It seems that you are not well educated regarding Governance in a given country. Kama ilani ya chama ndiyo huongoza kila kitu cha maendeleo nchini, jiulize kwa nini nchi huridhia makubaliano ya kimataifa? kwa nini nchi huwa ni mpango wa maendelao kwa mfano wa 2025 wakati ilani ya chama ni ya miaka mitano tu? kwa mfano tuna mpango wa kimataifa wa maendeleo wa 2030. Kwa nini tuna katiba? kwa nini tuna sheria na miongozo ya kisekta? tena sheria zingine ni za miaka ya nyuma kabisa kabla hata ya hiyo ilani ya juzi tu. Kwa nini tunafanya tafiti za kitaalamu wakati ilani ipo? My friend, for national development, you need to go beyond the mere interest of your party. Kwani daktari inahitaji ilani imuelekeze namna ya kumpasua mgonjwa au utaalamu ndio humuongoza? Mjenzi wa reli ilani inamsaidia nini katika utaalamu wa kuijenga? Ukweli ni kwamba kazi nyingi za maendeleo ya nchi huongozwa na utaalamu na siyo propaganda za ilani ya chama. Mkulima anasaidiwa nini kwenye utaalamu wa kilimo na hiyo ilani? Kwa kweli Ilani ya chama cha siasa ni sehemu ndogo sana ya mambo ya kusimamia kuleta maendeleo kwa sababu haijumuisha mambo mengi kiundani. Party manifesto is not Comprehensive enough to guide practices in development sectors. Tuna sekta nyingi sana za maendeleo ambazo mambo yake muhimu hayawezi kubebwa na kakitabu ka ilani. Ukubwa/ujazo wa ilani huwa ni sawa au mdogo kuliko sera ya sekta moja tu. Ukweli ni kwamba wanasiasa na ilani zao huwa na nafasi ya kusimamia tu yale ambayo wataalamu wameyapanga. Narudia tena kusema Ilani ya uchaguzi ya chama tawala ni sehemu ndogo tu ya kusimamia kuleta maendeleo ya nchi. Hamuwezi kuwagawia watumishi wote wa umma ilani ya uchaguzi mkadhani ndio maendeleo yatakuja. Nasema tena ilani ya chama si jumuishi bali ni ya kakikundi ka watu wa itikadi fulani. Natoa wito tusipoteze muda kuwagawia watumishi wa umma ilani ya chama eti iwaongoze kufanya kazi. Kazi za maendeleo huongozwa na utaalamu usiopatikana kwenye ilani bali kwenye taaluma husika. Hivi Rubani anayeendesha ndege unampa ilani imsaidie nini wakati ndege hurushwa kwa utaalamu? Acheni kupoteza muda na fedha za kurudufisha ilani badala ya kuwapa watu hizo fedha wafanye tafiti, na mengine ya kitaalamu.