Msichana kuwa makini unapokuwa hosteli (room)

NAKWEDE

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
27,971
35,118
Nawasalimu wana JF wote.

Kama kichwa cha habari kinavyoeleza, naomba kuwaasa wanafunzi hasa wa vyuoni wanapokuwa vyumbani kwao wawe makini. Wanachuo walio wengi aidha wawe hosteli za chuoni au za kupanga nje ya chuo huwa wanakaa zaidi ya mtu mmoja.

Umakini ninaouongelea hapa ni kwamba, usipende kukaa naked mbele ya wenzake hata kama ni wanawake wenzio, wala kukaa nusu uchi. Pia usipende kulala bila nguo halafu ukaacha kujifunika shuka au blanketi.

Athari ni kwamba, wenzio wanaweza kuwa sio watu wema, wanaweza kukupiga picha kwa siri sana wewe ukiwa hujui na kuanza kuzirusha kwenye mitandao ya kijamii, utadhalilika.

Nimemaliza.
 
Hakika mkuu visa hivi ni common kwa sasa.Pia kupiga picha za uchi na kuhifadhi kwenye simu nalo ni janga.Unaweza poteza simu au kumpa mtu ASIE mwaminifu.
Au hizo picha anazi save kwenye laptop, siku laptop ikiharibika akipeleka kwa fundi, fundi naye anafanya yake na zile picha!!!
 
Kwanini ulale uchi bila nguo wakati uliolala naye siyo mumeo/mkeo?
Huu ni uporomokaji mkubwa wa maadili.. Halafu wasomi wa siku hizi bhana, hivi unampigaje picha za uchi mwenzako bila ridhaa yake na kutuma mtandaoni?
 
Back
Top Bottom