Msimamo: Napinga Mkapa kupongezwa kwa kuandika kitabu kinachoeleza makandokando yake

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,657
218,145
Laiti kama Mzee huyu angeandika kitabu cha kufundishia watoto shuleni cha alphabet kama 'a e i o u' au cha hesabu ama kiswahili sanifu basi nisingetia neno lolote, lakini kwa kitabu hiki alichoandika sitathubutu kumpongeza hata chembe.

Benjamini Mkapa mtu aliyeingia madarakani baada ya kuapa kuilinda na kuitetea Katiba ya Tanzania, huku akiwa na akili timamu hawezi kupongezwa na yeyote mwenye akili timamu kwa kuandika kitabu kinachoelezea namna alivyofanya madudu yake ikiwa ni pamoja na mauaji ya wapemba akiwa madarakani jambo ambalo ni kinyume cha Katiba aliyoapa kuilinda, nani aliyekuwa hajui kuhusu yeye kufanya biashara Ikulu, nani hakufahamu kuhusu wizi wa kienyeji wa EPA uliokuja kunufaisha chama chake?

Alipokuwa madarakani mbona hatukumsikia akipigia chapuo Tume huru ya uchaguzi, why now? Amelenga kumdanganya nani na kwanini, ni hofu ya uzee?

Mtu ambaye miaka michache iliyopita aliwaita wapinzani wapumbavu leo amepata wapi huruma ya kuomba washirikishwe kwenye michakato ya nchi?

Ikiwa kama lengo la Mkapa lilikuwa ni kutubu basi ni vema angekutumia njia ya madhabauni lakini si ghiliba hii ya kitabu, ikiwa kama tutamsifia huyu basi bila shaka na hawa wengine watatumia njia hii hii kuja kutung'ong'a ili nao wahurumiwe.

Siungi mkono kitabu cha Mkapa na makandokando yaliyo ndani yake na naomba msimamo wangu uheshimiwe.

Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko.
 
Mimi sitalishangaa bandiko hili maana baadhi ya Watanzania wenzetu wao kazi ni pinga pinga tuu kila kitu, kiwe kizuri, kiwe kibaya wao watapinga tuu.

Watu wa aina hii, niliwazungumza hapa

P
 
Kwakuwa amekiri mwenye kuuua raia wasio na hatia pemba(Uhalifu wa kivita,mauaji ya halaiki,mauaji ya kimbali etc) na kupiga fedha za EPA wengine wapo jela kina farijala hussein na rajabu maranda(sina uhakika kama washatoka),BWM amequalify kabisa kubuluzwa The Hague kwa "Ocampo" wa sasa!!
 
Labda kunahitajika upembuzi yakinifu kujua hasara na faida ya hicho kitabu ktk nchi!!.. Hii inatoa alert kwa wenye akili,Upungufu wa katiba yetu ktk kuwabana viongozi pia inaonyesha udhaifu wa idara nyeti kwa kumuacha kiongozi kufanya madudu! Tujitafakari..
 
Tunajua akili zenu zilivyo finyu huwa mnasahau mambo kwa muda jiulize ilikuwaje kuhusu lowassa!
 
Siungi mkono kitabu cha Mkapa na makandokando yaliyo ndani yake na naomba msimamo wangu uheshimiwe.
Utapata kisukari kijana,si kila jambo unalopinga unafungua thread
Wewe anakujua nani mpaka malalamiko yalete impact?

Kitabu kimeisha baada ya siku mbili tu
Nakushauri tunga kitabu chako kumbamiza mkapa,badala ya kulia lia kama mtoto.
 
Mimi sitalishangaa bandiko hili maana baadhi ya Watanzania wenzetu wao kazi ni pinga pinga tuu kila kitu, kiwe kizuri, kiwe kibaya wao watapinga tuu.

Watu wa aina hii, niliwazungumza hapa

P
Never expect the whole universe to be on your side kaka, do what you think it’s right and ethical, the moral will judge
you.
 
Mimi sitalishangaa bandiko hili maana baadhi ya Watanzania wenzetu wao kazi ni pinga pinga tuu kila kitu, kiwe kizuri, kiwe kibaya wao watapinga tuu.

Watu wa aina hii, niliwazungumza hapa

P
Mimi sitoshanga comment yako manake unasifuu tu awamu hii, au wale wasiojulikana wameshakupa salamu zao?


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Back
Top Bottom