mshukiwa2

mshukiwa2

mtafuta-maisha

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2016
Posts
1,982
Reaction score
2,934
anaanzia hapa Alikaa gerezani miaka 20 akisubiri kunyongwa kwa mauaji ambayo hakuhusika.

Akiwa gerezani kwa muda huo wote Skinner alikuwa akiendelea kushikiria msimamo wake kuwa siyo yeye aliyetenda kosa hilo la mauaji. Alizidi kudai mpenzi wake Twila na Watoto wake wanastahili kupata haki kwa polisi kumkamata na kumfikisha kwenye vyombo vya dola muaji halisi ambaye huenda yuko mtaani akiwa huru anaendela na maisha yake huku yeye akiwa jera akishubiri kunyongwa kwa kosa ambalo hakulitenda.

Lakini waliokuwa majirani zake huko Pampa Texas wao walikuwa wanaamini kwamba haki ilitendeka na Skinner ndiye alikuwa mhusika wa mauaji hayo na kwa sasa alikuwa gerezani akisubiria kunyongwa. Mtu yeyeote angeenda sehemu yoyote katika mji wa Pampa akauliza watu mnawaza nini kuhusu hukumu ya Skinner, watu wangejibu kwamba inafaa awe amenyongwa kabisa wanamchelewesha.

Akiwa anasubiria kunyongwa, ilikuwa imepita miaka mitano toka hukumu yake imetoka, na mwaka 2000 kundi la wanafunzi wa kitovu cha Uandishi wa habari za kiuchunguzi katika Chuo Kikuu cha Nerthurstern walianza kupitia kesi ya Skinner kama mojawapo ya mazoezi katika masomo yao. Emily Probist Miller ambaye alikuwa mkufunzi wa masuala ya kiupelelezi kwa wanafunzi wao akishirikia na Profesa aliyejulikana kama Protass. Ikatokea nafasi kwa Emily kwenda katika Jimbo la Texas kwenye gereza linaloshikiria wafungwa waliohukumiwakunyongwa ili akamfanyie mahojiano Skinner. Yeye kama mwandishi wa habari za kiupelelezi hii ilikuwa ni nafasi ambayo asingeweza kuacha ipite.

Emily aliwatuma wanafunzi wake wamtafute aliyekuwa mpenzi wa Skinner Bi Leed ambaye kwa muda huu alikuwa amebadilisha kwa kupinga ushahidi alioutoa dhidi ya Skinner wakati wa kesi. Wanafunzi walimtafuta na kufanikiwa kumpata kasha walifanya mahojiano naye. Kitabia alikuwa mwanamama mtata sana ambaye alikuwa anakasirika haraka na ndani mwake alikuwa akiishi na nyoka.

Sharti alilowapa ni kwamba asirekodiwe kwa video au kupigwa picha bali alikodiwe sauti tu. Haya chini ni mahojiano yake baina yake na wanafunzi wa Emily.

Mwanafunzi: Uliwambia polisi, na kutoa ushahidi mahakamani kuwa Skinner alikuja mwenyewe hapa, na alipokuja ulienda uani kuwatazama watoto wako. Je ni kweli?

Leed: Hapana. Askari walikuwa walikuwa wananitisha, na kunifanya nijihisi kama ninajaribu kumlinda Skinner, na kama ningeendelaa kumtetea ningeweza kufungwa pia.

Mwanafunzi: Je ni kweli kwamba Skinner alithibitisha kwako kuwa alimuua Twila na watoto wake wakiume wawili?

Leed: Hapana hakuwahi.

Mwanafunzi: Hivyo una maana kwamba alikuelezea juu ya kutenda kwake jambo flani, lakini wewe hukuamini kama alikuwa anakiri juu ya kuhusika kwake kwenye mauaji?

Leed: Hapana

Wakati wa kesi, waendesha mashitaka alimchukua Andrea Leed wakampandisha ndege mpka Fort Worth na kumpangia chumba kwenye hoteli. Leed anadai kwamba alikuwa kama kawekwa kwenye kifungo cha nyumbani.

Emily anasema kwamba aliona kiapo alichokula Leed mwaka 1997, Leed anadai kwamba alikuwa akitishiwa na polisi na kujiona kama mfungwa na alianza kupata wasiwasi kuwa huenda na yeye wanaweza kumtafutia ushahidi utakaomweka pia katika eneo la tukio hivyo aliamua kukubari kufanya kile askari watakachotaka.

Emily akiwa kwenye gereza la wafungwa wanaosubiri kunyongwa, Skinner aliletwa kwa ajili ya kufanya naye mahojiano na anakumbuka kitu cha kwanza alichomwambia Emily ni kwamba hahusiki namauaji yale. Alimwambia angependa dunia ijue kuwa yeye siyo mhusika kwasababu failia ya marehemu wanaumia sana kwasababu ya kilichotkea na mtuhumiwa halisi yuko mtaani. Aliendela kusema kuwa hakukuwa na sababu yoyote ya yeye kumuua Twila na wanaye kwakuwa alikuwa anampenda sana Twila kuliko kitu chochote dunia hii. Emily anadai katika kuzngumza naye Skinner alimwambia kuna mshukiwa mwingine ambaye polisi hawakumfuatilia na anaitwa Robert Donnell.

