Mshahara unaweza kujenga utajiri!

Mshahara unaweza kujenga utajiri!

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
16,099
Reaction score
24,335
JE,INAWEZEKANA KUJENGA UTAJIRI WA VIZAZI KWA MSHAHARA WA SERIKALI?.

Ndiyo! Inawezekana kabisa. Hapa, tunaamini kujenga utajiri hakutegemei pekee ukubwa wa mshahara unaoingiza mwisho wa mwezi,bali nidhamu yako ya kifedha, mipango ya muda mrefu na mkakati thabiti wa kuwekeza.
Hebu tuangalie mchanganuo huu kwa mtumishi anayeingiza TZS 1,000,000 (Take-home) kwa mwezi

KANUNI ZA KIFEDHA ZA KUJENGA MTAJI.
Ili kutoboa lazima uwe na nidhamu
🎯 Jilipe Kwanza (Pay Yourself First)
Tenga hela ya uwekezaji kabla ya matumizi mengine yoyote!
🎯Kanuni ya 50/30/20 Gawanya mshahara wako hivi:
• 50% (TZS 500,000) ➡️ Mahitaji ya msingi.
• 30% (TZS 300,000) ➡️ Matumizi binafsi.
•20%(TZS 200,000)▶️ Uwekezaji Hili ndilo fungu la utajiri wa vizazi!.

📌 WAPI PA KUWEKEZA HIYO LAKI 2?
Ili kushinda mfumuko wa bei ambao NBS inaonyesha ni wastani wa 3% - 4%,wekeza kwenye

🎯Hati Fungani za Serikali (BOT)
Zinatoa faida ya 12% mpaka 15% kwa mwaka.
Usalama ni wa uhakika!

🎯Soko la Hisa (DSE)
Fanya Quality Investing kwenye makampuni yenye misingi imara yanayotoa gawio Mfano Sekta za Benk na Mawasiliano.
Utapata faida ya ongezeko la thamani na gawio.

🎯NGUVU YA RIBA JUMUISHI,COMPOUND INTEREST.
Kama utawekeza ile TZS 200,000 kila mwezi kwa miaka 20 kwenye uwekezaji unaokupa 12% kwa mwaka
💰Pesa uliyotoa mfukoni mwako kwa miaka 20 = TZS 48,000,000 tu!
🔥 Faida iliyozalishwa na soko = TZS 149,850,000
🎯 JUMLA KUU = TZS 197,850,000
Karibu Milioni 198!

Huu ni mtaji mkubwa unaotosha kuanzisha miradi mikubwa katika sekta zisizo za kibenk,non-banking investments na kuwarithisha wanao mali zisizohamishika! Unaweza pia kuharakisha safari hii kwa kuwa na vyanzo vya ziada vya mapato vinavyosimamiwa kwa tija kama vile kilimo au ufugaji makini nk.
Tushare Tujifunze pamoja.
Copied.
 
Utajir sio mshahara au pesa uzipatazo utajir ni matokeo ya fikra na ubunifu kipawa chako nina jamaa yangu yeye alibahatika kupata milion mia sita za madin na iliishia bar na hatukuwah kumwita tajir
 
Kwa afrika akuna tajir anaelipwa mshahara kama wapo au yupo bas ni mt wa 10%,fisadi au mtu ya diri uko ofisini(rushwa)
 
Mshahara haujawai kumfanya mtu awe tajiri wewe unless kama hujaoa hapo saw
Muulize swali moja tu kwa mfano amepokea mshahara akahifadhi pesa yake benki kwa kutumia hiyo kanuni yake let say kuna 300k kwenye akaunti halafu anapigiwa simu mkwe au mjomba anaumwa hoi bin taabani inahitajika 250k kwa ajili ya matibabu na yeye peke yake ndio mwenye uwezo wa kipesa kwa wakati huo je atalipia hizo gharama au atakataa mkwe au mjomba afe tu?
Mwisho wa siku utagundua kwamba hizi kanuni hazipo applicable Bongo ziliandaliwa kwa mazingira ya Ulaya ambapo kila mtu anabeba msalaba wake hakuna kutegemeana.
 
Back
Top Bottom