Msiba wa King Majuto: Aibu yako Kikwete, aibu yetu Watanzania...

Taifa lipo msibani!

Ni msiba wa kitaifa kuondokewa na mfalme wa sanaa nchini, King Majuto. Hakuna haja ya maelezo mengi maana historia yake inajitetea!

Nimetazama nyakati za mwisho wakati anapambania uhai wake Tanzania na India. Pongezi kwa waliofanya jitihada za kumuwezesha kumudu gharama za matibabu ikiwemo Serikali na wadau wengine.

Kifo cha mzee wetu kimetuacha na aibu. Aibu zaidi kwa Rais Mstaafu wa JMT, Jakaya M. Kikwete.

Ni mara nyingi kabla ya maradhi yake Mzee Majuto amekuwa akiomba kwa unyenyekevu apatiwe msaada wa Trekta ili aweze kufanya kilimo cha nguvu.. Aliamini kilimo kitamfaa katika nyakati zake za mwisho kwa maana sanaa haikumfaa vya kutosha.

Si mara moja au mbili alituma direct ombi lake kwa Rais aliye madarakani wakati huo JK aangalie uwezekano wa kumsaidia lakini mpaka anafikwa na mauti hilo halikuwezekana.

Kama Rais wa nchi na wasaidizi wake wameshindwa kusaidia hilo, wanajisikiaje leo wanapoenda kumuaga?

Nakumbuka alisema amesikia na atalifanyia kazi. Nilitarajia BASATA wangeangalia namna ya kutumia sanaa yake kumfanikishia lengo lake.

Hayo yangetokea, pengine mzee angeweza kumudu gharama za matibabu na kupunguza risk ya kufariki mapema. Pengine angekuwa na furaha akastaafu zake sanaa akala mema.. Pengine mambo yangekuwa tofauti.. Pengine, pengine..

Watanzania tuone aibu kwa hili na liwe funzo kwa yajayo.

Rest in Peace King Majuto.
tenor(2).gif
 
Huu ndo ujinga wa watanzania. Badala ya kusema Kijiji flan kimeomba Trekta ili lisaidie shughuli za Kilimo katika Kijiji hicho unakuja hapa Kuzungumzia Majuto kuomba Trekta. We una akili kweli? Kwa style hiyo kila muigizaji akienda kuomba utakuaje? Majuto amefanya sana kazi pesa zake kapeleka wapi?tuacheni ujinga wa Bei Rahisi.
 
Kila mtu akiomba sasa itakuwaje mkuu!!!????
Wenye matatizo nchi ni wengi sn. Bora ht mzee alikuwa na sehemu ya kumuingizia kipato.
Acheni lawama. Juzi rais JPM kamsaidia mtu bajaji watu wamelaumu kwanini kampa wakati walemavu tz ni wengi sana.
Ila ndio bongo yetu
He was very special!
 
Hata Mimi nilishaomba baiskeli tu ili niendeleze biashara yangu ya nyanya badala ya Noah lakini mpaka leo bila bila,

Hakika lawama hizi ni zao kabisa.
 
Pambana na hali yako acha kuilaumu serikali , kila mtu akianza kudai apewe trekta itakuwaje .

R.I.P King Majuto
 
Kama kuna kitu watanzania wanakiweza vyema ni kukosoana na kuzodoana.
 
Yule mzee amefanya kazi ya maigizo kwa muda wote.

Kaingia mikataba.

Kafanya matangazo.

Kalamba deals na Al Riyami.

Kaonyeshwa Channel 10.

VHS na DVDs zimeuzwa.

Steps walikua naye.

Ana muvi alizoitwa kama mshiriki.

Unamlaumu Kikwete kwa kutotoa trekta?
Unatulaumu waTanzania?

Kuna waTz wangapi hawana jukwaa la kumlalamikia raisi?
Unaona Majuto anastahili kuliko watu wote?
Umeziangalia fursa alizowahi kua nazo?
Umemaliza kila kitu mkuu, mleta thread njoo uchukue jibu lako usepe
 
Yule mzee amefanya kazi ya maigizo kwa muda wote.

Kaingia mikataba.

Kafanya matangazo.

Kalamba deals na Al Riyami.

Kaonyeshwa Channel 10.

VHS na DVDs zimeuzwa.

Steps walikua naye.

Ana muvi alizoitwa kama mshiriki.

Unamlaumu Kikwete kwa kutotoa trekta?
Unatulaumu waTanzania?

Kuna waTz wangapi hawana jukwaa la kumlalamikia raisi?
Unaona Majuto anastahili kuliko watu wote?
Umeziangalia fursa alizowahi kua nazo?

Ndugu naomba nitoe povu, tena la kiwango cha grisi. Hivi una uhakika kuwa mikataba aliyoingia, hela ilikuwa inaingia kwake? na alikuwa anapokea hela sahihi kulingana na kazi yake?
 
Taifa lipo msibani!

Ni msiba wa kitaifa kuondokewa na mfalme wa sanaa nchini, King Majuto. Hakuna haja ya maelezo mengi maana historia yake inajitetea!

Nimetazama nyakati za mwisho wakati anapambania uhai wake Tanzania na India. Pongezi kwa waliofanya jitihada za kumuwezesha kumudu gharama za matibabu ikiwemo Serikali na wadau wengine.

Kifo cha mzee wetu kimetuacha na aibu. Aibu zaidi kwa Rais Mstaafu wa JMT, Jakaya M. Kikwete.

Ni mara nyingi kabla ya maradhi yake Mzee Majuto amekuwa akiomba kwa unyenyekevu apatiwe msaada wa Trekta ili aweze kufanya kilimo cha nguvu.. Aliamini kilimo kitamfaa katika nyakati zake za mwisho kwa maana sanaa haikumfaa vya kutosha.

Si mara moja au mbili alituma direct ombi lake kwa Rais aliye madarakani wakati huo JK aangalie uwezekano wa kumsaidia lakini mpaka anafikwa na mauti hilo halikuwezekana.

Kama Rais wa nchi na wasaidizi wake wameshindwa kusaidia hilo, wanajisikiaje leo wanapoenda kumuaga?

Nakumbuka alisema amesikia na atalifanyia kazi. Nilitarajia BASATA wangeangalia namna ya kutumia sanaa yake kumfanikishia lengo lake.

Hayo yangetokea, pengine mzee angeweza kumudu gharama za matibabu na kupunguza risk ya kufariki mapema. Pengine angekuwa na furaha akastaafu zake sanaa akala mema.. Pengine mambo yangekuwa tofauti.. Pengine, pengine..

Watanzania tuone aibu kwa hili na liwe funzo kwa yajayo.

Rest in Peace King Majuto.
PUMBA
 
Back
Top Bottom