Msikilize Lusinde akiuza sera za CHAMA CHA MAPINDUZI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msikilize Lusinde akiuza sera za CHAMA CHA MAPINDUZI

Discussion in 'Jamii Photos' started by Bujibuji, Apr 5, 2012.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,289
  Likes Received: 22,056
  Trophy Points: 280
 2. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,132
  Trophy Points: 280
  Huyu ni mbunge kweli au zuzu magic?
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Apr 7, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280


  Kudadeki ahhhhhhhhhhhhhh Hivi huko bongo kuna Siasa au mambo ya kihuni?????????????????????
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Hotuba ya Livingstone Lusinde Katika Maandishi Kutoka Wavuti


  Mh mwenyekiti wa chama, waheshimiwa viongozi wenzangu na wanachama wenzangu, nataka nianze kutofautiana hapahapa jukwaani na wenzangu, habari ya sisi kutukanwa halafu tunasema sisi hatutukani hatufanyi kazi ya kanisa hapa, kudadadeeekimatusi yakija nitatukana hoja zikija nitasema, potelea mbali

  CCM oyeeeee.......oyeeee!

  Niseme nisiseme.....semaaaaaa!

  Unajua kuna wabunge wa chadema maji marefu unawalea sana, wewe ndio uliowachanja chale mpaka matakoni leo wanakutukana, nataka niwaambieni wenzetu wanajifanya wanajua kutukana hapa mwisho! ndio maana nimekuja kuwapasha kwamba hoja nyingine za kipuuzi wanazozisema chadema wanajitukana mpaka wao wenyewe, kuja kusema hapa kwamba mgombea wa ccm katoboa sikio kwa hiyo ni shoga maana yake na baba yake slaa nae ni shoga maana nae katoboa sikio kudadadeeeki CCM oyeeee....oyeeeee


  Nataka niwaambie ndugu zangu msindanywe, msidanganywe na rangi utamu wa chai sukari, wale waliojazana katika chadema wote karibu nusu baba zao wametoboa masikio kwa hiyo na wao mashoga? Niwaambie nisiwaambie. . . .waambie! mbunge wa arusha mjini juzi alikua mahabusu na si tunajua kule mahabusu alifanywa nini, lakini hatutaki kusema

  tuwalambe tusiwalambe.....walambeee!

  Ndungu zangu nataka niwaambieni kwa habari ya lugha chafu wote sisi tunazo wala msifikiri hatujui sisi hatuna, tunajua Lema alikua mahabusu amepata bwana kule tunajua, na kuna wanaume wengine wameolewa sisi tunawafahamu, nataka kuwasihi sana, kwenye uchaguzi, kwenye uchaguzi tunajenga hoja za msingi lakini wakileta maneno ya honyo na hapa yapo, kudadadeeeki

  nataka niwasihi sana, hakuna mtu asiye na makosa duniani, leo dr slaa anapita kuwasema wenzake wakati yeye upadri ulimshinda kanisa likamfukuza kwa kutia mimba wanakwaya

  Sioi oyeeee! Oyeeee!

  Mi nawafahamu wale, unajua tukiendelea kuwachekea hivi tukiendelea kuwambeleza hivi itafika mahali watatuchokoa machoni bora tule nao sahani moja, kuna
  *****
  mwingine yuko mle, kuna ***** mwingine yuko mle anajiita campain manager wa chadema, ukoo wa nyerere, baba yake mzazi wa nyerere akiitwa buhito alikua akitoboa masikio, alikua shoga? anajitukana mpaka mwenyewe kwa sababu ya akili mbovu, kutoboa masikio sio ushoga, masai wanatoboa, wagogo wanatoboa, wameru zamani walikua wanatoboa, wa-wakurya wanatoboa, wakamba wanatoboa, ye hajui historia anakuja hapa (huku kabana pua) ng'wee ng'wee ng'weeee, mbona ye ameliwa si hatusemi

  ccm oyeee, oyeeeee
  wanaokipenda chama mikono juuu!

