Habari zenu wadau, niko nimekaa hapa nawaza naona salio limesoma inaonekana salary imeingia.
Najaribu kuona mgawanyo ili mambo yaende ila daah naona nooo...kuna harusi, kilaji, sadaka (zaka), bills la maji umeme vocha etc. Baada ya kuwaza sana nimegundua mshahara sio wa kuhonga, unaweza pata laana.
Ni bora kama una deal
Ngingine uhonge lakini sio mshahara, kumbuka kuna watu wamejinyima sana ili usome, mkeo/mmeo, watoto wanajua unaenda kazini. Kiroho ni kama unaenda nao na unafanya nao kazi, sasa unaanzaje kuhonga mshahara?
Laana nyengine tunajitakia wenyewe tu, we sadaka hutoi, mkeo analalamika kila
Siku, mama ako yuko bush, alafu unapata ujasiri wa kutuma 80,000 ya keki ya b/day haaaaa!
Kuanzia leo sihongi mshahara potelea potee