Msikiti wa Mtambani Unawaka moto tena

Msikiti wa Mtambani Unawaka moto tena

mrangi

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2014
Posts
96,481
Reaction score
138,348
attachment.php
attachment.php


Msikiti wa Mtambani Umewaka moto tena. Safari hii Polisi wa zimamoto wamefanikiwa kuuzima moto huo. Siku chache zilizopita Msikiti huo uliwaka moto na kuunguza Vitu mbali mbali ambapo ulizua mjadala mkubwa kwenye hii thread Msikiti wa Mtambani Kinondoni waungua Moto. Hadi sasa bado chanzo cha moto hakijajulikana
 

Attachments

  • JF_mtambani00.jpg
    JF_mtambani00.jpg
    35.4 KB · Views: 2,633
  • mtambani11.jpg
    mtambani11.jpg
    36.4 KB · Views: 2,608
Kuna habari ya kuteketea kwa msikiti wa mtambani uliopo kinondoni dar es salaam
chanzo cha habari Radio Tumaini
 
Leo ni siku ya kusali. Chanzo kitakuwa ni nini? au ni umeme?. Je kuna historia ya viashirio vya migongano ya wahumini?

Maswali ni mengi ya kujiuliza, kwanini mfululizo wa misikiti kuungua? Mungu awainue na kuwa nanyi, pia kuwalinda huku mkiwa kwenye ufalme wake au mikononi mwa MUNGU.
 
radio manzese zinaripoti kuwa kuna ugomvi wa kiuongozi kati ya vijana na wazee!
 
Leo ni siku ya kusali. Chanzo kitakuwa ni nini? au ni umeme?. Je kuna historia ya viashirio vya migongano ya wahumini?

Maswali ni mengi ya kujiuliza, kwanini mfululizo wa misikiti kuungua? Mungu awainue na kuwa nanyi, pia kuwalinda huku mkiwa kwenye ufalme wake au mikononi mwa MUNGU.

Amiyyyyyn!!!!!!!!
 
hmm if it's true there must be a REASON BEHIND
mtambani kunawaka tenaaaaaaàa?????


mwenye info zaidi atu thibitishie pamoja na picha
POLEN SANA MUNGU AWAPE SUBRA
 
Wazee na vijana...hawa vijana wanaendekezwa sana....wametumika kwenye vurugu misikiti mingi
 
mkuu wazee wengi ni vibaraka wa serikali na vijana wengi ni wanaharakati na wapenda mabadiliko hapo ndo kwenye shida

Mkuu, lakini vijana wanafanya vutugu. Kwanini wasiweze kujenga hoja na kuwapindua wazee kwenye chaguzi za uongozi au waweke vijana wasomi na wawe viongozi wa msikiti?
 
Yaani hapa hatujaruhusu mahakama ya kadhi wanafanyiana hivyo,tukiiruhusu akina MZIMU watawadhuru sana wenzao,
 
Last edited by a moderator:
: Moto umezuka katika
msikiti wa Mtambani kinondoni jijini Dar
es Salaam na chanzo hakijajulikana.
Tutaendelea kukujulisha zaidi
 
Watu washapiga mpunga. Sasa wanataka kutakatisha ulaji wao. Nji hii!!
 
Ndugu wanajamvi,

Napita hapa hapa Mtambani mida hii naona wananchi wamekusanyika kuzunguka hapa msikitini na gari la zimamoto ndio linawasili. Kuna taarifa kwamba jengo la msikiti wa mtambani limeungua moto tena. Inasemekana moto umeanza kuwaka muda mrefu na kwa kweli sijaona dalili zozote za moshi. Nadhani labda utakuwa umezimwa na raia wema au umewaka hadi umezimika wenyewe.

Mimi najiuliza hivi, hii itakuwa ni ajali ya kawaida au kuna mkono wa mtu?

:israel:
 
Back
Top Bottom