  (sauti ya kike kwa mbaali inasikika - wamekwisha!)

  subiri niwaambie, hoja zinazojengwa hapa ni hoja za kipumbavu, kuna watu wanakuja kujenga hoja ya kitoto, kwamba msimchague sioi kwa sababu alizaliwa kenya, sio raia wa tanzania, mtu akizaliwa kwenye ndege anakua raia wa nchi gani? Acheni ushamba nyie, Suala la mtu kuzaliwa na suala na uraia ni vitu viwili tofauti, uchungu unapompata mwanamke anazalia hapohapo hawezi kusubiri, kuna wengine wamezaliwa kwenye mabasi mbona hatuwaiti raia wa basi, washamba wakubwa nyie, hiyo mnaona ni hoja ya kupita mnazungumza, halafu nyingine wanapita wamebana pua, msimchague sioi kwa sababu baba yake alikua mbunge, baba yake atarudi lini? Baba yake anarudi?

  Ngojeni niwaeleze, na bahati nzuri najua walipo ntakua napiga hapa afu napiga palepale, kudadadeeeki . . .

  CCM oyeee .....oyeeeee!
  Msikubali kudanganywa ndugu zangu maswala ya mtoto kufata kazi ya baba yake, katika tanzania ni kitu cha kawaida, tunao wanajeshi na watoto zao wanajeshi uongo kweli?....kweliiiiii! tunao madereva na watoto wao madereva uongo kweli?.....kweliiii, tunao wapiga debe na watoto zao wapiga debe uongo kweli . . . kweliiii! kuna ajabu gani kwa sioi piga makofi kwake.

  Niwaulize nisiwaulize.....ulizaaaaaaa! Marehemu sumari angekua daktari na mtoto wake daktari CHADEMA wangegoma kunywa dawa (sauti ya kimbea kwa mbali inajibu . . . . wathubutu!), washamba nyie!

  ccm oyee. . . oyeeee! Niwalambe nisiwalambe. . . . walambeee!

  Ndio maana tunataka tuwaambie chama cha mapinduzi ndiyo chenye makamanda wa ukweli sio nyie makamanda feki, Jakaya Kikwete mwenyekiti wa ccm kazi yake zamani alikua mwanajeshi uongo kweli?..... kweliiii, kapteni komba alikua mwanajeshi uongo kweli? .......kweliiii! lakini wanavaa nguo za kijani halafu washamba ambao hata mgambo hawajapita wanavaa makombati.

  ccm oyeee.....oyeeee!


  Halafu katika washamba hakuna mshamba kama dokta slaa, anavaa kombati kuuubwa akitembea kama kajinyea vile (anapata shangwe kutoka kwa wanaomsikiliza, sorry to say this hapa hata mke wangu alicheka, nikamtazama kwa hasira hadi akaogopa!)

  Nipige Nisipigeee?.........Pigaaaaaaa aaaaa
  Bendera ya CCM ina rangi ganiiiiiiiiiiiiii?............ .......Kijaniiiiiiiiiiiiii.
  Ukipanda mahindi yanaota na rangi ganiiiiiiiiiiiii?............K ijaniiiiiiiiiiiiii.
  Ukipanda mpunga unaota na rangi ganiiiiiiiiiiiiii?............ .Kijaniiiiiiiiiiiiiiii
  Migomba yote ina rangi ganiiiiiiiiiii?............... ............Kijaniiiiiiiii.
  Piga makofi na vigelegele kwa chama cha mapinduzi.

  Nataka niwaambie kama CHADEMA, kama viongozi wa CHADEMA ni vichaa wa kurogwa, mie ni kichaa wa kuzaliwa, kudadadeeeki!tarehe moja, dk slaa juzi, (anaguna) yaani katika watu washamba nimewashangaa dk slaa, anakakaa kwenye tv anasema eti ''ooooh hapa isipochaguliwa chadema patachimbika'' kama ni fujo itaanzia arumeru, kwa nini isingeanzia kwa mke wake? Ngoja niwaambie ndugu zangu, alichokua anakisema slaa, alichokua anatutishia vita slaa mimi namwambia anatishia kujamba wakati anaharisha.

  ccm oyeee....oyeeee!. wangapi mtampa kura kura sioi, mikono juu....(watu wananyanyua mikono), hatufanyi kazi ya kanisa hapa! hapa tumekuja kuwaambia kwa suala la kutishana hakuna mtu anayeogopa, wote si tumeaga na nataka niwaambie slaa yule anavimba macho ya watu, lakini kama slaa ana ubavu nipeni mi tuweke ulingo hapa, ngumi moja naua yule, nikikusanya yule nipige mkono mmoja mnakuja kuokota yule, akiona watu wamejaa (anabana pua) ng'weng'weng'wee ng'weng'weng'wee upadri umemshinda ataweza serikali? thubutuu!

