Msikilizeni huyu Meneja Mawasiliano wa SUMATRA David Mziray....Is he SIRIAZ...????

mzee wa njaa

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
1,366
223

David-Mziray.jpg

“Mv Skagit ilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 300 pamoja na mizigo tani 26, hivyo kulingana na idadi ya abiria 288 walioondoka katika chombo hicho isingeweza kuleta madhara kama hayo, ila tunawasiwasi waliongeza abiria njiani au mawasiliano ya hali ya hewa” Kwa mujibu wa Meneja Mawasiliano David Mziray.

Kauli hii inaufanya umma wa watu ambao sasa ni waelewa kwa asilimia kubwa kuamini kuwa baadhi ya taasisi za serikali watendaji wake wanafanyakazi pasipo kujua wanafanya kazi gani.

Haiwezekani leo hii useme kuwa Boti ile inawezekana iliongeza abiria njiani...sasa wapi kuna gati huko baharini na hao abiria wanatokea wapi? ilhali safari ya boti kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar (Unguja) hakuna kituo hapo njiani.

Lakini labda SUMATRA wana gati mpya Bagamoyo au Mbezi Beach huko. Ila hakika huu ni mtokoto wa mwaka 2012 na ni dharau kwa roho za watu na mali zao kwa mamlaka yenye dhamana ya kusimamiusafiri nchini.
 
"Mv Skagit ilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 300 pamoja na mizigo tani 26, hivyo kulingana na idadi ya abiria 288 walioondoka katika chombo hicho isingeweza kuleta madhara kama hayo
Mbona huwa hawasemi ilikuwa imebeba mizigo tani ngapi?
 
Masharti ya ununuzi hayakuzingatiwa.

-Abiria wasizidi 148
-meli isibebe mizigo

Siyo sahihi hata kidogo eti meli iliruhusiwa kubeba abiria 300 na mizigo tani 26.
 
Masharti ya ununuzi hayakuzingatiwa.

-Abiria wasizidi 148
-meli isibebe mizigo

Siyo sahihi hata kidogo eti meli iliruhusiwa kubeba abiria 300 na mizigo tani 26.

watawala wetu bado wanafanya kazi kwa mazoea/kizamani sana,hawajui kama kuna mjadala unaendelea huko Marekani kuhusu hiyo feri iliyopinduka na kuzama!
 
The m.v. SKAGIT was designed to carry a maximum of 230 passengers. The passenger-only ferry and a sister, the KALAMA were constructed in 1989 at Halter Marine in New Orleans, Louisiana. The original design of the boats was based on vessels that serviced off-shore oil rigs in the Gulf Of Mexico. An extra deck of superstructure was added to accommodate additional passengers. The boxy design of the cabin decks and the low twin funnels on either side gave the ferries a rather ungainly appearance. The SKAGIT went by the official number: D949140, call sign: WAA6309 and had a length of 112 feet, beam of 25 feet and a draft of 8 feet. The pair were ordered for service on Puget Sound but were laid up on arrival when there were no funds available to operate them. With the Loma Prieta earthquake in the San Francisco Bay area, the twins were loaned to that city to ferry passengers while the Bay Bridge was temporarily closed. After returning north, the 25 knot ferries entered service but met with complaints regarding erosion caused by their large wakes and their propensity to roll in the waves. They ultimately met with success when the route was transferred between Vashon Island and downtown Seattle. Washington State Ferries decided to discontinue their passenger-only service after the summer of 2009 with the SKAGIT and KALAMA being declared surplus. In an interesting move, the state tried unsuccessfully to sell them on eBay. They were finally sold in 2011 and taken to Tanzania where they operated for the Seagull Company between the mainland and Zanzibar.

Source:

MV SKAGIT, Former U.S. Ferry Capsizes Off Tanzanian Coast | MaritimeMatters

Maajabu toka SUMATRA, meli yenye designed maximum capacity ya passenger 230 inatetewa kuwa uwezo wa kubeba abiria 300 pamoja na mizigo tani 26. Meli iliyokuwa na ugonjwa wa kuyumba ikipigwa na mawimbi hapa kwetu inaonekana inafaa!!! Kweli Tanzania kichwa cha mwenda wazimu,
 
Hii melim ilipelekwa mombasa ambapo kuna"gereji" ya kuzirekebisha na ikaongezewa urefu hivyo ingekua na uwezo wa kuchukua abiria zaidi kuliko ilivyotengenezwa (japokua sii salama)
 
Uko sahihi kabisa, this can only happen in Tanzania . Utanikumbusha jinsi Omari Nundu alivyokuwa anashupalia tununue vitu vichakavu including Ndege na injini za gari moshi . Hii Tabia ya wafanyakazi wa serikali na wanasiasa kutokufanya biashara.

Vituko ni vingi mno CCM walianza kurushusu mitumba ya nguo soksi na chupi, wakaendelea na Magari madogo ya watu binafsi wakaendelea hadi wakaruhusu kutumia chai maharage kubeba abiria .
Hadithi inaendelea wakaruhusu hiace kubeba abiria Leo hii wameruhusu pikipiki kubeba abiria na Kikwete ameamua kuruhusu Bajaji ziwe ambulance . Sitashangaa kesho baiskeli zikaruhusiwa kubeba abiria ili kupunguza foleni Dar.
Kama tusipoiondoa ccm madarakani hata kwa kutumia staili ya Libya we are to see a lot of funny undertakings by ccm how do you exempt tax over 1.2 Trillion shillings and bow to EU wakupatie Euro milioni 136 kwa mbwembe na huku fedha zikielekezwa kwenye mambo ya kipuuzi yasiyo endelevu??
 
Hii yote ni kwa sababu wanajua watanzania wengi huwa wanashau mapema mambo ya msingi na hata kwenye kuchagua viongozi watanzania hawako serious ndiyo maana jamaa wanachezea tu maisha yetu wanajua hakuna wa kuwahadhibu maana mwenye kura yake (mtanzania) hayuko seriuous sasa kwa nini jamaa asitoe majibu ya kipuuzi. Ninavyojua meli kabla ya kuondoka lazima ofisa wa SUMATRA apite sehemu wanazokaa abiria akague kuhakikisha kila abiria amekaa kwenye seat na hakuna abiria aliyezidi na ndipo anaruhusu meli kuondoka lakini hapa hawafanyi. Hivi sasa ni hatari kupanda ndege,basi na hata meli maana hakuna taasisi zinazotuhakikishia usalama wa hivyo vyombo ni hatari kubwa unapokuwa huna taasisi inayomuhakikishia mwananchi usalama wake anapokuwa anasafiri itafikia watu wataanza kuogopa kusafiri na ndiyo mwanzo wa kuanguka kwa uchumi
 
Hii melim ilipelekwa mombasa ambapo kuna"gereji" ya kuzirekebisha na ikaongezewa urefu hivyo ingekua na uwezo wa kuchukua abiria zaidi kuliko ilivyotengenezwa (japokua sii salama)
Wewe nawe! Punda ana uwezo wa kubeba watu wawili, huwezi kumfunga kiti nyuma ili abebe zaidi.
Back to the topic: Usishangae kuwa huyo meneja wa SUMATRA hawahi hata kuiona bahari ndio maana akasema hivyo. Njia ya Bahari DAR-ZNZ si barabara ya Posta-Mwenge.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom