Mshindi wa BBA Idris

Mshindi wa BBA Idris

Steph Curry

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
5,936
Reaction score
4,713
Mnamo tarehe 11.12.2014 Big Brother Africa ilipata mshindi mpya wa season 8, na mshindi hiyo alitokea Tanzania akijulikana kwa jina Idris Sultan. Mshindi alijishindia $ 300,000 takribani Million 500 za kibongo..

Tangia ametoka kwenye nyumba wengi walisubiri waone ni kipi atakifanya na hiyo pesa.. Lakini kijana kajibu mapigo, kaja na clothing line business.. Hii idea yake imebishangaza sana na ikabidi nijiulize maswali kadhaa;

1. Is his idea viable?? Yaani pamoja na kupata mkwanja mrefu hivo ameishia kufikiri that low....

2. Kuna clothing line (brand) yeyote ya Africa inayojulikana na yenye nguvu sokoni??

3. Mwaka jana mshiriki mwenzake Army Nando alivyotolewa pia alianzisha ya kwake, naweza kusema Nando alikuwa anapendwa na alikua na fans wengi kuliko Idris Lakini hizo T-shirt aliishia kuvaa mwenyewe na hiyo biashara yake haipo tena..

Watanzania lazima tujifunze kuwa creative na tufanye research kabla ya kuanzisha biashara yoyote. Asione ana fans wengi huko kwenye mitandao ya kijamii akajua ashapata uhakika wa soko lake.


Wadau mbalimbali walimshauri alivyopata hizo pesa arudi kwao Arusha au atafute mji wowote unaukuwa kiuchumi kama Mwanza, Mtwara, Dodoma, Mbeya akafanye investment huko. Lakini naona kaamua kukomaa na jiji... Kazi kwake

idris ed.png
 
Sidhani kama unamtendea haki huyo Mshindi wa BBA 2014 Ndg. Idris maana kwa mawazo yake hilo ndo anaona atafanikiwa la muhimu ni kumuunga mkono kwenye business (kama na wewe Unajiweza KIUCHUMI), halafu, hapo si mwisho wa Mawazo yake anaweza kuja na kipya/creativity nyingine, binafsi ile tu kununua nyumba na gari la kawaida nimemuona ana akili ya maisha angekuwa mwingine angeishia kuwa*** wakina Sepetua na wengineo na kusafiri kila kona ya Dunia. Tumpe Muda kijana anaonekana ni mwenye upeo, after all hata akila hela yote inakuuma nini? Hela si yake?
 
Money follow business and not otherwise! When you have money and not entrepreneurship in your blood just by assets like houses and land!
 
secrete

Hela ni zake, wacha afanye yake. tutafute zetu tufanye yetu.

DON FRANCIS
 
Last edited by a moderator:
Nilimsikia akijinadi kuwa anategemea kuwa Billionea kijana siku si nyingi na kwamba atafungua makampuni kibao,we wish him all the best,ingawa easy said than done.

Alisema atafika Hollywood kabla ya miaka mitatu.. Lakini cha kushangaza kawaponda Bongo Movie na kasema hayuko tayari kufanya nao kazi kwasababu kazi zao hazieleweki.. Nilifiki angetumia ujuzi aliofundishwa kule ndani kuwatengeneza bongo movie pamoja na kuinua sanaa yetu.. Sasa sujui atafikaje huko Hollywood
 
Ndg. Idris seems ana akili ya maisha tofauti na mastaa wengi wa Bongo (Diamond excluded). Mbali na hivyo akiamua kula/kuto.mbea hela yote ni Sawa tu,hakuna kesi
 
Ametokelezea kwenye video mpya ya ommy dimpoz-Wanjera,akiwa yeye,Wema na Pettyman.
 
secrete

Tofautisha maneno na utendaji.. Richard aliongea mengi mazuri ambayo alitarajia kuyafanya. Yuko wapi sasa??

