Msimamo wa CCM kuhusu tuhuma za kuhusika na mauaji ya wana-CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msimamo wa CCM kuhusu tuhuma za kuhusika na mauaji ya wana-CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAMA POROJO, May 8, 2012.

 1. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  [h=3]MSIMAMO WA CCM KUHUSU TUHUMA ZA KUHUSIKA NA MAUAJI YA WANACHADEMA[/h]
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


  Hivi karibuni chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kilielezea kile ilichoeleza kuwa ni kutishwa na wimbi la mauaji yanayotishia amani ya nchi kikidai kuwa jumla ya wanachama wake 15 wameuawa katika wilaya ya Igunga peke yake.


  Madai hayo ya CHADEMA, pamoja na wanachama wengine na mashabiki wao, yalitolewa na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, ambaye alidai kuwa mauaji hayo yana mkono wa serikali ya CCM, ambayo kwa madai yao imeona wazi kuwa upepo wa kisiasa umekiendea vibaya na sasa kinataka kujiimarisha katika utawala kwa kuua watu wanaoipinga.


  Akifungua kikao cha Baraza Kuu la chama hicho jijini Dar es Salaam Aprili 29 mwaku huu mwenyekiti huyo alifafanua kuwa mbali na kuuawa kwa watu wanne kwa pamoja na juzi kifo cha mwenyekiti wao wa tawi huko Arumeru mkoani Arusha, jumla ya wanachama wake 15 wameuawa katika wilaya ya Igunga peke yake tangu kumalizika kwa uchaguzi mdogo wa jimbo hilo mwaka jana.


  Mbowe katika maelezo yake alijaribu katika maeneo kadhaa kuihusisha CCM na au serikali yake katika matukio kadhaa yaliyowakabili baadhi ya wanachama na viongozi wa Chadema katika maeneo mbalimbali nchini likiwemo lile la Mbunge Highness Kiwia ambaye Suala lake bado Lipo mikononi mwa vyombo Vya dola likishughulikiwa.


  Katika sehemu kubwa ya maelezo ya Ndg. Mbowe amejitahidi kuonesha kuwa mauaji yote yaliyoikabili na yatakayokuwa yakiikabili Chadema kupitia wafuasi wake yanafanyika kisiasa, Jambo ambalo ni la uzushi, kwani Halina ushahidi wa kisheria hata kimazingira, wa Moja kwa Moja unaoondosha ujinai au makosa hayo, na kuwa ni makosa yanayolenga muktadha wa kisiasa.


  Huku akitaka kuuaminisha umma kuwa huo ndio ukweli, Ndg. Mbowe amesisitiza kuwa hilo lime kuwa likitekelezwa na CCM kwa lengo la kuwatisha wananchi kujiunga na chama hicho hoja ambayo haina msingi wowote wa kiutafiti.


  Hivyo CCM kwa kutambua kuwa Suala la mauaji linabeba Kosa la jinai, na kwa kuwa Ndg. Mbowe ameshutumu Moja kwa Moja CCM na serikali yake kuihusisha na mauaji hayo, ni vema sasa nasi tukatoa msimamo wetu dhidi ya tuhuma, hiyo.


  Kwanza, si busara hata kidogo kuihusisha CCM katika matukio hayo, kwani uchunguzi unaofanywa na vyombo vya dola umeshindwa mpaka sasa kuhusisha matukio hayo na siasa, badala ya kuyahusisha na makosa ya jinai ambayo hufanywa na watu kwa malengo tofauti na yale ambayo Ndg. Mbowe anataka kuwaaminisha watu.


  Pili, CCM haijawai, haiwezi, na haitakuja fanya jambo lolote lenye lengo la kuvuruga Amani na Usalama wenye utulivu ndani ya taifa letu, hivyo uzushi na usingiziaji uliofanywa na Mtu Kama Ndg. Mbowe, si vema kuuacha kimya, badala yake nimetumia wasaa Huu muhimu Kujibu, na kutoa ufafanuzi ili Kuupa umma wa watanzania habari sahihi.


  Ni aibu kwa Chama kama Chadema kujitahidi kwa nguvu zote kujaribu kuficha ukweli wa mauaji yanayotoa roho za watanzania wenzetu kwa kuyapa sura ya kisiasa. Hizi ni juhudi za makusudi za kutaka kuficha ukweli wa kinachotokea.


