Asante sana ndugu
Jodoki Kalimilo kwa kuona umuhimu wa info zangu kuhusu hili suala la ualimu.
Unajua mkuu Ualimu kama ualimu umegawanyika katika nyanja nyingi tu, na karibu Ofisi zote huwa na waalimu ndani yake...........
mwalimu si lazima mpaka ashike chaki kufundisha, la hasha....Ualimu ni kazi ya kitaaluma ambayo humtoa yule afundishwae na mwalimu
kutoka kutojua chochote mpaka kufikia level ya ufahamu na kujielewa.
Ni lazima upitie course ili uweze kufuzu utaalamu fulani......hata kama huko nyuma ulihitimu mpaka Degree.
Hata yule anaekusaili ni Mwalimu vile vile........tofauti yake ni kwamba pale huwa hashiki chaki wala kitabu....bali husema na CV zako na muonekano wako.
Wengi wenye upeo mdogo huidharau kazi ya ualimu na kuifananisha na Daraja lipitishalo watu kuelekea sekta nyingine.......hatukatai, ndio ni lazima mimi nikupitishe wewe Ally kutoka side A kwenda side B, C, D.....an so on ili uweze kufaidika na matunda nikupayo kwa kazi yangu hii.
Ila kama ulivosema mkuu, Raha ya hii kazi ni kujiendeleza,.......na si hii tu bali kazi yoyote ni lazima ujiendeleze ili uweze kufika mbali.
Binafsi....
I
Jodoki Kalimilo, mie ni mwalimu wa intake ya mwaka 2011, nanimekuta mfumo wa Draj IIIA......nadani Daraja la IIIB walikuwa wale wa enzi za UPE.
Asante.
Nakala kwa gfsonwin, snowhite, Evelyn Salt na Baba V.