Mshituko: Hotuba za hayati Magufuli zinaweza kuja kutumika kuiondoa CCM madarakani

Kwani unatakaje?
Si habari ya ninavyotaka mimi.

Kimantiki uchumi unafuata nguvu za soko, nguvu za urari wa utengenezwaji, upatikanaji, usambazaji na mahitaji ya kitu.

Hizi nguvu (supply and demand) ndizo zinapanga bei, zinapanga ushindani, zinapanga ufanisi.

Ukimpa kazi ya kuzalisha, kusambaza umeme mtu mmoja tu, hana mshindani. Ana uhakika na soko, anaweza hata kupanga bei.

Atapataje motisha ya kufanya vizuri zaidi wakati hana mpinzani na watu ni lazima wanunue kwake tu?

Jibu hapo ni kufungua soko, waje wapinzani wengi kupambana naye.

TANESCO wanazingua na umeme wao? Aaah, tunahama tunakwenda kwenye kampuni nyingine ya umeme ambayo umeme wake ni wa uhakika zaidi.

Kungekuwa na mfumo huo, hata kama tusingekuwa na mfumo usio matatizo, tungemaliza ukiritimba na matatizo yanayotokana na monopoly.

Kwa sasa hata mtu ukiwa na mtambo wako wa solar wa kuhudumia umeme kijiji tu, lazima uwekewe undava na TANESCO.
 
Si habari ya ninavyotaka mimi.

Kimantiki uchumi unafuata nguvu za soko, nguvu za urari wa utengenezwaji, upatikanaji, usambazaji na mahitaji ya kitu.

Hizi nguvu (supply and demand) ndizo zinapanga bei, zinapanga ushindani, zinapanga ufanisi.

Ukimpa kazi ya kuzalisha, kusambaza umeme mtu mmoja tu, hana mshindani. Ana uhakika na soko, anaweza hata kupanga bei.

Atapataje motisha ya kufanya vizuri zaidi wakati hana mpinzani na watu ni lazima wanunue kwake tu?

Jibu hapo ni kufungua soko, waje wapinzani wengi kupambana naye.

TANESCO wanazingua na umeme wao? Aaah, tunahama tunakwenda kwenye kampuni nyingine ya umeme ambayo umeme wake ni wa uhakika zaidi.

Kungekuwa na mfumo huo, hata kama tusingekuwa na mfumo usio matatizo, tungemaliza ukiritimba na matatizo yanayotokana na monopoly.

Kwa sasa hata mtu ukiwa na mtambo wako wa solar wa kuhudumia umeme kijiji tu, lazima uwekewe undava na TANESCO.

Bado una imani kuwa Tanzania inaweza kuwa “rational environment” kiasi hicho?
 
Bado una imani kuwa Tanzania inaweza kuwa “rational environment” kiasi hicho?
Si suala la imani tu.

Ni suala la kufanya kazi ngazi kwa ngazi kubadilisha.

Kwa sababu ukichunguza vizuri hakuna sehemu iliyo "rational environment" duniani. You always have contradictions and idiosyncracies. In fact, without these cobtradictions, imperfections and idiosyncracies, the universe would not exist. If you look at entropy and the second law of thermodynamics, quantum physics, Godel's Incompleteness Theorems, they are always and insecapably there.

Hata huko kwenye soko huria nako kuna changamoto zake tunazotakiwa tuzijue ili tuweze kuzi regulate.

Kwa hivyo kila mfumo utahitaji watu waufanyie kazi kuuboresha.

Watu wachukue ownership. Consumer advocacy iongezeke.

Uwezekno au kutowezekana kwa Tanzania kuwa "rational environment" kiasi hicho cha kufanya umeme uwe wa uhakika ni suala lililo katika uamuzi wa Watanzania. Halipo nje ya uamuzi wao.

Swali ni, je, Watanzania wanataka hilo?

Au wameridhika wanasema "kula ugali wako ukalale" ?
 
Mshituko mkubwa nimeupata baada ya kugundua kuwa watanzania wengi wamezitunza video mbalimbali za hayati Magufuli kama reference na kipimo cha kupima utendaji wa serikali iliyopo madarakani na serikali zitazokuja.

