Mshahara na pesa za kujikimu ajira mpya za walimu 2017

Abuwhythum

JF-Expert Member
Jan 7, 2015
837
495
Ukweli ni kwamba Halmashauri nyingi hazijatoa pesa ya kujikimu kwa walimu wapya wa Sayansi na Hisabati walioajiriwa na Serikali mwezi uliopita (APRIL 2017)
Hali ni tete sana, ila cha kushangaza sioni malalamiko makubwa kama ilivyokuwa kipindi kile ajira zimecheleweshwa kwa sababu za uhakiki ambao ulichukua takriban mwaka mzima. Sasa sielewi ni sababu ipi kati ya hizi inasababisha :

1. Wanaogopa kutumbuliwa?

2. Wamepangiwa vijijini sana ambako mtandao wa internet ni shida (hivyo hawawezi kuchangia kwa njia ya mtandao kama ilivyokuwa awali)?

3. Ndo wameishiwa kabisa hata pesa ya kununulia vocha kwa ajili ya kupata access ya mtandao hawana?

4. Au wamebaini dhahiri kuwa kulalamika kwenye mtandao hukusaidii lolote maana kipindi kile wanasubiri ajira walilalamika sana pasina mafanikio yoyote!
 
Mnaumwa ugonjwa wa kulalamika, yaani mnataka kufanya malalamiko kama 7ehemu ya maisha kwamba watu lazima walalamike
 
Naongea kwa masikitiko kwani baadhi ya halmashauri mpaka sasa hakuna pesa ya kujikimu wala mshahara hatujapata. Tunaomba wahusika kuarakisha swala hili wengine tunafamilia lakini cha kushangaza wanasema tusaidiwe na walimu wenyeji kila kitu kuanzia kula kulala dawa za miswaki na kadhalika.

Amakweli alieshiba hamjui mwenye njaa!
 
Mvumilivu hula mbivu, pole sana kwa kipindi unachopitia.. Tafuteni njia nyingine sahihi ya kuwasilisha malalamiko yenu..ila pia kupitia hapa watawasikieni pia
 
Jamani! Toka mwezi wa nne mshahara hamna, pesa ya kujikimu hamna ni zaidi ya siku hamsini kazini, hata mwezi wa tano waajiriwa wapya wamesahaulika tena kuwekewa mshahara!
Huruma ichukue mkondo wake.
Siyo kila siku sheria ichukue mkondo wake
 
Kwa wenye familia mtaambiwa walimu wenyeji wahudumie hadi wake zenu! Ni hatari hii! Siyo masihara.
 
Jamani! Toka mwezi wa nne mshahara hamna, pesa ya kujikimu hamna ni zaidi ya siku hamsini kazini, hata mwezi wa tano waajiriwa wapya wamesahaulika tena kuwekewa mshahara!
Huruma ichukue mkondo wake.
Siyo kila siku sheria ichukue mkondo wake
Kwaiyo tufanye nini?

Tuko bize na mchanga wa madini, we shukuru umeingizwa kwenye system tu mambo mengine yatafuata
 
Ukweli ni kwamba Halmashauri nyingi hazijatoa pesa ya kujikimu kwa walimu wapya wa Sayansi na Hisabati walioajiriwa na Serikali mwezi uliopita (APRIL 2017)
Hali ni tete sana, ila cha kushangaza sioni malalamiko makubwa kama ilivyokuwa kipindi kile ajira zimecheleweshwa kwa sababu za uhakiki ambao ulichukua takriban mwaka mzima. Sasa sielewi ni sababu ipi kati ya hizi inasababisha :

1. Wanaogopa kutumbuliwa?

2. Wamepangiwa vijijini sana ambako mtandao wa internet ni shida (hivyo hawawezi kuchangia kwa njia ya mtandao kama ilivyokuwa awali)?

3. Ndo wameishiwa kabisa hata pesa ya kununulia vocha kwa ajili ya kupata access ya mtandao hawana?

4. Au wamebaini dhahiri kuwa kulalamika kwenye mtandao hukusaidii lolote maana kipindi kile wanasubiri ajira walilalamika sana pasina mafanikio yoyote!
Hivi sasa hivi mshahara wao ni kiasi gani ( BASIC SALARY)......?
 
Mshahara watu wanasubiri hata miezi mitatu, wewe wiki 2 umeshaanza kulia! acha kazi uone ilivyokazi kupata kazi.
Hadi unasema wiki mbili kwako wiki ni siku ngapi? Watu wapo kazini toka tarehe 18/04
 
Back
Top Bottom