Msiba wa kusikitisha!!!!!!!

Msiba wa kusikitisha!!!!!!!

Aine

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
1,603
Reaction score
489
Kwa kweli hata nashindwa jinsi ya kuanza inavyotia simanzi!!
Kwa wale waliosoma Chuo cha Mzumbe miaka ya 2004, 2005, 2006, na miaka mingine na wote wenye mapenzi mema, kuna dada anaitwa MANSUETA MBENA alisoma LLB na kumaliza 2006, jana alinipigia simu amefiwa na mtoto wa dada yake, mkubwa tu amezalliwa 70's anaitwa Jenny kwamba amefariki juzi alikuwa anaumwa malaria. Sasa Mansu anafanya kazi mkoani, alipofika kwao tu akanipigia tena kwamba dada yake naye amefariki!!!!!! Yaani hadi mwili unataka kuganda, kwao ni Morogoro. Kwa hiyo kwao kuna misiba miwili na mazishi kwa marehemu wote ni kesho Jumamosi tarehe 14/5/2011 saa 9 alasiri .Wanakaa karibu na makaburi ya Kola na ukienda panda gari za Kilakala shuka kituo cha makaburi ya Kola kulia utaona watu wengi tu kwenye msiba. Jamani wale tulio karibu naomba tuende tukawafariji jamani maana misiba miwili si mchezo! Kweli Mungu AWAPE FARAJA YA PEKEE!! (Samahani wana jf nilipost kwenye utambulisho ni kuchanganyikiwa tu jamani mnisamehe tu!)
 
Nimesoma Kilakala girls maeneo hayo nayapata...
Poleni sana wafiwa bwana ametoa bwana ametwaa jila lake lihimidiwe
 
Pole sana wafiwa, na Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi..... Amen!
 
inaisikitisha naombea roho zao zipunzike kwa amani peponi.
 
Ni vigumu ukikabiri hali hiyo ngumu, lakini kwa Tumaini lililo kuu tuamini kuwa wametutangulia kwenye Uzima wa milele, kila nafsi ya mmoja wetu itakwenda huko ila wao wametutangulia tu.

Maeneo hayo nayaelewa vizuri sana, ni karibu na Ikweta Bar,Maeneo ya Lyasembe kwa kuwa sipo mkoa huo ntatuma mwakilishi ambaye ataniwakilisha.

Pole sana wafiwa!
 
Kwa kweli hata nashindwa jinsi ya kuanza inavyotia simanzi!!
Kwa wale waliosoma Chuo cha Mzumbe miaka ya 2004, 2005, 2006, na miaka mingine na wote wenye mapenzi mema, kuna dada anaitwa MANSUETA MBENA alisoma LLB na kumaliza 2006, jana alinipigia simu amefiwa na mtoto wa dada yake, mkubwa tu amezalliwa 70's anaitwa Jenny kwamba amefariki juzi alikuwa anaumwa malaria. Sasa Mansu anafanya kazi mkoani, alipofika kwao tu akanipigia tena kwamba dada yake naye amefariki!!!!!! Yaani hadi mwili unataka kuganda, kwao ni Morogoro. Kwa hiyo kwao kuna misiba miwili na mazishi kwa marehemu wote ni kesho Jumamosi tarehe 14/5/2011 saa 9 alasiri .Wanakaa karibu na makaburi ya Kola na ukienda panda gari za Kilakala shuka kituo cha makaburi ya Kola kulia utaona watu wengi tu kwenye msiba. Jamani wale tulio karibu naomba tuende tukawafariji jamani maana misiba miwili si mchezo! Kweli Mungu AWAPE FARAJA YA PEKEE!! (Samahani wana jf nilipost kwenye utambulisho ni kuchanganyikiwa tu jamani mnisamehe tu!)

Poleni wafiwa, mazishi shuka pale mti mkubwa.
 
Poleni sana wafiwa mungu awape faraja.

Wito wangu wanaJF, tujitahidi kuwa tunacheki afya zetu mara kwa mara si mbaya kujua health status kila baada ya miezi mitatu au sita inasaidia sana.
 
Poleni sana MANSUETA .....sisi ni mavumbi na mavumbini tutarudi....
 
Polen sana wafiwa wote Mungu awape faraja za mioyo. Wapumzike kwa amani. Amen!
 
2 in One? I can hardly imagine wafiwa wanafil aje. Poleni ndugu, inshallah mtapita kipindi kigumu hiki...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom