Kinuju
JF-Expert Member
- Mar 20, 2021
- 2,390
- 5,310
Mshituko mkubwa nimeupata baada ya kugundua kuwa watanzania wengi wamezitunza video mbalimbali za hayati Magufuli kama reference na kipimo cha kupima utendaji wa serikali iliyopo madarakani na serikali zitazokuja.
Kiongozi yoyote sasa hivi akitoa visingizio kwamba jambo fulani haliwezekani kufanyika watanzania wanamjibu kwa kumuwekea video za Magufuli na kumuuliza mbona kipindi cha hayati Magufuli hilo jambo liliwezekana?
Alianza waziri wa nishati January Makamba kuwadanganya watanzania kuwa mgao wa umeme unaotikisa nchi kwa sasa unatokana na awamu ya tano kuzuia maintanance baada ya hayati Magufuli kusema hataki kusikia mgao wa umeme na hivyo vifaa kupata uchakavu uliosababishwa na kuwaka mfululizo kwa miaka 5.
Kabla ya uongo wake haujakauka watanzania walimshushia video za Magufuli akianika uozo na mbinu chafu za watendaji wa Tanesco kuhongwa pesa na kufungulia maji ili baadhi ya wafanyabuashara wasio waaminifu wauze jenerata zao!
Ghafla TANESCO wsmebadilika tena na kusesema mgao wa umeme unasababishwa na kupungua kwa maji kwenye mabwawa na siyo regular maintanance iliyosemwa na Makamba.
Kwenye mkumbo wa kusema uongo hadharani ameingia pia waziri wa uwekezaji Godfrey Mwambe baada ya kuwadanganya watanzania kuwa hakuna mkataba wowote uliowahi kusainiwa kuhusu ujenzi wa bandari ya Bagamoyo na akaonyesha kushangaa hayati Magufuli aliyatoa wapi hayo maneno!
Mwambe bila kujali onyo la wahenga linalotaka kuogopa Mungu na technologia akasahau kuwa kuna video ikionyesha rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete akiweka jiwe la msingi ujenzi wa bandari ya Bagamoyo!
Je, jiwe la msingi huwa linawekwa bila mkataba wowote? Hata mtaani mama ntilie, bodaboda, wachimbaji wadogo machinga mara kwa mara wamekuwa wakirejea hotuba za Magufuli zilizokuwa zinasisitiza kuwa sera za CCM lazima ziegemee kuwalinda wanyonge ili nao watajirike na siyo kuwafukuza na kuwanyanyasa.
Ninavyoona mbele ya safari kuna hatari ya hotuba mbalimbali za hayati rais Magufuli kutumiwa na wananchi kuibana serikali kutakakosababisha CCM kuondolewa madarakani.
Kwenye kizazi hiki CCM wana njia moja tu ya kupona nayo ni kufanya kazi zaidi kuliko hayati Magufuli na siyo kufanya kazi chini ya kiwango huku wakitoa visingizio mbalimbali.