Ni kweli pesa ni zake na wala hazituhusu ila tutaonekana watanzania ni hopeless kama huyu nae akifail.. Look at Mwisho and Richard.. Sipendi Idris nae apotee kama hao, ukuzingatia bado ni Kijana mdogo. Lakini pia huwezi shinda million 500 ukabaki na marafiki kama Wema, Lulu, Ommy Dimpoz ukajidanganya utaendelea.. Wakati huu pia aangalie company ya marafiki wenye mawazo chanya
 
Last edited by a moderator:
Pesa hiyo angejenga uswahilini
nyumba za kutosha za hali ya chini.
Kila mwisho wa mwezi angekuwa na uhakika
wa kuingiza senti.
Na kwa baadae angekaa kibarazani kajifunga
msuli anakula kichwa cha samaki mkavu
ghahwa, kashata na tende.
''Life is criminal''

 
Pesa hiyo angejenga uswahilini
nyumba za kutosha za hali ya chini.
Kila mwisho wa mwezi angekuwa na uhakika
wa kuingiza senti.
Na kwa baadae angekaa kibarazani kajifunga
msuli anakula kichwa cha samaki mkavu
ghahwa, kashata na tende.
''Life is criminal''


Yeye kanunua bangalow kule Africana na kukimbilia kupost kwenye mitandao.. Wahindi wana multi-million deals hapa mjini lakini yupo National Housing. Ukimwona muhindi kajenga nyumba au kanunua aishi ujue huyo ana billions nyingi kwenye account yake..

Kama alikua anataka kukaa sehemu nzuri na usafiri mzuri million 50 pekee ingemtosha.. 21 years old kukaa kwenye jumba kama lile tena huna familia ni matumizi ya kipumbavu
 
Pesa hiyo angejenga uswahilini
nyumba za kutosha za hali ya chini.
Kila mwisho wa mwezi angekuwa na uhakika
wa kuingiza senti.
Na kwa baadae angekaa kibarazani kajifunga
msuli anakula kichwa cha samaki mkavu
ghahwa, kashata na tende.
''Life is criminal''

miradi ya kivivu.
 
Sidhani kama unamtendea haki huyo Mshindi wa BBA 2014 Ndg. Idris maana kwa mawazo yake hilo ndo anaona atafanikiwa la muhimu ni kumuunga mkono kwenye business (kama na wewe Unajiweza KIUCHUMI), halafu, hapo si mwisho wa Mawazo yake anaweza kuja na kipya/creativity nyingine, binafsi ile tu kununua nyumba na gari la kawaida nimemuona ana akili ya maisha angekuwa mwingine angeishia kuwaTIA wakina Wema Sepetua na wengineo na kusafiri kila kona ya Dunia. Tumpe Muda kijana anaonekana ni mwenye upeo, after all hata akila hela yote inakuuma nini? Hela si yake?


Ila nyumba kwa habari za kitaa ile sio yake ni kuwa kapewa aishi na yule jamaa mmiliki wa HSC
 
Pesa hiyo angejenga uswahilini
nyumba za kutosha za hali ya chini.
Kila mwisho wa mwezi angekuwa na uhakika
wa kuingiza senti.
Na kwa baadae angekaa kibarazani kajifunga
msuli anakula kichwa cha samaki mkavu
ghahwa, kashata na tende.
''Life is criminal''


Hahaha
 
Pesa hiyo angejenga uswahilini
nyumba za kutosha za hali ya chini.
Kila mwisho wa mwezi angekuwa na uhakika
wa kuingiza senti.
Na kwa baadae angekaa kibarazani kajifunga
msuli anakula kichwa cha samaki mkavu
ghahwa, kashata na tende.
''Life is criminal''

Wazo zuri ila ni mawazo ya sie tunaoogopa kufeli
 
Ndg. Idris seems ana akili ya maisha tofauti na mastaa wengi wa Bongo (Diamond excluded). Mbali na hivyo akiamua kula/kuto.mbea hela yote ni Sawa tu,hakuna kesi

kwanini huyo unam-exclude?
 
Pesa hiyo angejenga uswahilini
nyumba za kutosha za hali ya chini.
Kila mwisho wa mwezi angekuwa na uhakika
wa kuingiza senti.
Na kwa baadae angekaa kibarazani kajifunga
msuli anakula kichwa cha samaki mkavu
ghahwa, kashata na tende.
''Life is criminal''


500m unafikiri atapata chumba na sebule ngapi?! Itamchukua miaka mingi sana kurejesha hiyo pesa.
mimi naona yuko sahihi, sidhani kama mayai yake yote ameyaweka kwenye kapu moja.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom