Uchawi: Nguvu ya uchawi na uwezo wa kuloga, jua kwanini unalogwa na kuchezewa

simon2016

Senior Member
Oct 19, 2020
148
500
Basi kwa neema na baraka zake Mungu baba alie juu mbinguni mahali patakatifu ahimidiwe kwa busara na hekima zake kwa uhai aliotujalia na afya na anijalie niandike vyema ili kusudi langu lieleweke, Kuna jambo katika mambo ambayo yapo, jambo ambalo ni dogo katika mengi ambayo kwangu nimeyaona na kuamini katika hayo kuhusu uchawi.

Nitasema kuhusu nguvu ya uchawi na uwezo wa kuloga kwa nafasi niliyoshudia na kugundua kwa miaka yangu hii michache niliopata kuishi toka nijitambue kwa upana, hili jambo ni muhimu na si la mzaha hata kidogo.

Nitaanza na kukili kuwa uchawi upo duniani kote tena hapa bongo upo mwingi sana mbwa kila siku hawachoki kuwabwekea wakipita usiku saa sita, upo kwa karne na karne na utakuwepo sikuzote za maisha yetu kwa kutaka na bila kutaka.

"Mtanisamehe wenzangu kwa kunukuu hiki kifungu "

"Ufunuo 22:15 inasema hivi Huko nje wako mbwa, WACHAWI, na wazinzi, na wajuaji, na hao waabuduo sanamu , na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.

Baadhi ya mazoea ya kiuchawi ambayo watu hujihusisha sana nayo ni uaguzi na kuwasiliana na pepo kutia ndani unajimu, ubashiri wa kutumia namba, usomaji wa viganja, kuwasiliana na “wafu” na vilevile ulozi. Mazoea hayo yana historia ndefu, kwani mengi kati yake yalianzia Babiloni la kale (Isaya 47:1, 12, 13)

Inasema (12 Endelea basi na uganga wako, tegemea wingi wa uchawi wako. Wewe uliyapania hayo tangu ujana wako ukitumainia kwamba utafanikiwa au kusababisha kitisho kwa watu! 13 Wewe umejichosha bure na washauri wako. Basi, na wajitokeze hao wanajimu wakuokoe! Wao huzigawa mbingu sehemu sehemu, huzichunguza nyota na kubashiri kila mwezi yatakayokupata.) Kutoka Babiloni, mazoea ya uchawi yalienea kote katika ulimwengu wa kale na kutia mizizi katika tamaduni na jamii nyingi.

Nimenukuu ili kuaaminisha uchawi upo kwa wale ambao hawajawahi kutana na kadhia hii mpaka waamini labda wataamini kwa neno la bwana ili nitakolosema waelewe.

Nguvu za gizaa zinatumiwa na watu wenye maarifa maalumu yasiyo ya kisayansi katika jamii nyingi duniani (zikiwemo za Afrika, Asia, Ulaya n.k.), ingawa kuna tofauti nyingi kulingana na mahali au utamaduni.

SASA KWA NINI WANA NGUVU NA WANALOGA KWA MAFANIKO MAKUBWA.

Wameingia maagano na wakuu wa nguvu za giza kiasi wameweza kuwaangusha na kuuwa maelfuu ya watu kuna wengine ni watu wa Mungu na wameweza kuwachezewa watakavyo na kuwa acha katika majonzi, magonjwa, shida, mikosi na kubebewa nyota, hata akili wanachukua na kuvuruga kila walionalo wakiendeshwa na tamaa, wivu pamoja na chuki binafsi wao wakiona unaringa, unafaidi una raha n.k

Kwanza wachawi wanaasheria kali sana, hawana utu na wenye kufata sheria za Maagano yao na wanatekeleza vizuri kabisa sheria zao licha ya kua wachache wao hukwama ila wako vizuri.

Nguvu zao zipo kwenye damu, damu wanazomwaga ndio nguvu ya kwanza kuliko chochote kile halafu ndio yanafata mambo mengine ya mitishamba. Wachawi wanatoa sadaka wanauua watu, wanaua wanyama tena mara nyingi au kila mara, ili kufanikisha kazi zao.

Nataka kutoa mfano " Mtu akitaka kuloga au kuaguliwa lazima alete kimoja wapo kama ni mayai,nazi, njiwa, kuku, mbuzi , mtoto wa mtu, mtu baki au zaidi ili kutimiza lengo lake.

Basi sadaka anayotoa huwa ndio njia ya kufanya mambo yake yaende kwa kutumia majini, mashetani au mapepo kwenda kwa adui yake ambae ndo wewe " upo ofisini, sijui mwinjilisti, mwana jamii una maisha yako, upo kwenye gari, upo bafuni, unacheza mpira , umepumzika, au umelala usiku " kinatumwa kitu 'puuu" unacho.

TUJUE KWA NINI UNALOGWA NA KUCHEZEWA AU KUHARIBIWA MAMBO YAKO.

Kwanza kama huna msimamo husali, hulogi kotekote haupo wewe ni chakula cha wenzio. Hili kundi la watu hubebwa sana labdaa kama kwenu kuna mizimu mikali utapona na haya mawindo .

Mwinjilisti, mwana dini, askofu,padre mchungaji , hata kama una cheo gani upande wa dini hii vitaa ni yaa wote muda wote wapo kazini kuangusha waliojiwekea ngome za kiimani kwa sababu ndio wazuri zaidi na ndio wanaharibu kazi zao zaidi, hawa watu wakiangukia kwenye uzinzi,ulevi, uasherati hapo hapo wakinasa wanapigiwa haraka sana na kuharibu huduma, biashara, mafanikio hawa ni dhahabu muda wote wanatafutwa ndio sehemu ya kupandia cheo .

Sasa kama hujajizindika hesabu kulogwa na kuchezewa au kuharibiwa mambo yako muda wowote na ukizidiwa nguvu lazima yatakusibu.

KWA WALE WANAO TAKA KUTOLOGWA KABISA NA KUISHI KWA AMANI FANYA HAYA.

MTUMAINI MUNGU, Mungu ananguvu kuliko chochote kile hakuna kiwezacho akiweka mkono wake.

Toa sadaka na zaka " Et mtu analipwa mshahara wa laki 4, wengine laki 9 , wengine millioni 1 au zaidi anatoa
SADAKA mia mbili , mia tano, shilingi 100, anaomba Mungu amlinde na Mungu kweli anatulinda na choyo zetu, Muda huo huo unaenda bar unakula na kusaza unaacha elfu 50,laki moja, laki mbili halafu unasema utapata .
Wengine wanahonga nyumba , gari , malaki wanawapa malaya halafu nae anataka Mungu amtendendee makubwa zaidi binadamu tunakwama sana.

" Muda huo mtu kaenda kununua jini la millioni 2 akutumie likumalize, muda huo mtu katoa mbuzi ili ufe, muda huo mtu kachinja kuku ufe, muda huo mtu kavunja nazi kuharibu maisha yako.

Je utafua dafu kwa sadaka yako? Ili kuzuia kombora za maadui zetu.
Tujifunze kutoa sadaka ndugu zangu, tufunge tusali, umeenda mnadaani mmeangusha mbuzi si bora mchange mnunue mwingine aende kanisani, nunua vikuku viwili au kimoja peleka kanisani Watu wapo tayari kupeleka kuku kwa mganga lakini sio kanisani.

TUBADILIKE KWA KUTOA SADAKA NA ZAKA ZA MAANA NA KUSALI ILI KUWASHINDA ADUI ZETU HAWATUWEZI TUKIWEKEZA HUO UPANDE ILI KUKABILIANA NAO.

Mwisho siamini katika uganga lakini hivi vitu vipo na wanatibiana na kupona ila vikiwa chini ya nguvu za giza. Kwahiyo kama wanaweza kuloga basi hawezi kunshindwa kutegua wakilogana na Mungu hafungamani na haya mambo, mimi pia sifungamani na haya mambo ya uganga na uchawi.

