Mshtakiwa akimbia kizimbani

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Mshtakiwa akimbia kizimbani


na Walter Mguluchuma, Mpanda


amka2.gif
GEORGE Simoni (24), mkazi wa mtaa wa Kigamboni, Wilaya ya Mpanda anayetuhumiwa kwa kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha, ametimka kizimbani mbele ya hakimu mkazi wa Wilaya ya Mpanda Dezidel Magezi baada ya kunyimwa dhamana na mahakama.
Tukio la kukimbia kizimbani kwa George limetokea jana majira ya saa 7:20 mchana baada ya hakimu kukataa ombi la mshtakiwa la kutaka dhamana.
Hakimu Magezi alimwambia mshtakiwa kuwa kesi iliyokuwa inamkabili kwa mujibu wa sheria haina dhamana hivyo mshtakiwa alitakiwa kwenda mahabusu hadi Januari 30 ndipo kesi hiyo ingetajwa tena.
Baada ya kuambiwa hivyo mshtakiwa aliamua kukimbia mbio akitokea kizimbani hali iliyomfanya mwendesha mashtaka wa polisi (ASP) Magnusi Milinga pamoja na polisi waanze kumfukuza kwa mbio mshtakiwa huyo.
Hata polisi walipoamua kupiga risasi mbili hewani, mshtakiwa aliendelea kukimbia tu, hali iliyowafanya wanafunzi wa Shule ya Kashaulili na Mwangaza watoke madarasani na kuweza kumzingira mashtakiwa na polisi kumkamata.
Mshtakiwa huyo anatarajiwa tena kufikishwa mahakamani leo, kujibu shtaka la kutoroka chini ya ulinzi halali wa polisi.
Ilielezwa kuwa awali mshtakiwa huyo alimpora kwa kutumia silaha mfanyabiashara wa duka Julius Kasangae mnano Desemba 30, 2010 katika mtaa wa Kigamboni majira ya saa 8 usiku.
Vitu anavyodaiwa kuvipora mshtakiwa ni baiskeli, mito ya makochi, mabati, mafuta ya kula, sukari vyote vikiwa na thamani ya sh 500,000.



h.sep3.gif

 
Back
Top Bottom