Mshitakiwa

Nape Nnauye

MP Mtama
Joined
Dec 26, 2012
Posts
99
Reaction score
408
(makala hii imeandikwa na Dr. Mohammed Seif Khatibu)

MWAKA 1984, mkoani Dodoma ndani ya ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kulikuwepo kesi kubwa. Kesi ya kiongozi wa juu wa serikali ya Zanzibar. Alishitakiwa kwa kosa la kwenda kinyume cha Òhati za MuunganoÓ uliosainiwa na Abeid Amani Karume na Julius Nyerere.

Mtuhumiwa, Rais wa Zanzibar, hakuwahi kujiandaa vyema na kufikisha hoja yake mbele ya mamlaka ya Chama chake. Marafiki zake wa karibu walimuendea kinyume na kuiba waraka muhimu wa mashitaka katika shubaka la Ikulu.

Bila shaka wale waliohusika walifanya wizi huu kwa siri kubwa kwani waraka wenyewe uliibiwa na kutolewa nakala na kurejeshwa ulipochukuliwa bila wahusika kujulikana. Waraka huo ukapelekwa Butiama kwa Mwalimu kwa ndege ya kukodi.

Njama hizo za kumwangamiza na kumtosa kiongozi huyo wa Zanzibar katika majanga ilikuwa ajali kubwa ya kisiasa na ya kihistoria kutokea katika taifa letu. Mipango ikapangwa kesi ikadhihirishwa katika kikao cha Chama na kuwa kama mahakama. Mshitakiwa ni Rais wa Zanzibar. Akasomewa mashitaka yake yote mbele ya viongozi wenzake katika ukumbi wa Chuo cha CBE huko Dodoma.

Mwendesha mashitaka dhidi ya Rais wa Zanzibar alijitokeza kwa haraka na kuona kama vile amepata bahati ya pekee. Sio mwingine ila alikuwa Maalim Seif. Akasimama kidete mbele ya hadhara na kuelezea kwa nini kiongozi huyo wa Zanzibar amefanya kosa na dhambi kubwa ya kutaka kuubadilisha muundo wa Muungano badala ya kuwa wa serikali mbili alitaka uwe wa serikali tatu kinyume na sera za Chama.

Mwendesha mashitaka huyu kwa jasiri alijenga hoja zake za kutosha za kuonesha uzuri wa Muungano, tija ya Muungano wa Serikali mbili na kwa nini kiongozi huyo wa juu wa Zanzibar inapaswa achukuliwe hatua kali sana bila huruma!

Mwendesha mashitaka huyo akaungwa mkono sana na wafuasi wake akiwamo marehemu Shaaban Mloo. Mwendesha mashitaka huyo baadaye ikaonekana kuwa yeye ndiye aliyehusika mapema kuiba waraka huo katika shubaka au suraka ya huko Ikulu.
Hivyo, basi alifanya kazi mbili za kuiba waraka na kumkabidhi Nyerere na kusimama kama mwendesha mashitaka namba moja dhidi ya Rais wake huyo. Mshitakiwa, Rais wa Zanzibar, kwa unyonge alikubali adhabu ya kujiuzulu kwa nafasi zake zote tatu. urais wa Zanzibar, makamu wa rais wa Tanzania na umakamu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi.

Hakuruhusiwa kuishi Zanzibar. Viongozi wenzake wa karibu, wote wakafuata nyayo zake za kujiuzulu akiwemo waziri kiongozi wake. Viongozi wake waandamizi wakawekwa katika vifungo vya nyumbani katika mikoa kadhaa ya Tanzania Bara.

Matokeo yote hayo, mabaya kwa Rais wa Zanzibar na wenzake ni kazi ÒnzuriÓ ya kuiba nyaraka Ikulu na kusimamia kidete Mwendesha Mashitaka huyu stadi, bingwa, mahiri na jasiri - Maalim Seif. Ni bahati mbaya kuwa mwendesha mashitaka huyo ni mwanafunzi wa mshitakiwa katika Chuo cha Lumumba.

Pia ni bahati mbaya mwendesha mashitaka alipewa nafasi ya masomo ya kwenda kusoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mshitakiwa. Ni bahati mbaya mwendesha mashitaka huyu alipewa kazi serikalini baada ya masomo na kumwingiza katika siasa na yeye mshitakiwa pia hata kufika nafasi aliyonayo sasa.

Hiyo ndio fadhila yake? Hiyo ndio ahsante yake? Ni bahati mbaya kuwa mwendesha mashitaka hivi sasa hayupo kizimbani kwa kutenda kosa na dhambi ileile aliyoifanya Rais wa Zanzibar aliyejiuzulu.

Mwendesha mashitaka huyu aliyetetea Muungano wa serikali mbili kwa uchungu na hoja, leo amegeuka. Huyo ndiye leo anaongea hadharani kuwa sio tu anakataa serikali mbili bali anataka Muungano huo adhimu uliomfikisha leo hapo alipo uvunjwe kabisa.

Yeye kama kiongozi wa juu na mtendaji mkuu wa chama chake anakwenda kinyume pia na sera ya Chama chake ya Muungano wa serikali tatu.

Hivi mwendesha mashitaka huyu wa kesi kama hii kwa nini na yeye asishitakiwe na chama chake? Uadilifu wake uko wapi? Ukweli wake uko wapi? Sheria si msumeno? Unafiki na uzandiki umemtawala. Mwendesha mashitaka ni mshitakiwa, afikishwe kizimbani. Anayo kesi ya kujibu.
 
Nape Nnauye bhana haishi vituko, haya mkuu tumesoma makala! kuna lingine tena??????
 
