, na kutoa ufafanuzi ili Kuupa umma wa watanzania habari sahihi.
Ni aibu kwa Chama kama Chadema kujitahidi kwa nguvu zote kujaribu kuficha ukweli wa mauaji yanayotoa roho za watanzania wenzetu kwa kuyapa sura ya kisiasa. Hizi ni juhudi za makusudi za kutaka kuficha ukweli wa kinachotokea.
Ni aibu kwa chama kama Chadema kujaribu kutumia mauaji mabaya kama haya kutafuta mtaji wa kisiasa. Huku ni kuonyesha jinsi gani wamefilisika kisiasa mpaka wanafikia mahali pa kuamini kuwa wanaweza kutumia chochote kama mtaji wa kisiasa, vikiwemo vifo vya watanzania wenzetu. Huku si kufilisika tu ila kwakweli ni unyama unaotakiwa kulaaniwa na kila muungwana.
Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
Ideology and Publicity Secretary
Nape: Mlijipongeza wakati mnafanya gizani sasa mambo yanaanza kuwa peupe mnaanza kujitokeza kujibu, lazima waliopanga watajulikana tu. Jueni kwamba damu ya mtu huwa haipotei itawaandama wote popote mtakapokwenda, iwe nyumbani, ofisini hata kwenye vikao vyenu lazima hili litawasumbua tu, uwe hukuhusika moja kwa moja ila kile kitendo cha kupanga na au ku-facilitate ni sawa na kuhusika.
Sisi tuna M4C nyie mna M4K.
taratibu unatupeleka siko lete hoja kwa hoja
Hii Press Release imetolewa na CCM au imetolewa na serikali ya CCM?
Nape anasema hivi: ...Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, ambaye alidai kuwa mauaji hayo yana mkono wa serikali ya CCM..."
Sasa kama madai yaliekezwa kwa serikali ya CCM, Nape anajibu kama nani? Yeye ni nani serikalini?
Bado Nape anaendelea kusema "...si busara hata kidogo kuihusisha CCM katika matukio hayo, kwani uchunguzi unaofanywa na vyombo vya dola umeshindwa mpaka sasa kuhusisha matukio hayo na siasa..."
Nape anafahamu nini kuhusu haya mauji? ana report ya uchunguzi toka Jeshi la Polisi tayari? Kama anayo report kwa nini asiweke wazi ili wanafamilia waliofiwa wajue ukweli ni upi?
Hii Press Release ni mbaya sana.
Nape, is the most hopeless.
Wamajamii, japo siwezi kumtaja jina kwa sababu zinazoeleweka, lakini hivi karibuni nilikuwa nikiongea na afisa mkubwa wa Jeshi la polisi ambaye amekuwa akishughulikia masuala ya mashambulio dhidi ya viongozi/wapenzi wa CHADEMA, kwa maneno yake alisema, 'CHADEMA wana haki ya kulilaumu jeshi la polisi lakini na sisi hatuna la kufanya maana mashambulio haya yanafanywa na wafuasi wa CCM kwa maelekezo'; nilimwuliza kama yanafanywa kwa maelekezo ya viongozi wa chini wa CCM, naye aliniambia kuwa ingekuwa rahisi kushughulikia kama yangekuwa yanafanywa kwa maelekezo ya viongozi wa ngazi za chini lakini haya ni maelekezo ya viongozi wakubwa wa CCM. Na mwisho alisema kuwa jeshi la polisi halifurahishwi, haliungi mkono, halipendi lakini kwa mfumo wa sasa ni vigumu sana kutenda haki bila ya wewe polisi kudhibitiwa. Kwa hiyo ni vema watu wakajua kuwa mashambulizi haya yote yanafanywa na CCM. Na ndiyo maana hata Nape, katika huo waraka wake ameshindwa kujitetea, hajatoa utetezi wowote zaidi ya kumshambulia kwa maneno Mh. Mbowe. Wapenda mabadiliko wote, mnapoendesha harakati zenu, jihadharini na CCM maana ipo tayari hata kutoa roho za watu kwaajili ya kutetea uwepo wake.
Kuna uwezekano mkubwa sana kuwa chadema wanauana wenyewe kwa wenyewe ili kutafuta mtaji wa kisiasa kwa njia chafu. Wachagga wanajulikana kwa kutoana kafara hata kwa wizi tu. Lakini kuna siku watabainika.
Chadema ni chama hatari sana kwa usalama wa Tanzania.
Naishauri Serikali ikifungie hiki chama kwani kimeshakuwa na mtaji wa ukabila, ukanda na udini.