  Ni aibu kwa chama kama Chadema kujaribu kutumia mauaji mabaya kama haya kutafuta mtaji wa kisiasa. Huku ni kuonyesha jinsi gani wamefilisika kisiasa mpaka wanafikia mahali pa kuamini kuwa wanaweza kutumia chochote kama mtaji wa kisiasa, vikiwemo vifo vya watanzania wenzetu. Huku si kufilisika tu ila kwakweli ni unyama unaotakiwa kulaaniwa na kila muungwana.


  Nape Moses Nnauye
  Chama Cha Mapinduzi
  Ideology and Publicity Secretary

   
 2. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,791
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Una beyond repair mental disorders, majibu mengine heri uyapime kwa mkemia kabla ya kuyaweka hadharani
   
 3. B

  Bhavick JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 314
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kaacha kujitetea,kaanza kumshambulia Mbowe,kweli Nape hamnazo!
   
 4. mtalae72

  mtalae72 Member

  #4
  May 8, 2012
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hivi hilo neno "ideology and PUblicity Secretary" Halina tafsiri ya kiswahili? Huyu bwana anatoa taarifa kwa umma kwa lugha ya kiswahili tangu mwanzo hadi mwisho lakini anashindwa kutafsiri nafasi yake katika chama, tumuelwe vipi? Huku ndiko kushindwa kazi au??!!
   
 5. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,760
  Trophy Points: 280
  Nape is a mugger dog who bark at the flying birds.
   
 6. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Si muda mrefu hawa tutawazika wazima wazima! It is just a matter of time! CCM siyo Mungu hata itawale milele. Vyama vyote vya siasa Africa vilivyo-take over baada ya wakoloni mwishoni mwa miaka ya 1950 na mwanzoni mwa miaka ya 1960 kusini mwa Sahara imebaki CCM tu. Very soon tutawazika wazima wazima. VERY VERY SOON!
   
 7. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  taratibu unatupeleka siko lete hoja kwa hoja
   
 8. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,760
  Trophy Points: 280
  wewe ndo Nape???
   
 9. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,588
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  IGUNGA kwenye Hoteli walipanga Chadema saa 8 usiku walifuata nini na madumu ya petroli kama hawana nia hiyo?
   
 10. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #10
  May 8, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Kwa mara nyingine tena,Nape anaonyesha asivyo na hoja
  CHADEMA haijasema kuwa mauaji si jinai,mauaji ni Jinai na ushahidi wa mazingira unaonyesha kuwepo kwa mkono wa ccm na dola yake(serikali)na hata mara moja CHADEMA haitumii mauaji haya kama mtaji wa kisiasa,bali lazima penye ukweli tuseme wazi,ccm inahusika.
   
 11. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #11
  May 8, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 829
  Trophy Points: 280
  Tuambieni basi nani anasababisha yote haya?? Ina maana wananchi wameuiliwa tangu uchaguzi wa Igunga na mpaka leo chombo husika hakijakamata wahusika???

  Nape,Nani aliwashambulia wabunge wa CDM Mwanza??Hivi wamekamatwa??

  Nadhani hii issue haihitaji majibu mepesi kiasi hiki!!!!
   
 12. papason

  papason JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Binafsi nalaumu sana ukimwa na upole wa sisi wanachama, wafuasi, viongozi wa CDM, wenzetu wamagamba ustamilivu wa kisiasa umewashinda, baada ya kuona tunawashinda kwa hoja kwenye kila kona sasa wanaanza kutu uwa mmoja mmoja, na sisi tunaishia kulalamika tuu tukisubiri polisisiem watusaidie wakti na sisi nguvu na uwezo wa kijitete tunao, sijui tunangoja nini wakati siku zote tunajua kabisa anayekuanza mmalize!
   
 13. F

  FJM JF-Expert Member

  #13
  May 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hii Press Release imetolewa na CCM au imetolewa na serikali ya CCM?

  Nape anasema hivi: ...Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, ambaye alidai kuwa mauaji hayo yana mkono wa serikali ya CCM..."

  Sasa kama madai yaliekezwa kwa serikali ya CCM, Nape anajibu kama nani? Yeye ni nani serikalini?

  Bado Nape anaendelea kusema "...si busara hata kidogo kuihusisha CCM katika matukio hayo, kwani uchunguzi unaofanywa na vyombo vya dola umeshindwa mpaka sasa kuhusisha matukio hayo na siasa..."

