iPhone 5S
Senior Member
- Jun 6, 2014
- 158
- 102
Kwa manufaa ya jumuiya wana JF, na watanzania wengine,
Naomba mfahamu hili.
Ndugu Wilson Kabwe ambaye mnapiga kelele humu jamvini kuhusu kutumbuliwa kwake hajaanza ufisadi leo wala jana.
Huyu ni mtu anayepiga dili na watu wakubwa serikalini, na wao ndio humtumia kufanikisha ufisadi. Na mara anapofanikiwa kufisadi sehemu moja basi huamia sehem nyingine.
Usilolijua ni hili hapa:-
1. Bwana Wilson Kabwe ameoa katika familia moja....na aliyekuwa Waziri Mkuu....mzeee wa kulialia machozi...mzee wa kupinda na Zengo....na Pita. Kwa hiyo Wilson Kabwe na waziri mkuu alyestaafu ndugu Mizengo ni kama mtu na ndugu yake....na huyu PM mstaafu ndio aliyekuwa anambeba bwana kabwe muda wote.
2. Lakini alipofanya ufisadi mbeya...na kupigiwa kelele.....Mizengo pinda akaona isiwe taabu...akamuhamisha mtu wake na kumpeleka mwanza.
Kumbuka kuna kipindi fulani Mh.Sugu (mbunge wa mbeya mjini) alipiga sana kelele kuhusu ufisadi alioufanya Kabwe pale mbeya lakini akalindwa kwa kuhamishwa. na maojawapo ni ile ujenzi wa soko jipya baada ya kuungua moto ulikuwa chini ya kiwango na yeye ndie aliyekula 10% .
3. Akahamishiwa Mwanza...nako akaharibu....akamishiwa dar. Sasa kumbuka kuwa ilikuwa ngumu kumuwajibisha Wilson kabwe kwa sababu aliyekuwa anateua...ni waziri Mkuu.....ambaye by then alikuwa mtu waliye-oa katika familia moja, je unadhani atawajibishwa na nani?? Hata Mkwere alikuwa anajua Kabwe na pinda wameoa familia moja...unadhani rahisi kumuwajibisha?
NB: Usidhani Rais ndio anateua wakurugenzi wa manispaaa, miji au majiji,....Waziri mkuu ndio incharge....na ndipo hapo WILSON KABWE ALIPOBEBWA NA MUME MWENZIE ndugu PM ...a.k. mzee wa kulialia.
Hata sasa huo uchunguzi lazima utamsafisha tu kabwe kwa sababu ni mtu amabaye analindwa na system na ufisadi aliofanya yeye alikuwa ni daraja tu ila amekula na watu wakubwa wa serikali iliyopita.
Kama kuna mengine...karibu muongezee.
*****NYONGEZA TOKA KWA MDAU......BONGE BONGE......ASANTE...Kiongozi ******
Yadaiwa kila anakohamishiwa kikazi huzua fujo
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe
Bunge limetangaza 'kumshughulikia' Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe, ang'olewe kwa madai kuwa ni kiongozi mbovu na tatizo.
Kwa kuanzia, wabunge wamemshtakia' kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakidai amekuwa akizua fujo kila anakohamishiwa kikazi, huku akiendelea kulindwa na baadhi ya vigogo serikalini.
Hatua hiyo ilitangazwa na Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu, wakati akijibu mwongozo wa Spika ulioombwa na Mbunge wa Rombo (CHADEMA), Joseph Selasini, bungeni jana.
Mwongozo huo uliombwa kufuatia kauli ya Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli bungeni jana kwamba Kampuni ya Tanzania Building Works Limited inachunguzwa kwa kushindwa kutekeleza ujenzi wa soko la Mwanjelwa, mkoani Mbeya kwa wakati kinyume cha mkataba, uliofikiwa kati yake na Halmashauri ya Jiji la Mbeya na hivyo, kunyang'anywa kazi hiyo.
Katika ombi lake, Selasini alihoji iwapo kampuni hiyo itachunguzwa, kwanini isichunguzwe sambamba na Kabwe kwa madai kwamba mkurugenzi huyo ameonyesha kila anapohama, huhama nayo na kuipatia kazi kwenye maeneo ambayo anapewa.
Akijibu, Zungu ambaye pia ni Mbunge wa Ilala Jiji la Dar es Salaam, alisema yeye akiwa ni sehemu ya watu wenye maslahi na suala linalosemwa na Selasini atailaumu serikali.
"Serikali bado mnazembea viongozi wabovu, mnawahamisha kutoka sehemu moja kuwapeleka sehemu nyingine. Huyu mtu (Kabwe) ni tatizo kubwa sana. Na siyo tatizo Dar es Salaam, amefanya tatizo Mwanza. Chama Cha Mapinduzi kimekosa uongozi Mwanza sababu ya huyu mkurugenzi," alisema Zungu.
Aliongeza: "Huko Mbeya amefanya fujo, sasa mnamleta Dar es Salaam anafanya fujo, na Dar es Salaam siyo fujo. Tumetangaza na tumetoa taarifa serikalini mipaka ya halmashauri imechukuliwa, Tamisemi wamekaa kimya, mkuu wa mkoa amekaa kimya."
"Mimi naiagiza serikali na leo hoja hii ya huyu mkurugenzi tunakwenda nayo kwa waziri mkuu."
Awali, Selasini akiomba mwongozo huo, alisema Kabwe akiwa mkurugenzi wa jiji la Mbeya ndiye aliyeipa kampuni hiyo kazi hiyo.
Hata hivyo, alisema Kabwe aliondoka Mbeya baada ya kelele za madiwani na wananchi na kuliachia jiji hilo hasara kubwa.
"Kabwe huyo huyo alipelekwa Mwanza na pale Mwanza ameacha hasara kubwa sana. NSSF pamoja na viwanja, ambavyo aliuza na fedha hazikujulikana zilikokwenda. Lakini amehama na kampuni hii," alisema Selasini.
Aliongeza: "Kabwe huyu huyu aliondoka Mwanza baada ya kelele kubwa za wananchi pamoja na madiwani. Mheshimiwa mwenyekiti, sasa Wilson Kabwe yuko pale Dar es Salaam, Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam."
Alisema akiwa Dar es Salaam, nako pia ameanzisha mtafaruku mkubwa akipora vitega uchumi vya manispaa akizifanya kuwa za jiji.
Selasini alisema Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imeshatoa maelezo na mapendekezo mengi kwa serikali kuhusu Kabwe, lakini hakuna hatua zinazochukuliwa.
"Mheshimiwa mwenyekiti, picha inayotolewa ni kwamba, inawezekana Wilson Kabwe mkurugenzi anao wakubwa wanaomlinda huko Tamisemi," alisema Selasini.
Aliongeza: "Sasa mheshimiwa mwenyekiti, naomba mwongozo wako, kama hii kampuni ya Tanzania Building Works itachunguzwa, kwanini isichunguzwe sambamba na Wilson Kabwe ambaye ameonyesha kwamba kila anapohama, anahama nayo na kuipatia kazi kwenye maeneo, ambayo anapewa?"
CHANZO: NIPASHE