Mshike mkono mwenzako

Shilingi ngapi kwanza zipo tayari kutolewa?
Sasa hata haujasema, huyo sponsor ni kwa ajili ya nini, unaulizia kiwango cha pesa.
Je, ni sponsor wa biashara(mradi) au unataka kusoma Phd eenh!
 
Sasa hata haujasema, huyo sponsor ni kwa ajili ya nini, unaulizia kiwango cha pesa.
Je, ni sponsor wa biashara(mradi) au unataka kusoma Phd eenh!

Hahaaa mkuu hawa watu wa hivi huwa wanatoa kiwango maximum cha kiasi gani kiko available..halafu watu ndio wanajiongeza..sio mtu aseme kwa ajili ya nini kumbe hela yenyewe hakuna,lol
 
Daktari wa meno AKA mtanesco ndio ndio
Mimi ni Daktari wa Meno, nafanya kazi usafi majumbani kwa watu, nimeanza shughuli hii yapata miaka 7 na ninahudumia familia ya watoto 4 na wategemezi wengine 7.

(Nitakusaidia kutangaza kazi yako ila iwe ya kipekee)
 
Mkuu angalizo,kuna watu wamekata tamaa sana ya maisha na wapo humu,wakiona hili bandiko lako watakutafuta wakitumaini kuona mwanga tena. Kama unafanya mzaha hii dhambi utafunga nayo mwaka na kufungua nayo pia,inshort usijekuwa unajitafutia laana kuwa makini
 
Nitoe shukrani kwa wote mliopata kuweka michango yenu kwenye huu uzi. Japo nimesikitika kwa jinsi ambavyo tumebeba kila kitu katika mzaha ambao mwisho wa siku hauna msaada wowote kwetu.

Nina nafasi ya kuinua mtu kwa kumsaidia kutangaza kile ambacho anafanya tena bure BILA HATA KUNIPA SENTI YAKE. Nakuja kazini kwako kwa gharama zangu na muda wangu ila bado tupo kwenye jamii yenye watu aina ya buibui wasiopenda kuona mtu mwingine akiinuka.

Nimepata kukutana na wanawake wawili ambao ilibidi niongee nao kwa namna walivyokuwa na uthubutu kwa kufanya kazi ambazo wengine hawawezi kufanya hasa wanaume ila wanawake hawa waliweza na kuendelea kutunza familia zao kupitia kazi zao.

Wote ambao mmetoa kejeli zenu niwashukuru.
 
Twende twende twende kuna jamaa hapa wanafanya comedy ya kimya kimya maana ni mabubu,, wakamate mikono wanaitaji media coverage
Hii comedy wanafanya kwa vitendo au inakuwaje. Wapo wapi hawa vijana.
 
Mkuu, hakuna jambo la kipekee chini ya jua. Lolote linalofanywa ujue kuna watu waliwahi kulifanya hapo kabla.

Labda ungeanza kwa kutoa maana halisi ya huo upekee unaomaanisha wewe.
Jambo la kipekee ni lile ambalo ukiliona lazima litakuacha na mshangao kidogo. Kuna kipofu mmoja nasikia anashona nguo huyu mtu anafanya jambo la kipekee. Nazungumzia masuala ya aina hii.

Wajasiriamali wanaofuga mende wameanza kujaa Tanzania, huu ufugaji wa mende jamii inatamani kujua una manufaa gani kwao.
 
Sitafuti watu waliokata tamaa na maisha, natafuta watu wenye kujihusisha na kazi ambazo wengi wetu hatujui kama zipo na hata kama tunajua ila kuna vitu ambavyo tungepata kujua zaidi kutoka kwao.

Nimetoa mfano sehemu kwa sasa Tanzania inaendelea kupata wafugaji wa mende. Najua wewe au mtu mwingine yule anatamani kujua ufugaji wa mende unafanyika vipi na faida ni ipi.
 
Nachezesha karata
 
M Mkuu ungeelezea au kufafanua Kama ulivyofafanua hapa watu wasingetania
 
Ndugu mganga Daktari wa Meno mimi nipo arusha na ninajishugulisha na upigaji wa picha mahali mbalimbali hapa arusha, nakutana na watu wa aina tofauti kutokana na kazi ya siku hiyo, hebu nipe muongozo kuanzia hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…