*** Msibani kwa XYZ ***

Baba_Enock

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
7,076
2,445
Siku za hivi karibuni nimekuwa nikiona vibao vinavyoelekeza wapi palipo na msiba...
Msiba unatokea sehemu fulani na waliofiwa wanachukua jitihada za kuweka "vibao vya matangazo" vinavyoelekeza ni wapi ulipo msiba...

"MSIBANI KWA XYZ.."

Hivi kama hujawahi kufika kwangu nikiwa hai kwanini ufike nyumbani kwangu nikiwa chumba cha kuhifadhia maiti?

Labda ni matokeo ya maendeleo... Labda ni maendeleo yenyewe...
 
Watu wengi huficha wakaako mpaka kifo kikiwaumbua. Dereva wa ofisini kwetu alifiwa na mke na tulipofika home kwake wote tulishikwa na butwaa....hekalu kaka!
 
ni kweli mkuu...
Na binadamu kwa hila ndo maana wengi huficha wanapoishi kuepuka maneno maneno na fitina
 
Hivi, wote wanaokuja msibani unadhani wana mahusiano na wewe?

Hivi unadhani kinachotupeleka msibani ni marehemu tu?

Wakati mwingine tunakuja kuwasapoti waliobaki ambao tuko karibu nao.

Mfano, mfanyakazi mwenzangu kafiwa baba, najua anapoishi mfanyakazi huyo ila sijui anapoishi baba yake.
Kwa hiyo nisiende kumsapoti mfanyakazi mwenzangu sababu sijui anapoishi baba yake?

Think Baba Enock Think.

Hata marehemu anaweza kuwa kahamia makao mapya tofauti na nilikokujua.
 
Kongosho umesema vema sana...anaweza kuwa ni muumini mwenzio ambaye hamjawahi kuwa karibu
Mfanya kazi mwenzio ambae hakuwa karibu na wewe imagine ofisi iwe na wafanyakazi more than 200 si rahisi kujua kila mmoja anakaa wapi..NK NK lakini tukio la msiba na harusi huwa wanakuja unaowafahamu na usiowafahamu pia
 
@ Kongosho

Hawa unaokwenda kuwapa sapoti hawawezi kukuelekeza wapi msiba ulipo? I think I'm missing something somewhere...!
 
Siku za hivi karibuni nimekuwa nikiona vibao vinavyoelekeza wapi palipo na msiba...
Msiba unatokea sehemu fulani na waliofiwa wanachukua jitihada za kuweka "vibao vya matangazo" vinavyoelekeza ni wapi ulipo msiba...

"MSIBANI KWA XYZ.."

Hivi kama hujawahi kufika kwangu nikiwa hai kwanini ufike nyumbani kwangu nikiwa chumba cha kuhifadhia maiti?

Labda ni matokeo ya maendeleo... Labda ni maendeleo yenyewe...

Hoja nzuri na ina mashiko; lakini si wote wanakuja kwenye msiba kwa mapenzi au ukaribu waliokuwa nao kwa marehemu. Wengi wanakuja kwa ukaribu walionao na wafiwa yaani ndugu na jamaa za marehemu.
 
Kongosho umesema vema sana...anaweza kuwa ni muumini mwenzio ambaye hamjawahi kuwa karibu
Mfanya kazi mwenzio ambae hakuwa karibu na wewe imagine ofisi iwe na wafanyakazi more than 200 si rahisi kujua kila mmoja anakaa wapi..NK NK

Kwahiyo mabango ya matangazo ya nini? Unakwenda msibani kwa mfanyakazi mwenzio ambaye kwa vyovyote vile anafahamiana na mfanyakazi mwingine na mwingine... The bottom line ni lazima kutakuwa na mfanyakazi anayefahamu nyumbani kwa huyo aliyefikwa na mauti au aliyepotelewa na ndugu...
 
Sioni kama mabango yakufahamisha watu wapi msiba ulipo ni tatizo,inawapa watu wepesi wakufika baada ya kusimama wakauliza nakupoteza time...
 
Kwahiyo mabango ya matangazo ya nini? Unakwenda msibani kwa mfanyakazi mwenzio ambaye kwa vyovyote vile anafahamiana na mfanyakazi mwingine na mwingine... The bottom line ni lazima kutakuwa na mfanyakazi anayefahamu nyumbani kwa huyo aliyefikwa na mauti au aliyepotelewa na ndugu...

