Msiba kwenye pombe au pombe msibani

Msiba kwenye pombe au pombe msibani

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2012
Posts
3,036
Reaction score
8,394
Awali yalipoletwa makufuli hakuna aliyedhani ndani ya nyumba kulikuwa na ulevi tena chupa kubwa ilionekana waziwazi ikiwa na neno pombe. Yamkini kumeremeta na upya wa yale makufuli uliwasahaulisha watu habari ya kileo.

Kadiri muda ulivyosogea harufu ya pombe ilianza kuwa dhahiri, na baadhi ya watu wakaanza kulewa. Wenye mioyo makini wakaanza kutafuta suluhu, maana Kadiri siku zinavyosonga maisha ya kesho kwa wengi ni majaliwa.

Hata walio tulia kwa job, wawe mameneja au Makonda wote hawana hakika na kesho yao. Wanakula na kusaza sasa na huku wakiomba ulevi wao usiwazidi kimo watu wakavunjilia mbali kufuli la mlango.

Fikiria starehe zikiwazidia na pombe inavyozidi kuwalevya si kuna hatari ya mlango kuvunjwa. Maana walioko nje wana ghadhabu kubwa.

Hata hivyo huu msiba umekuwa changamoto kubwa tena, ni kama unazidi kuwachanganya waliochoshwa na ulevi. Mambosasa yanazidi kuwa magumu.

Tangu tundu litokee mwakajana, hakujawa na dalili za kuziba. Yaelekea pombe ni kali sana._

Yuko mwalimu alijaribu kufundisha lakini wapi somo halikueleweka. Nadhani alikuwa kwenye mada ya demokrasia lakini alikuwa hajaingia mle ndani mle ndani waliamua iwe siku ya maulid kwa hiyo mwalimu alipoteza muda na maandalizi yake bure kabisa.

Hivi ninavyokusimulia nje kabisa tena mbali kuna mwalimu wa tuisheni wa hisabati, baada ya kuambiwa na kushuhudia namna wananchi walivyo mahiri kwenye kusoma namba, yeye kaja na namba ya kutujaribu. Namba hii imewachanganya mpaka waliomo ndani. Nao wanapaza sauti wanasoma mwalimu anavyotaka. Hata ulevi umetulia wanamfuata mwalimu. Kila kona sasa ni 26042018. Viranja wengi wamejitokeza kumsaidia mwalimu wa hesabu. Wamecharuka utadhani wameng'atwa na ma-nge, wale wadudu wenye sumu

Ukiikosea kutamka unakula fimbo tena na wale waliongia ndani....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom