Msigwa awachezesha kwata CCM Iringa

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
122,485
96,050
Hongera sana mbunge wa Iringa kwa kuwachezesha kwata kadri unavyotaka wapinzani wako CCM.

Sasa ni takribani wiki ya pili viongozi wa CCM wanashinda mitaani wakipaka rangi shule za msingi bila kupenda wakiwa na lengo la kutafuta ushawishi toka kwa wana Iringa bila mafanikio.

Hongereni wana wa Iringa kwa kukataa kudanganyika, mbunge wa kweli ni yule anayewajali wapiga kura wake na siyo kipindi cha kutafuta kuungwa mkono.
 
Sasa hapo kawachezesha kwata gani?

We kijana acha viroba,punguza stress,piga kazi. Hao wanaopiga rangi wanatimiza wajibu wao.....wewe soon maisha yatakupigisha kwata la kimyakimya
Miaka yote walikuwa wanajiona mungu watu lkn baada ya kukataliwa sasa inabidi wapige kwata ili kuwashawishi wapiga kura jambo ambalo tayari wameshachelewa
 
Kwa hiyo wanaopaka Rangi ni CCM au Serikali? CCM wanabajeti ya kapaka rangi kwenye mashule? Hizi siasa zimeharibu sana ubongo wa vijana.
 
Back
Top Bottom