Wakati mwingine siyo vyema kuanzisha thread ambazo hazina mashiko! kuna shida gani kuweka kibao kama kuna watu hawajawahi fika mahali msiba ulipo? huyo mwingine anayepajua kama hujaongozana naye kwasababu kila mmoja ana gari lake na mmeenda msibani katika muda tofauti huoni kama hivyo vibao vinarahisisha mtu kufika ku-compliment maelezo ya direction aliyopewa mwanzo? aaaaah bwana nahisi una tatizo wewe!!
 
@ Kongosho

Hawa unaokwenda kuwapa sapoti hawawezi kukuelekeza wapi msiba ulipo? I think I'm missing something somewhere...!

Kiutamaduni nadhani hii itakuwepo kwa makabila mengi Tanzania na Afrika, mtu anapofariki ndugu na jamaa wengine hujumuika si tu kumlilia yule aliyefariki bali pia huwalilia jamaa wengine waliofariki kabla na kutangulia mbele za haki. Huu ni utamaduni ambao umekuwepo vizazi hata vizazi na ndio kinachoendelea kwa kiasi kidogo hata sasa. Kwa mlioishi vijijini mtakubaliana nami si haba kule kukuta watu wakiomboleza kwa staili kama, "eeeh oooh XXX kamsalimie fulani, mwambie nasi tutakuja".
Vingine Kongosho kavielezea kwa mapana.
 
Hapana baba, mie namlilia babangu, nahangaika na logistics na kuhakikisha mambo yanaenda sawa, unaweza kupiga simu yangu ikawa busy wakati wote ama isipokelewe. Kama kuna vibao inasaidia, saa zingine tunapigiana wa ofcn kuelekezana kwao king' ni wapi.

Ila nadhani utaratibu wa kichaga ndo mzuri. Msiba ukitokea kikao kinafanyika Mwika bar, maiti inaagiwa lugalo! Nyumbani kwa marehemu, kama hekalu ama kibanda cha miti haihuuu.
@ Kongosho

Hawa unaokwenda kuwapa sapoti hawawezi kukuelekeza wapi msiba ulipo? I think I'm missing something somewhere...!
 
Unawaelekeza kwa ramani ya wapi?

Masaki karibu na Sea Cliff? Tandale kwa Tumbo? Kimara bonyokwa? Madale? au Malamba mawili?

@ Kongosho

Hawa unaokwenda kuwapa sapoti hawawezi kukuelekeza wapi msiba ulipo? I think I'm missing something somewhere...!
 
Kwahiyo mabango ya matangazo ya nini? Unakwenda msibani kwa mfanyakazi mwenzio ambaye kwa vyovyote vile anafahamiana na mfanyakazi mwingine na mwingine... The bottom line ni lazima kutakuwa na mfanyakazi anayefahamu nyumbani kwa huyo aliyefikwa na mauti au aliyepotelewa na ndugu...

Baba Enock na wewe Bwana lol
Kama kila mtu anayetaka kuja kwako anapiga simu kuelekezwa hii ni kazi sasa.
Ndio maana watu wamegundua njia mbadala na rahisi
Msiba ukiisha wanaondoa mabango
Na si lazima watu wote mwende kwa muda mmoja kila mmoja anaenda kwa wakati wake katika eneo la tukio
Mie binafsi sioni tatizo..
 
Kwahiyo mabango ya matangazo ya nini? Unakwenda msibani kwa mfanyakazi mwenzio ambaye kwa vyovyote vile anafahamiana na mfanyakazi mwingine na mwingine... The bottom line ni lazima kutakuwa na mfanyakazi anayefahamu nyumbani kwa huyo aliyefikwa na mauti au aliyepotelewa na ndugu...

inategemea na ukubwa wa ofisi kwa mtu mmoja awapeleke....
Na uswahilini kwetu kulivyokaa, hakuna mipango mji unadhani bila vibao watu watafika? Ni muhimu kuelekeza direction, misiba ina mambo mengi hata kumpata mhusika nayo huwa isshu
 
kwa sisi wengineee tunasemaa msiba sio harusi hauna kadi...sikujui hunijuii ila nikiona msibaa naambatana na wafiwaaa.kislamu tunasema ni twawabu kumzika binadamu mwezako.
 
Back
Top Bottom