Kwa wale wanaoujua mji wa Moshi wataweza kufuatilia kirahisi sana namna ambavyo uamuzi huu uluvyofanyika bila kufuata ukweli wa kisheria wala kimazingira.
Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi Mgombea Mwenza wa kiti cha urais kwa tiketi ya CCM Dr. Ghalib Bilal alikuwa awe mjini Moshi kesho tr. 18/10/2010. Badala yake amefika leo.
Baada ya CCM kujua kuwa Bilal atakuwepo Moshi leo walimwandikia barua Msimamizi wa uchaguzi wakimtaka ahamishe mkutano wa mgombea ubunge bw. Salakana kutoka katika kata ya Longuo B kwenda Pasua. Barua hiyo badala ya kusubiri ama kuitishiwa kikao cha pamoja cha makatibu wa vyama vinavyoshiriki uchaguzi mjini Moshi ilijibiwa na Msimamizi mwenyewe kwa kuwaruhusu kufanya mkutano wanavyoona wenyewe inawafaa.
Hatua iliyofuatia Msimamizi leo amepeleka barua kwa Katibu wa CHADEMA Manispaa ya Moshi akimweleza kusitisha mkutano wa chama hicho katika kata ya Bondeni ili kupisha mkutano wa Bilal ufanyike bila usumbufu wowote.
Akielezewa kuwa mikutano hiyo iko kata tofauti Msimamizi alijibu kuwa Mkutano uko katika barabara ambayo CCM watapita wakienda kwenye mkutano wao.
Nalo jeshi la polisi mkoani hapa baada ya kupewa nakala ya barua hiyo wamepeleka magari yaliyojaza askari wa FFU wenye silaha katika uwanja ambao CHADEMA wangefanyia mkutano. Kuanzia saa 7.30 mchana leo gari la maji ya kuwasha limekuwa likivinjari katika mitaa ya Moshi kama tishio kwa yeyote atakayethubutu kwenda katika mkutano wa CHADEMA.
Muda huu nimepata habari kuwa mkutano wa Bilal ambao ulikuwa upambwe kwa kurejeshwa kwa kadi za CHADEMA ambazo wamezitengeneza wenyewe umekuwa na mahudhurio mabaya sana.
Kwa kweli kwa msimamo, watu wa Moshi ni mwisho, t-shirt na kofia wanavaa, nauli wanapokea na pilau wanakula, ila siku ya siku, kurua wanapeleka Chadema.Moshi hawataki upumbavu.
Wana akili. Wana Elimu. Wana mali. HAWAITAKI CCM. This is the kind of people we want in Tanzania.
CCM inawauma kweli kuhusu Moshi!!
kwa wale wanaoujua mji wa moshi wataweza kufuatilia kirahisi sana namna ambavyo uamuzi huu uluvyofanyika bila kufuata ukweli wa kisheria wala kimazingira.
Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi mgombea mwenza wa kiti cha urais kwa tiketi ya ccm dr. Ghalib bilal alikuwa awe mjini moshi kesho tr. 18/10/2010. Badala yake amefika leo.
Baada ya ccm kujua kuwa bilal atakuwepo moshi leo walimwandikia barua msimamizi wa uchaguzi wakimtaka ahamishe mkutano wa mgombea ubunge bw. Salakana kutoka katika kata ya longuo b kwenda pasua. Barua hiyo badala ya kusubiri ama kuitishiwa kikao cha pamoja cha makatibu wa vyama vinavyoshiriki uchaguzi mjini moshi ilijibiwa na msimamizi mwenyewe kwa kuwaruhusu kufanya mkutano wanavyoona wenyewe inawafaa.
Hatua iliyofuatia msimamizi leo amepeleka barua kwa katibu wa chadema manispaa ya moshi akimweleza kusitisha mkutano wa chama hicho katika kata ya bondeni ili kupisha mkutano wa bilal ufanyike bila usumbufu wowote.
Akielezewa kuwa mikutano hiyo iko kata tofauti msimamizi alijibu kuwa mkutano uko katika barabara ambayo ccm watapita wakienda kwenye mkutano wao.
Nalo jeshi la polisi mkoani hapa baada ya kupewa nakala ya barua hiyo wamepeleka magari yaliyojaza askari wa ffu wenye silaha katika uwanja ambao chadema wangefanyia mkutano. Kuanzia saa 7.30 mchana leo gari la maji ya kuwasha limekuwa likivinjari katika mitaa ya moshi kama tishio kwa yeyote atakayethubutu kwenda katika mkutano wa chadema.
Muda huu nimepata habari kuwa mkutano wa bilal ambao ulikuwa upambwe kwa kurejeshwa kwa kadi za chadema ambazo wamezitengeneza wenyewe umekuwa na mahudhurio mabaya sana.
huyo aliyekuletea habari ni muongo kwani mimi nilikuwepo ktk mkutano huo na mahudhurio ya wananchi yalikuwa makubwa na yakutia moyo hivyo wacheni propaganda zenu!!!
kama moshi ni ngome ya chadema mbona manispaa ya moshi tangu uchaguzi wa 1995 mpaka leo inaongozwa na madiwani wengi ni ccm na meya ni ccm!! Yaani hapa kuna mbunge kweli wa chadema lakini hana nguvu yoyote ya kuchangia sera za chadema kwani wenye kura nyingi ni madiwani wa ccm!!!
Hii ishu ni kweli namlidhani kuwa mtapata wananchi wengi kwa kuwateka kisaikolojia watu wa chadema. pia inaonesha namna gani CCM haiheshimu utawala wa sheria kwa kunyonga demokrasia. mmelazimisha mkutano huo. Mmmekosa wasikilizaji mpaka wale wanachama feki wa kurejesha kadi mmekosa pia.
sasa ngome iko wapi?
Watu wengine hawatumii hata hekima. Yaani, watu unaenda kuwaomba kura, bado unawafanyia ubabe hao hao! Labda wameshakata tamaa ya kupata kura za wananchi wa kawaida sasa wanajaribu kulinda za wanaccm wenzao.
Wao waendelee tu lakini watavuna chuya