Nawasilisha.

Mungu azidi kutulinda, Amina
 
Holy Man

JF-Expert Member
Feb 4, 2021
1,646
2,000
Soma neno la Mungu kwa bidii zaidi.
Utajua unamshinda vipi mchawi.

Utoaji wa Sadaka kanisani haukukingi na roho za kichawi.
Mchawi au shetani anamshambulia mtu anapokuwa na kitu chake ( inaweza ikawa dhambi, laana mambo manyonge yasiyo na utii kwa neno la Mungu etc ). Kama huna hivyo, hakuna mchawi wala shetani atae sogeza pua.. ndio kuna ile statement Yesu aliitoa na kuwambia shetani hana kitu kwangu;

** Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu. **
 
Surya

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
6,155

Soma hapa itakusaidia, usipo elewa kitu, niulize swali.
Uzi huu 👇👇
 
Maova

Member
May 31, 2019
20
45
Hiv sadaka ni tu kupeleka kanisani, kwa mfano: nikimyima jirani yangu hela ya chakula siku hiyo na kuileta kanisani ni sawa? Msaada mkuu hapo.
 
Holy Man

JF-Expert Member
Feb 4, 2021
1,646
2,000
Haya yote nayajua. Kama hujaelewa point chache niliyo andika hapo, waweza niuliza pia nikakueleza nini namaanisha. Mashambulizi hutokana na kilichomo ndani ya mtu, kama ndani una nuru tupu hakuna shambulizi mtu anapata, ila kama mtu ndani mixer shetani au mchawi anapata mlango kupitia hilo hilo giza
 
Tuko pamoja Holy Man

Nina swali nje kidogo, ukinipa majibu nadhani yatanijenga zaidi.

Katika maisha ya usafi, yani kutokutenda chambi, wewe umeishinda dhambi kabisa ?

Kama uliwahi kua mwenye dhambi, uliwezaje kuacha dhambi ile iliyo kuteka hapo mwanzo, na kuanza maisha ya usafi ? nipe siri ya mafanikio yako.
 
- Hakuna mwanadamu mwenye uwezo wa kuishinda dhambi isipokuwa yupo mmoja tu alie ifia dhambi. Ushindi wangu katika dhambi unakaa katika kile ambacho Yesu alikifanya msalabani. Ila kuna maisha ( asili ya mwili na taarifa zilizopo katika nafasi ) bado naendelea kuzibadiri kwa neno la Mungu ( ku renew mind by His word ). Nikikaa katika nafasi ambayo Yesu ameniweka nitakujibu nimeshinda dhambi kabisa, si ushindi wangu bali ni ushindi wa Kristo. Ila Nayabiri maisha yangu asili kwa uwezo wa neno la Mungu ili ku fit alicho nishindia Yesu. Ulinzi wangu 100% damu ya Yesu Kisto ila ina work kama kuna utii.

Maisha ya dhambi ( zile tabia zilizo sababishwa na dhambi ikaingia ndani yangu ), ni kitu endelevu kuzishinda na kuzibadili, njia pekee ambayo naitumia ni kubadilisha mazingira, na kuomba kilq iitwapo leo Roho wa Mungu aniondolee vinamvyo muuzuniasha. Maombi na Neno ndio vinapiga nguzu za kuacha zile asili ( tabia za dhambi kila iitwapo leo ). Ni process bado namlilia Mungu zaidi katika maombi ili Nira yake ichukue nafsi zote katika mwili na nafsi
 
Sasa nikisema mimi nishetani...
Nakuvizia nataka nikuangamize, kwa kukuvizia muda ukitenda dhambi tu, nitakukamata najua, muda ukijikwaa tena kwenye dhambi, kwani bado unapambana kuyafanya mapenz ya Mungu kikamilifu.
Na nitakumaliza.

Au tuseme.

Sita weza kukuangamiza kwani wewe umeshika chenye nguvu, unayo imani katika Yesu kristo.
 
Surya

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
6,155
2,000
Hiv sadaka ni tu kupeleka kanisani, kwa mfano: nikimyima jirani yangu hela ya chakula siku hiyo na kuileta kanisani ni sawa? Msaada mkuu hapo.
Mahubiri yanayozungumzia jinsi ya kumtolea Mungu sadaka, yanaweza chukua hata masaa 6 na zaidi hadi mtu kuelewa.

Kama unahitaji kumjua Mungu zaidi.
Weka juhudu sana katika kujifunza neno lake, kwa kusoma biblia wewe binafsi na kusikiliza mahubiri.
 
Emmanuel Kasomi

Verified Member
Oct 18, 2019
3,100
2,000
Basi kwa neema na baraka zake Mungu baba alie juu mbinguni mahali patakatifu ahimidiwe kwa busara na hekima zake kwa uhai aliotujalia na afya na anijalie niandike vyema ili kusudi langu lieleweke, Kuna jambo katika mambo ambayo yapo, jambo ambalo ni dogo katika mengi ambayo kwangu nimeyaona na kuamini katika hayo kuhusu uchawi.

Nitasema kuhusu nguvu ya uchawi na uwezo wa kuloga kwa nafasi niliyoshudia na kugundua kwa miaka yangu hii michache niliopata kuishi toka nijitambue kwa upana, hili jambo ni muhimu na si la mzaha hata kidogo.

Nitaanza na kukili kuwa uchawi upo duniani kote tena hapa bongo upo mwingi sana mbwa kila siku hawachoki kuwabwekea wakipita usiku saa sita, upo kwa karne na karne na utakuwepo sikuzote za maisha yetu kwa kutaka na bila kutaka.
" Mtanisamehe wenzangu kwa kunukuu hiki kifungu "

"Ufunuo 22:15 inasema hivi Huko nje wako mbwa, WACHAWI, na wazinzi, na wajuaji, na hao waabuduo sanamu , na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.

Baadhi ya mazoea ya kiuchawi ambayo watu hujihusisha sana nayo ni uaguzi na kuwasiliana na pepo kutia ndani unajimu, ubashiri wa kutumia namba, usomaji wa viganja, kuwasiliana na “wafu” na vilevile ulozi. Mazoea hayo yana historia ndefu, kwani mengi kati yake yalianzia Babiloni la kale (Isaya 47:1, 12, 13)

Inasema (12 Endelea basi na uganga wako, tegemea wingi wa uchawi wako. Wewe uliyapania hayo tangu ujana wako ukitumainia kwamba utafanikiwa au kusababisha kitisho kwa watu! 13 Wewe umejichosha bure na washauri wako. Basi, na wajitokeze hao wanajimu wakuokoe! Wao huzigawa mbingu sehemu sehemu, huzichunguza nyota na kubashiri kila mwezi yatakayokupata.) Kutoka Babiloni, mazoea ya uchawi yalienea kote katika ulimwengu wa kale na kutia mizizi katika tamaduni na jamii nyingi.

Nimenukuu ili kuaaminisha uchawi upo kwa wale ambao hawajawahi kutana na kadhia hii mpaka waamini labda wataamini kwa neno la bwana ili nitakolosema waelewe.

Nguvu za gizaa zinatumiwa na watu wenye maarifa maalumu yasiyo ya kisayansi katika jamii nyingi duniani (zikiwemo za Afrika, Asia, Ulaya n.k.), ingawa kuna tofauti nyingi kulingana na mahali au utamaduni.

SASA KWA NINI WANA NGUVU NA WANALOGA KWA MAFANIKO MAKUBWA.

Wameingia maagano na wakuu wa nguvu za giza kiasi wameweza kuwaangusha na kuuwa maelfuu ya watu kuna wengine ni watu wa Mungu na wameweza kuwachezewa watakavyo na kuwa acha katika majonzi, magonjwa, shida, mikosi na kubebewa nyota, hata akili wanachukua na kuvuruga kila walionalo wakiendeshwa na tamaa, wivu pamoja na chuki binafsi wao wakiona unaringa, unafaidi una raha n.k

Kwanza wachawi wanaasheria kali sana, hawana utu na wenye kufata sheria za Maagano yao na wanatekeleza vizuri kabisa sheria zao licha ya kua wachache wao hukwama ila wako vizuri.

Nguvu zao zipo kwenye damu, damu wanazomwaga ndio nguvu ya kwanza kuliko chochote kile halafu ndio yanafata mambo mengine ya mitishamba. Wachawi wanatoa sadaka wanauua watu, wanaua wanyama tena mara nyingi au kila mara, ili kufanikisha kazi zao.

Nataka kutoa mfano " Mtu akitaka kuloga au kuaguliwa lazima alete kimoja wapo kama ni mayai,nazi, njiwa, kuku, mbuzi , mtoto wa mtu, mtu baki au zaidi ili kutimiza lengo lake.

Basi sadaka anayotoa huwa ndio njia ya kufanya mambo yake yaende kwa kutumia majini, mashetani au mapepo kwenda kwa adui yake ambae ndo wewe " upo ofisini, sijui mwinjilisti, mwana jamii una maisha yako, upo kwenye gari, upo bafuni, unacheza mpira , umepumzika, au umelala usiku " kinatumwa kitu 'puuu" unacho.

TUJUE KWA NINI UNALOGWA NA KUCHEZEWA AU KUHARIBIWA MAMBO YAKO.

Kwanza kama huna msimamo husali, hulogi kotekote haupo wewe ni chakula cha wenzio. Hili kundi la watu hubebwa sana labdaa kama kwenu kuna mizimu mikali utapona na haya mawindo .

Mwinjilisti, mwana dini, askofu,padre mchungaji , hata kama una cheo gani upande wa dini hii vitaa ni yaa wote muda wote wapo kazini kuangusha waliojiwekea ngome za kiimani kwa sababu ndio wazuri zaidi na ndio wanaharibu kazi zao zaidi, hawa watu wakiangukia kwenye uzinzi,ulevi, uasherati hapo hapo wakinasa wanapigiwa haraka sana na kuharibu huduma, biashara, mafanikio hawa ni dhahabu muda wote wanatafutwa ndio sehemu ya kupandia cheo .

Sasa kama hujajizindika hesabu kulogwa na kuchezewa au kuharibiwa mambo yako muda wowote na ukizidiwa nguvu lazima yatakusibu.

KWA WALE WANAO TAKA KUTOLOGWA KABISA NA KUISHI KWA AMANI FANYA HAYA.

MTUMAINI MUNGU, Mungu ananguvu kuliko chochote kile hakuna kiwezacho akiweka mkono wake.

Toa sadaka na zaka " Et mtu analipwa mshahara wa laki 4, wengine laki 9 , wengine millioni 1 au zaidi anatoa
SADAKA mia mbili , mia tano, shilingi 100, anaomba Mungu amlinde na Mungu kweli anatulinda na choyo zetu, Muda huo huo unaenda bar unakula na kusaza unaacha elfu 50,laki moja, laki mbili halafu unasema utapata .
Wengine wanahonga nyumba , gari , malaki wanawapa malaya halafu nae anataka Mungu amtendendee makubwa zaidi binadamu tunakwama sana.

" Muda huo mtu kaenda kununua jini la millioni 2 akutumie likumalize, muda huo mtu katoa mbuzi ili ufe, muda huo mtu kachinja kuku ufe, muda huo mtu kavunja nazi kuharibu maisha yako.

Je utafua dafu kwa sadaka yako? Ili kuzuia kombora za maadui zetu.
Tujifunze kutoa sadaka ndugu zangu, tufunge tusali, umeenda mnadaani mmeangusha mbuzi si bora mchange mnunue mwingine aende kanisani, nunua vikuku viwili au kimoja peleka kanisani Watu wapo tayari kupeleka kuku kwa mganga lakini sio kanisani.

TUBADILIKE KWA KUTOA SADAKA NA ZAKA ZA MAANA NA KUSALI ILI KUWASHINDA ADUI ZETU HAWATUWEZI TUKIWEKEZA HUO UPANDE ILI KUKABILIANA NAO.

Mwisho siamini katika uganga lakini hivi vitu vipo na wanatibiana na kupona ila vikiwa chini ya nguvu za giza. Kwahiyo kama wanaweza kuloga basi hawezi kunshindwa kutegua wakilogana na Mungu hafungamani na haya mambo, mimi pia sifungamani na haya mambo ya uganga na uchawi.

Nawasilisha.

Mungu azidi kutulinda, Amina
Ngoja nijisaniteze nivae na barakoa ili nisome kwa uzuri uzi huu
 
Holy Man

JF-Expert Member
Feb 4, 2021
1,646
2,000
Sasa nikisema mimi nishetani...
Nakuvizia nataka nikuangamize, kwa kukuvizia muda ukitenda dhambi tu, nitakukamata najua, muda ukijikwaa tena kwenye dhambi, kwani bado unapambana kuyafanya mapenz ya Mungu kikamilifu.
Na nitakumaliza.

Au tuseme.

Sita weza kukuangamiza kwani wewe umeshika chenye nguvu, unayo imani katika Yesu kristo.
Dhambi ni mlango, na ukiangalia vizuri dhambi inatabia ya kukua na kuzaa hata mauti kwa lugha nyingine dhambi ina stage (level). Mtu anapokosea tu mwenye kumjua Mungu, anajua na anae shuhudiwa na Roho Mtakatifu hutubu mda huo huo. Ila kuna mazoe ya dhambi na ndio dhambi ifuanguayo milango ya mashambulizi, inafikia hatua mtu hatubu hata kama ana shuhudiwa. So: aliepo ndani yangu ( Yesu kristo kupitia Roho wake mtakatifu ) ni mkuu kuliko wa ulimwengu huu, by that point shetani hana huwezo wa kuniangamiza.
 
Kwahiyo tukijibu upya swali hili,
Nawezaje kumshinda mchawi asiniroge ?

Ni kufanya hivi..

Kumpokea Yesu akae ndani yako.
(Yani Roho wake mtakatifu)

NADHANI NDIO JIBU BORA.
 
Holy Man

JF-Expert Member
Feb 4, 2021
1,646
2,000
Kwahiyo tukijibu upya swali hili,
Nawezaje kumshinda mchawi asiniroge ?

Ni kufanya hivi..

Kumpokea Yesu akae ndani yako.
(Yani Roho wake mtakatifu)

NADHANI NDIO JIBU BORA.
Upo sahihi 100%. Yesu Kristo ni Bwana na mwakozi wa kila jambo. Upo sahihi kabisa kabisa, bila Yesu Kristo moyoni mwa mtu, huyo mtu hana maisha, na kama hana maisha basi adui anafanya chochote kwa huyo mtu. 🤝🤝🤝.. Asate kwa kushare maarifa
 
Surya

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
6,155
2,000
Upo sahihi 100%. Yesu Kristo ni Bwana na mwakozi wa kila jambo. Upo sahihi kabisa kabisa, bila Yesu Kristo moyoni mwa mtu, huyo mtu hana maisha, na kama hana maisha basi adui anafanya chochote kwa huyo mtu. 🤝🤝🤝.. Asate kwa kushare maarifa
Nawe pia Asante.
Kristo azidi kuumbika ndani yako.

Hakika Yesu katufanyia wepesi.
Mathayo 11:29-30
[29]Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
[30]kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.
 
Holy Man

JF-Expert Member
Feb 4, 2021
1,646
2,000
Nawe pia Asante.
Kristo azidi kuumbika ndani yako.

Hakika Yesu katufanyia wepesi.
Mathayo 11:29-30
[29]Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
[30]kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.
Amen.
 
keisangora

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
1,624
2,000
Yaani mie nimeelewa kuwa unataka watu watoe sadaka.
Kulindwa sio lazima utoe sadaka. Inaonekana unaumia sana watu wanapohonga nyumba Magari kuna mmoja akajengewa ghorofa na akapewa viti maalumu hapo unasemaje. Ila ni tetesi hii
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom