Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,055
Taifa lipo msibani!
Ni msiba wa kitaifa kuondokewa na mfalme wa sanaa nchini, King Majuto. Hakuna haja ya maelezo mengi maana historia yake inajitetea!
Nimetazama nyakati za mwisho wakati anapambania uhai wake Tanzania na India. Pongezi kwa waliofanya jitihada za kumuwezesha kumudu gharama za matibabu ikiwemo Serikali na wadau wengine.
Kifo cha mzee wetu kimetuacha na aibu. Aibu zaidi kwa Rais Mstaafu wa JMT, Jakaya M. Kikwete.
Ni mara nyingi kabla ya maradhi yake Mzee Majuto amekuwa akiomba kwa unyenyekevu apatiwe msaada wa Trekta ili aweze kufanya kilimo cha nguvu.. Aliamini kilimo kitamfaa katika nyakati zake za mwisho kwa maana sanaa haikumfaa vya kutosha.
Si mara moja au mbili alituma direct ombi lake kwa Rais aliye madarakani wakati huo JK aangalie uwezekano wa kumsaidia lakini mpaka anafikwa na mauti hilo halikuwezekana.
Kama Rais wa nchi na wasaidizi wake wameshindwa kusaidia hilo, wanajisikiaje leo wanapoenda kumuaga?
Nakumbuka alisema amesikia na atalifanyia kazi. Nilitarajia BASATA wangeangalia namna ya kutumia sanaa yake kumfanikishia lengo lake.
Hayo yangetokea, pengine mzee angeweza kumudu gharama za matibabu na kupunguza risk ya kufariki mapema. Pengine angekuwa na furaha akastaafu zake sanaa akala mema.. Pengine mambo yangekuwa tofauti.. Pengine, pengine..
Watanzania tuone aibu kwa hili na liwe funzo kwa yajayo.
Rest in Peace King Majuto.