Elections 2020 Mshituko: Wananchi Kigoma mjini wamtaka Prof. Joyce Ndalichako

Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
3,799
2,000
Habarini wana jukuwaa.

Taarifa za kushitusha ni kwamba huenda kwenye bunge lijalo (2020 -2025) mbunge aliyefukuzwa chadema na Tundu Lisu mh Zito Kabwe asionekane tena! , hii ni kufuatia wananchi wa Kigoma kumchoka kwani hatimizi ahadi yoyote jimboni ,kazi yake ni kushinda mitandaoni akifyatua uzushi na uongo wa kila aina.

Badala ya kuwatumikia wapiga kura wake yeye ameenda kuungana na watesi wake akina Lisu na Mbowe na kuanza kuishutumu serikali kwa kupinga miradi yenye tija kwa wananchi masikini kama ujenzi wa viwanda na bwawa la pili kwa ukubwa barani Afrika litakalotumika kufua umeme.

Baada ya wana Kigoma kugundua hilo wameamua kuungana na kwenda kumshawishi waziri wa elimu Joyce Ndalichako ili agombee jimbo la Kigoma mjini uchaguzi ujao wa 2020.

Kila laheri Prof Ndalichako ushinde hilo jimbo ili kupunguza wanafiki na wasaliti wa nchi yetu bungeni , itapendeza zaidi na Lisu akishindwa jimboni kwake. Hawa wasaliti wanatakiwa wakalime nyanya vijijini mwao badala ya sasa wanatumia mishahara tunayowalipa kwa kodi zetu kwenda kutusaliti kwa kutoa siri za nchi yetu kwa wazungu.​

Sent using Jamii Forums mobile app
 

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,012
2,000
nilitaka nikutukane tusi baya wewe mleta mada basi nimeogopa mods wangenishukia kama mwewe, lakini huu ulioleta ni uhalo mtupu. Kuna majimbo kama Mtera mbunge weke anashinda humo jimboni yana nini? ZAIDI WANANCHI WAKE WALIWAUWA WALE WANASAYANSI WA SERIAN KWA IMANI ZA KIJINGA.
 
Top Bottom