Kiongozi yoyote sasa hivi akitoa visingizio kwamba jambo fulani haliwezekani kufanyika watanzania wanamjibu kwa kumuwekea video za Magufuli na kumuuliza mbona kipindi cha hayati Magufuli hilo jambo liliwezekana?

Alianza waziri wa nishati January Makamba kuwadanganya watanzania kuwa mgao wa umeme unaotikisa nchi kwa sasa unatokana na awamu ya tano kuzuia maintanance baada ya hayati Magufuli kusema hataki kusikia mgao wa umeme na hivyo vifaa kupata uchakavu uliosababishwa na kuwaka mfululizo kwa miaka 5.

Kabla ya uongo wake haujakauka watanzania walimshushia video za Magufuli akianika uozo na mbinu chafu za watendaji wa Tanesco kuhongwa pesa na kufungulia maji ili baadhi ya wafanyabuashara wasio waaminifu wauze jenerata zao!

Ghafla TANESCO wsmebadilika tena na kusesema mgao wa umeme unasababishwa na kupungua kwa maji kwenye mabwawa na siyo regular maintanance iliyosemwa na Makamba.

Kwenye mkumbo wa kusema uongo hadharani ameingia pia waziri wa uwekezaji Godfrey Mwambe baada ya kuwadanganya watanzania kuwa hakuna mkataba wowote uliowahi kusainiwa kuhusu ujenzi wa bandari ya Bagamoyo na akaonyesha kushangaa hayati Magufuli aliyatoa wapi hayo maneno!

Mwambe bila kujali onyo la wahenga linalotaka kuogopa Mungu na technologia akasahau kuwa kuna video ikionyesha rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete akiweka jiwe la msingi ujenzi wa bandari ya Bagamoyo!

Je, jiwe la msingi huwa linawekwa bila mkataba wowote? Hata mtaani mama ntilie, bodaboda, wachimbaji wadogo machinga mara kwa mara wamekuwa wakirejea hotuba za Magufuli zilizokuwa zinasisitiza kuwa sera za CCM lazima ziegemee kuwalinda wanyonge ili nao watajirike na siyo kuwafukuza na kuwanyanyasa.

Ninavyoona mbele ya safari kuna hatari ya hotuba mbalimbali za hayati rais Magufuli kutumiwa na wananchi kuibana serikali kutakakosababisha CCM kuondolewa madarakani.

Kwenye kizazi hiki CCM wana njia moja tu ya kupona nayo ni kufanya kazi zaidi kuliko hayati Magufuli na siyo kufanya kazi chini ya kiwango huku wakitoa visingizio mbalimbali.
Kwa hicho kichwa cha habari sina haja ya kusoma kilichopo ndani maana
ccm ilishatoka madarakani miaka mingi kwa sasa ipo hapo kwa nguvu za dola ambao nao wanapigika
 
Mfano mtu apige hela ya madawa au vifaa tiba kwenye hospital zetu watu wakose huduma matokeo yake ni nini kama sio kuua usiwe na mawazo robo kilomita.
Muuaji lazima atakuwa fisadi pia, maana lengo la kuua wanaokukosoa ni ili iweje kama sio kuiba?
 
Ni kweli ccm wanatakiwa kufanya kazi sana, kwa kiwango, au hata kumzidi hayati Magufuli, kama wanataka waendelee kuonekana relevant kwa wananchi. Kumtumia Magufuli as a scapegoat ya utendaji mbovu haitawasaidia.

Hilo la kuondolewa madarakani kwa sasa ni gumu kwa sababu hakuna chama mbadala. Ingekuwa chadema bado ina nguvu kama enzi zile za Dr Slaa, ccm wangepata tabu sana

Kwa sasa hivi labda wananchi waamue kuchagua chochote tu kisichokuwa CCM bila kujali athari zake ndo hilo litawezekana.
Kiongozi wewe upo wapi? Mbona inapigwa tu mieleka kama kumsukuma mlevi!!!! Mpaka goli la mkono limefeli, sasa wanatumia Taasisi zenyewe kuwepo hapo walipo, yaani wako kama pete na chanda na Taasisi hizo bila hivyo watatoweka mazima.
 
Back
Top Bottom