Last edited by a moderator:

Naona bwana Nape baada ya kupewa ulaji kelele zote za uanaharakati zimeisha sasa umebaki kushabikia siasa za maji taka....vipi ulhairisha kuihama nchi....nape kuna watu wanakufahamu zaidi ya unavyojifahamu na unafiki wako kwenye siasa.....hapo unamaanisha nini..mwenezi wangu?
 
It's Nape again......!
 
mimi wala sisomi thread za watu wanaombikizia watu kesi za uongo,..to hell!!!
 
sioni kosa la mshitakiwa, alikuwa bado kijana - wanasiasa vijana wanapita katika majaribu mengi hata huyu mleta hii sredi pia yumo majaribuni.
 

Hana tofauti na Yuda Iskarioti, alisema "Yule nitakaye msalimia kwa kumbusu ndiye Yesu mkamateni"

Maalim Seif Sharif Hamad anahasira kwani alitarajia kwamba Mwl angemteua yeye kuwa Rais wa Zanzibar kwa kufanya kazi nzuri ya unafiki. Kumbe principles za Mwl ni kwamba "huyu aliyemsaliti mwenzie leo, kesho atakusaliti wewe"
 
Maalim Seif anajua anataka nini kwa sasa. Zanzibar irudi 10.12.1963 period. Amani Abeid Amani Karume naye anataka nchi irudi ujombani. Yeye si mtoto halisi wa Abeid Amani Karume. Hana cha kupoteza kwa sasa.

Amesahau kabisa alivyoupata Urais wa Zanzibar kwa kusaidiwa sana na muundo huu wa serikali mbili.
 
Sawa mkuu tumejifunza kutoka kwako,endelea kutukumbusha na hata kutufundisha mambo nyeti yanayohusu historia ya taifa letu
 
Mheshimiwa @Napennauye ,asante kwa kutukumbusha jambo muhimu na la kihistoria,miaka hiyo wengine wetu tulikuwa bado wadogo kujua kinachoendelea nchini(Ukiwemo wewe mheshimiwa),hata hivyo tumezikuta historia njiani,na nyingine zikiwa si kamilifu,na watu kama wewe wanasaidia kuainisha mapungufu ya historia(kama watakuwa wazalendo kweli)hata hivyo mh hii uliyoletaa hapa inaendelea kubaki kwenye mstari wa historia tu,ni kitu sahihi(au kinyume chake)kilichofanyika/chotokea kwa wakati sahihi kulingana na mazingira sahihi(or otherwise) mifumo mingi ya kiutawala hiko static kihivyo mh nape,kuna wakati ambapo tuliihitaji katiba hii tuliyonayo kuliko wakati mwingine wowote,kuna walioapa kuilinda na kuitetea (kama mh warioba ,kikwete &co)kuna pia waliostahili kwenda jela kipindi hicho kwa kujaribu kuweka fikra zao(njema au mbaya)juu ya katiba yetu tukufu,tulikuwa na Azimio la Arusha mh nape! Unaajua lilipo leo? je kuliundwa tume ya kukusanya maoni juu ya uvunjwaji wa azimio hilo? Je utakuwa tayari kumvisha kitanzi yeyote atakayebainika kulinajisi n kuliua azimio letu tukufu? Kama mh Kambona angelikuwako leo je ile dhambi aliyotupiwa wakati ule ingeendelea kuhuishwa na kustahili adhabu ile ile ya wakati huo?mhaini wa wakati ule angeweza kuwa mhaini wa wakati huu? Hapana mh!! Wale walioilinda katiba ndiyo hawa waliobeba jukuma la kuitupa leo,huu ni wakati sahihi kufanya hivyo! Na hata leo nikiitetea na kuipiganiaa katiba hii ili iendelee kuwepo nitaishia magereza mh! EAC ilikuwepo kwa wakati wake,ikavunjika kwa wakati wake na sasa ni wakati wa kuiunda upya!! Nothing out of ordinary Mh,kama ungependekeza Maalim seif ahukumiwe kwa dhambi ya ridhaa za walio wengi,mimi ningependekeza wale waliovunja azimio la arusha kwa ridhaa yao peke yao si hata wanyongwe,bali hata wanyooshewe kidole!!kina warioba nao wahukumiwe kwa kusimamia zoezi waliloapa kutolifanya,na wewe @Nape uhukumiwe kwa dhamira yako ya kale ya kuahini chama cha baba yako na kutaka kuanzisha chama chako.alamsik
 
Kumbe umeanza kugundua hiyo ndo kazi ya CCM,MAJUNGU NA KUCHONGEANA.Hana tofauti na wewe unachokifanya leo kubamba watu kesi za ugaidi.Mnatofautiana kwa moja tu:wawa yeye alijitambua na kuamua kuondoka CCM,wewe na Chemba mmeenda hatua ya juu zaidi yaani kung"oa watu kucha,kulipua mabomu n.k.
 

Lengo na nia ya Maalim Seif kumshtaki Rais wake kwa Mwalimu ilikuwa ni kutafuta huruma ya Mwalimu ili amteue awe Rais wa Zanzibar.
Inasikitisha huyo huyo Maalim Seif anakula matapishi yake.
Maalim Seif anatakiwa ashtakiwe na wananchi kupitia kwenye sanduku la kura, kwanza kuanzia kwenye chama chake hata kabla hajafika kwenye sanduku la uchaguzi mkuu!
Nchi nyingine anatakiwa apigwe Risasi hadharani kwa unafiki wake!!!

Baada ya kuona hoja za CHADEMA kuhusu serikali tatu ina mashiko kaanza kudandia hoja za wenzake!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…