Katika somo la habari,ukiacha mambo bilakuyatolea maelezo,unatengeneza ombwe la habari.
Ukitengeneza ombwe la habari, habari ina tabia ya kukataa ombwe, zitajiweka habari zozote, zichukue sehemu ambapo habari imekosekana.
Kwa msingi huo, ni rahisi sana kwa watu kusema serikali haijalaani mabomu haya kwa sababu imeyapanga yenyewe.
Serikali kutokemea ugaidi huu hakusaidii kutupa imani kwamba haijahusika na hata kama kauli hiyo haitakuwa sahihi, itaaminika zaidi kwa kuwa serikali haijakemea ugaidi huu.
Ndiyo maana ni muhimu sana kuweka wazi msimamo wa serikali kuhusu mambo haya.