  Nape anafahamu nini kuhusu haya mauji? ana report ya uchunguzi toka Jeshi la Polisi tayari? Kama anayo report kwa nini asiweke wazi ili wanafamilia waliofiwa wajue ukweli ni upi?

  Hii Press Release ni mbaya sana.
   
 14. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #14
  May 8, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  walikuja kuchoma moto magari ya CHADEMA,na kuua wanachadema,tena walikuwa Wabunge wa ccm,nilikuwepo,nilishuhudia kwa macho yangu.
  Arumeru mashariki viongozi wa ccm walimteka na kumuhasi mwenyekiti wa Chadema wa Tawi,Arusha viongozi wa ccm tena wa kitaifa walimteka kada wa CHADEMA kwa zaidi ya siku nne,wakamwachia baada ya kugundulika kuwa ni wao_Orodha ni ndefuuuuuuuuuuu
   
 15. I

  IWILL JF-Expert Member

  #15
  May 8, 2012
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 311
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  hivi huyu kibaraka hajui tunajua njama za CCM na kundi la uharamia usalama wa taifa wanavyo chukua roho za watu wasio na hatia? kikwete ndio ajibu hoja ya mwenyekiti mbowe badala ya kiongozi wa CCK kutoa *****! na kama mauaji mbona imekuwa siku nyingi hao watu wa Igunga kuuwawa. na leo aje na tamko! au baada ya kuona wadanganyika na na akina Mapuli wanaamka kwa kazi kwenye usingizi uliodhaniwa ni wa fofofo! too late....jini limeshatoka kwenye chupa. na kiongozi wa kuwapa ndozi ingine ya usingizi sioni....kikwete is meat head ndio anaunda kikosi cha kuua watanzania akidhani atavuruga harakati.
   
 16. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #16
  May 8, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Yani we Nape ndo umeonyesha wazi kabisa jinsi ambavyo CCM haina huruma na roho za watu. Ningetegemea katika hii kauli yako uanze kwa kuonyesha masikitiko yako na wanachama wenzio wa CCM juu ya hizo roho zilizopotea bila hatia. Kinyume chake wewe umeenda kumshambulia tuu Mbowe...kweli ndugu umekosa busara na utu hata chembe! Shame on you na hao wanaokutegemea uwe msemaji wao...
   
 17. P

  PETERSON Member

  #17
  May 8, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NAPE kwisha kazi! Ni kelele za Mfa maji tu. CDM haiui kimwili mtu yeyote, inaua DHANA,MTAZAMO,FIKRA NA MAZOEA yote ya KIFISADI.Na hatimaye CCM itakufa.
   
 18. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #18
  May 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,588
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  Kamanda Nanyaro mi nadhani ifike mahali muwashitaki mahakamani, tushuhudie jinsi mahakama itakavyowasafisha kuwa hawana hatia hilo litaongeza hasira za wananchi kwa tunafahamu kila kitu kuwa ccma ndiyo wanaovuruga amani ya nchi aidha moja kwa moja au kwa kutumia polisi hilo kila mtanzania analijua. Nape asijitetee hapa shame on him.
   
 19. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #19
  May 8, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kumbe Nape ndio mama porojo!!!! sasa na hayo makalio ndio kusema anafikili kwa kutumia naniii au masaburi!!!
   
 20. F

  FJM JF-Expert Member

  #20
  May 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nimemuona Nape akiongea muda si mrefu TBC1 -Usiku wa habari na moja ya mambo aliyosema ni kutaka CHADEMA iombe radhi umma kutokana na kauli ya Nassari. Nape ametumia maneno 'CHADEMA wanataka kuigawa nchi vipande vipande'.

  Maoni yangu: Nassari ameteleza na sasa polisi wanamhoji, wakati huo huo mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ameshasema wazi wazi kuwa huo sio msimamo wa chama.

  CCM na hasa Nape waone busara ya kutojiingiza kwenye hii issue. Inaweza kugeuka vibaya sana na kwa vyovyote vile itakuwa kwa CCM. Mt wa Lumumba wangekuwa na akili timamu wangekaa kimya waiache polisi ihangaike na Nassari, lakini maadam sasa Nape ameonesha interest ya ku-score political points hii issue itaanza kuchukua sura tofauti.
   
Loading...