  Nataka niwaambie, ndugu zangu wa arumeru, suala la uchaguzi mdogo sio suala la kudanganywa, wanakuja CDM hapa wanakudanganyeni, kwamba watapora mashamba ya wazungu wawagawieni, muasisi wa chama cha CDM ndugu mtei ana shamba hapa heka 700 mbona hawampori wawagawie? wangeanza kwanza la mtei, sio kuwadanganya wananchi, kama wanawapenda kweli wa meru wamwambie mzee mtei chukua shamba lako rudisha kwa watu wa meru(sauti ile ya kike. . . hatudanganyiki)

  ccm oyeee.....oyeeee!
  Niwachane nisiwachane?......wachaneee!

  Vijana wenzangu, CDM inawapa pesa za kunywa viroba, mnalewa viroba na bangi mnazomea wazee wenu, halafu wenzenu wanapita na helikopta wanawaona machizi

  niseme nisiseme.....semaaa!

  Kokote duniani askari wanaoteka nchi ni askari wa miguu wacha wao waruke juu si tunateka nchi, wao wanaruka na helicopter si tunachukua jimbo asubuhi, kudadadeeki, mnakuja mnadanganywa hapa eti ooh chadema, sijui ooh nasari ataleta ajira na soko, ajira atazitoa wapi? Watu hawana shukrani anasimama hapa dk slaa anatukana ccm, hawajafanya kitu, hawajafanya kitu, shule alizosoma yeye zimejengwa na baba yake? shule zimejengwa na serikali ya chama cha mapinduzi, watu wanajiita wamesoma chuo kikuu (chuo hicho) kimejengwa na serikali ya chama cha mapinduzi, nionesheni hapa chuo walichojenga CDM. . . hakunaaa!

  ccm oyeee....oyeeee!

  Wanatuletea sera ya jogoo, nataka mkatae sera ya CDM ni sera ya jogoo, Jogoo katika makuku maongo hakuna kama jogoo, Jogoo linapokua linamtaka kuku mwenzake linadanganya linamwambia nitakushonea gauni reeefu mpaka huku (anainama huku akizunguka kuonyesha mfano wa jogoo, watu wanalipuka kwa kicheko)

  Niseme nisiseme. . . .semaaaa!

  Kataeni uongo wa jogoo, linaahidi kushona gauni refu wakati lenyewe likiinama hata chupi halina, waongo wakubwa tunawajua, na hivyo viroba mnavyokunywa vijana, viroba mnavyokunywa vijana mwisho tarehe moja, wataondoka watakuacheni mmetukana wazee wenu, mmewapiga mawe wazee wenu, na mimi nataka niwaambie vijana wa CDM utaonekana kichaa ukionekana unazomea rangi ya kijani maana utakuta mti una rangi gani....kijani! unaanza uhuuuu watu wanasema huyu chizi, mchezaji aliyeumia ni mchezaji wa timu ya ccm tunaweka mchezaji wa ccm, suruali yangu nyeusi imetoboka siwezi kuweka kiraka cheupe kama nina akili nzuri, inabidi niweke cha rangi gani? Kijaniii! Hata hilo mnataka mtu atoke dodoma kuja kuwaambia? Kama huoni kwa macho papasa kwa mkono utapa majibu.

  Ccm oyeeeee.....oyeeeee!


  Niwaambie nisiwaambie hawa.....waambie!...ngoja niwaambie watu wa CDM nyie

  nikakutana na kijana mmoja akanichekesha sana, ananiambia mwanaume mzima, basi kati ya watu ambao hawajui kiswahili mbowe hajui kiswahili, mbowe anasimama anasema nina uchungu mkubwa, bibilia inasema hivi wanawake mtazaa kwa uchungu, wanaume watakula kwa jasho uongo kweli...kweliiii! kama mbowe anauchungu ana mimba?....vicheko

  ccm oyeeee.....oyeeee!

  Nataka niwaambie, kipindi hiki ni kipindi cha lala salama, ukiona mtu anasikia kichefufu, ukiona mtu anatema mate, ukimuona mtu anaichukia ccm ujue tayari tumeshamtia mimba, ndio maana unawaona saa hizi wanapiga kelele, unaona kina slaa wanapiga kilele, wameshapigwa mimba, mbowe pigwa mimba, nasari pigwa mimba....mayoweee

  Tarehe moja wanaenda kujifungua mtoto anaitwa sioi, piga makofii. Kichefuchefu chote kitawaisha utawaona ooh tulikua pamoja tulikua pamoja kudadadeeki.

  Niwachane nisiwachane?.....wachane!

  we ukiona unapita mwanaccm humsemeshi mtu anakufanyia hivi (anaonesha V, ishara ya CDM) ujue ana mimba ya mapacha, mnunulie udongo, mnunulie maembe mabovu, mnunulie vitu vya uchachu tarehe moja anajifungua sioi anakwenda bungeni na wao mimba wanazaa hapohapo.

  Tuwapime wenye mimba tusiwapime....tuwapimeeee
  Tuwapime wenye mimba tusiwapime....tuwapimeeee

  nitakuuliza swali, nitakuuliza swali, atakaempigia kura sioi anyoshe mkono kama hakunyosha jua ana mimba

  ccm oyeeee....oyeeee!


  Source: "Kudadadeki, matusi yakija nitatukana, hoja zikija nitasema..." - L. Lusinde - wavuti.com*
   
 5. SaidAlly

  SaidAlly JF-Expert Member

  #5
  Apr 7, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,798
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Dah! Kweli inasikitisha, mtu kama huyu ndio wakumvua ubunge haraka sana maana amechafua kabisa hadhi ya ubunge.

  kwenye utetezi wake anadai aligadhabika...hivi kweli muda wote huo anaporomosha MIJITUSI hiyo alikua peke yake? Hakukuwa na kiongozi wa ccm akamtuliza hiyo gadhabu?

  Mie naona wote waliona ni sawa na sahihi, na inavyoonyesha alijipanga muda mrefu jinsi atakavyo yavurumisha hayo matusi.

  Dah, tunakoelekea kweli kubaya.
   
 6. salito

  salito JF-Expert Member

  #6
  Apr 7, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  mimi siasa hata sijui,lakini sidhani kama haya ni maneno stahiki ya kiongozi,huyu ni kiongozi wa ngazi gani alieongea hivi?
   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  Apr 7, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Mbunge..
   
 8. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #8
  Apr 7, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  ccm ndo aina ya wanasiasa walioko nao wanawatuma kuomba kura kwa watu wenye heshima zao na wanamjua na kumwamini Mungu
   
 9. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #9
  Apr 7, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kweli siasa ni uendawazimu..
   
 10. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #10
  Apr 7, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,451
  Likes Received: 4,734
  Trophy Points: 280
  Mimi nakataa kwamba siasa ni mchezo mchafu ila nakubali kwamba WANASIASA NDIO WACHAFU
   
 11. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #11
  Apr 7, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,451
  Likes Received: 4,734
  Trophy Points: 280
  Wataalamu wanasema kwamba Kenge ndiye mnyama anayeongoza mkwa mdomo mchafu akifuatiwa na Paka na hatimaye niseme ukweli kamba wa tatu atakua LuSINDE
   
 12. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #12
  Apr 7, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Mzizimkavu ni nomaaaa umetishaaaaa!
   
 13. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #13
  Apr 7, 2012
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,898
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Wamevuna walichopanda.Sasa kwa speech kama hii huyu mbwiga alidhani anakampein au ndio anafukuza kura za chama chake?Na wasipojiangalia na kuendekeza mijinga kama hii verry soon CCM will be a history..
   
 14. mgeni10

  mgeni10 JF-Expert Member

  #14
  Apr 7, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 1,112
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wanao wakilishwa nae Wamechemsha, Hawatapata kitu HUMU
   
 15. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #15
  Apr 7, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  na kasema anajiandaa kwenda arusha tena
   
 16. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #16
  Apr 7, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  .... Usingizi wa ndondocha!!! Consuming the whole Nation!!!

  .... How Long? How Long?!!!!
   
 17. TASLIMU

  TASLIMU Senior Member

  #17
  Apr 7, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmmmmmm!!!huyu Lusinde ndo ameng'oa MARECHELA,
   
 18. Emilia

  Emilia JF-Expert Member

  #18
  Apr 7, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 266
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  my Lord..nimecheka hadi huzuni ya Kanumba
  imepungua.
   
 19. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #19
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  He he naji marefu aliwachanja chale mpaka matakoni...tt sentence just made me laugh insanely
   
 20. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #20
  Apr 8, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,872
  Likes Received: 6,222
  Trophy Points: 280
  hhahaaaanananaaaaaaa imebidi nicheke tu
   
Loading...