Robert Donnell aliwahi kufungwa kwa kosa la wizi, uporaji na kudhuru watu. Alikuwa ni mjomba wake Twila na watu wengi walikuwa wakimwita kama Uncle Bob. Skinner anadai alikuwa ana tabia ya kuja nyumbani kwa Twila na kumyeshwa pombe kasha Twila akishalewa alikuwa anajaribu kumwingilia kinyume na maumbile. Jopo la wanasheria waliokuwa wakimtetea Skinner walimwambia Emily pia kuwa walimwingiza Donnel kwenye kesi kama mshukiwa ambaye anaweza kuwa alihusika kwenye mauji hayo badala ya Skinner kutokana na maelezo ya Skinner kuwa aliwahi kumkuta Donnel akiwa anajaribu kumbaka Twila ndipo yeye akaingia ndani ghafla. Hili tukio lilitokea wiki kadhaa kabla ya mauaji hayo.

Skinner anadai kwamba alimkuta Donnell akiwa kamfunga kamba Twila huku akiwa katika harakati za kumuingilia nyuma huku Twila akiwa anajaribu kujitetea, Donnell akawa anamambia akileta vurugu atamuua. Skinner anadai alimvamia Donnell akampiga kasha kumburuza na kumwingiza kwenye gari lake na kumwamuru aondoke na asirudi hapo kamwe. Anasema kuwa hawakutoa taarifa polisi kwakuwa lilikuwa tukio la aibu ukizingatia yule alikuwa ndugu wa damu kwa Twila hivyo waliamua kuwa hawatolizungumzia.

Wanafunzi wa Emily, waliafanya kazi ya kutafuta mashahidi wanaoweza kuthibitisha madai haya ya Skinner na wanafanikiwa kumpata mwanamama Vicki Treat ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa Twila. Vicki anadai kuwa anamfahamu Uncle Bob kama mjomba wake Twila na anadai walikuwa wakifanya ngono mra kwa mara na Twila alipoamua kuacha kufanya ngono naye Uncle Bob mara kadhaa alijaribu kumbaka. Na alidai kwamba Twila mwenyewe aliwahi kumwambia mara kadhaa kuwa Uncle Bob amejaribu kumbaka. Pia anadai kwa upande wake anahisi ni Uncle Bob aliyeua ile familia kwakuwa alikuwa anaona wivu Skinner kuishi pale nyumbani kwa Twila.

Katika mahojiano ambayo Emily alifanya na baadhi ya watu waliomuona Skinner usiku ule wa mauaji, wote hawaamini kama Skinner alitenda mauaji yale kwa jinsi alivyokuwa kalewa na hajiwezi. Howard Mitchell ambaye alikwua ni rafiki yake Twila anadai kwamba yeye alipita kwa Twila kusalimia usiku huo na alimuona Skinner akiwa kalala kwenye kiti hajitambua anakoroma tu akiwa kasinzia na ananuka pombe.

Wakati Skinner akiwa kalala pale kwenye kiti, Twila aliondoka na gari kuelekea kwenye tafrija ya kusubiri mwaka mpya ambapo kwenye tafrija hiyo Uncle Bob alikuwepo. Mtoto wa wa kike wa Horwad Mitchell ajulikanaye kama Sarah alikuwa kwenye hiyo tafrija pamoja na Twila na Uncle Bob.

Haya ni mahojiano aliyofanyiwa na wanafunzi wake Emily

Mwanafunzi: Je uliona jambo lolote la ajabu baina ya Uncle Bob na Twila usiku huo?

Saraha: Ndiyo, Uncle Bob alikuwa akimfuata fuata Twila kila mahali akimghasighasi, pia alikuwa hatakiazungumze na wanaume na alikuwa akifanya vitu vya ajabu ambavyo hakupashwa kufanya. Pia alikuwa akijaridbu kuanzisha mazungumzo ya kingono na Twila.

Twila na Uncle Bob walikuwa sehehmu moja muda mfupi kabla ya mauaji hayo kutokea, na shuhuda andai alikuwa akimghasighsi na kumsumbua. Jambo hili lilihitaji kufanyia upelelezi na polisi lakini hawakufanya hivyo.

Wakiwa sasa wamepata sababu za kufikiria kuwa huenda Uncle Bob ndiye mhusika wa mauaji hayo, Emily na wanafunzi wake sasa wanakaribia kugundua kuwa kulikuwa an ushahidi unaonyesha uwepo wa Uncle Bob katika eneo mauaji yalipotokea.

Itaendelea bonyeza link hapo chini kusoma sehemu ya tatu
Earn money on short links. Make short links and earn the biggest money - shorte.st
 
Ipo poa sana...

Nimesoma sehemu ya kwanza na ya pili...

Inafikirisha sana...


Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom